Simuungi tena mkono Rais Samia kwa haya yanayoendelea na kadhia ya Mafuta

Simuungi tena mkono Rais Samia kwa haya yanayoendelea na kadhia ya Mafuta

Aisee!
Ndugu ukapimwe kama akili inafanya kazi ipasavyo.
Nitaendelea kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa siku zote.Nitakuwa upande wake,nitasimama naye popote alipo na kumtetea popote niwapo, nitasema kwa nguvu zangu zote mazuri yote anayoendelea kuyafanya katika Taifa letu.kila mtu anatambua dhamira njema aliyonayo mh Rais katika Taifa letu. Sote tumeona kazi kubwa aliyoifanya katika secta ya Elimu, Afya, miundombinu,kilimo n.k. Tumeona shule zilijengwa kila eneo,tumeona vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 20 vikijengwa,tumeona Elimu ikitolewa bure hadi kidato cha sita,tumeona vituo vya afya vikijengwa kila kona ya Taifa letu.Tumeona leo hii miradi mbalimbali ya maendeleo ikichipua kila sehemu .kwa hakika nitaendelea kuwa pamoja na Rais samia na serikali yake mpaka mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuwa nikimtetea Sana Rais Samia kwenye mambo mbalimbali. Hata kwenye issue ya DP world nilikuwa naona wanamuonea, nimesimama Daima kuona alifanya uamuzi sahihi

Kwa hakika alikuwa na Kura yangu ya kumsogeza mpaka 2030, lakini leo rasmi natangaza simuungi mkono tena na nimeona udhaifu wake.

Mafuta ya petrol na Diesel imekuwa mateso sasa Tanzania. Yaani Rais kashindwa simamia issue ndogo ya Mafuta tunapaki magari, na vyombo vya usafiri, mkoa mzima kuna Petrol station moja tu kwa takribani wiki na hakuna kauli iliotoka? Kwa hakika Mama nchi amepelea.

Nami naunga sasa mkono tutafute mwanaume tena aongoze nchi. Wanawake wameshafeli

Zile kauli za "Ninaomba mkalitazame na hili", nahisi ndio zimetufikisha hapa, mikoani huku petrol na Diesel hakuna. Vituo vya mafuta vimefungwa.

Hii ilitokea mwezi uliopita tukadhani ni bahati mbaya, imetokea na mwezi huu, tafsiri ni kuwa kila mwezi itatulazimu watu wa mikoni kupaki gari zetu kwa wiki moja au zaidi kukiwa hakuna mafuta, lakini pia tukitumia muda kupanga foleni masaa hadi kumi kupata mafuta kwenye station chache mathalani moja inauokuwa imebaki na akiba, na Serikali ipo.

Hivi sio hawa walituaminisha Serikali inatumia na kuagiza mafuta ya miezi mitatu nyuma? Leo wanaficha mafuta kusubiri bei zipande Raia tunaumia. Gari kutoka dar kufika bukoba, musoma, sumbawanga, songea tangu bei kupanda ni siku 3

Rais yupo na hatoi kauli, akitoa anasema naomba na hili mkalitazame...aisee..

Its a time, I'm no longer backing President Samia for Second term of Presidency. Tukomae tu na wanaime hata akiwa badhirifu kuna kuda anatoa Sauti ya Mamulaka
Hata mimi simuungi mkono tena.

Yeye mwenyewe alishuhudia mambo yasiyofaa awamu iliyopolita na huenda alikuwa mwathrika then anarudia yale yale?
 
Rais amezungukwa na Watu waovu kupitiliza, Tumuombee!
Hii ndiyo shida tuliyo nayo Tz. Na hili ni zao la Katiba iliyochakaa. Kilichonishagaza sana ni kwamba baada tu ya bei mpya kutangazwa vituo vyoote vikaanza kuuza mafuta. Hii inamaanisha nini? Wahusika wa usimamiaji wa maswala ya nishati hiyo ni watu wasiokua na maadili kiasi kwamba wanawataarifu wafanyabiashara mapema kwamba wanafanya mchakato wa kupandisha bei? Usalama wa nchi unaweza kuharibiwa na/au kuchafuliwa na tabia kama hizi. And they walk free?
 
Nitaendelea kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa siku zote.Nitakuwa upande wake,nitasimama naye popote alipo na kumtetea popote niwapo, nitasema kwa nguvu zangu zote mazuri yote anayoendelea kuyafanya katika Taifa letu.kila mtu anatambua dhamira njema aliyonayo mh Rais katika Taifa letu. Sote tumeona kazi kubwa aliyoifanya katika secta ya Elimu, Afya, miundombinu,kilimo n.k. Tumeona shule zilijengwa kila eneo,tumeona vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 20 vikijengwa,tumeona Elimu ikitolewa bure hadi kidato cha sita,tumeona vituo vya afya vikijengwa kila kona ya Taifa letu.Tumeona leo hii miradi mbalimbali ya maendeleo ikichipua kila sehemu .kwa hakika nitaendelea kuwa pamoja na Rais samia na serikali yake mpaka mwisho.
Hebu tutolee ujinga hapa
 
Mnamchukia Samia kisa ni muislam. Wakristo mna chuki sana na udini sana nchi hii
 
Mnamchukia Samia kisa ni muislam. Wakristo mna chuki sana na udini sana nchi hii
ALiyeanzisha msemo wa anaupiga mwingi ni Malisa ambaye ni mkristo kipindi anafanya vizuri, JPM alikuwa ni mkristo safi tena RC lakini RC walipinga kwa waraka tena mrefu, sema ulikuwa bado mtoto 2018, hatupo kupiga dini tupo kupiga maovu
 
Hii ndiyo shida tuliyo nayo Tz. Na hili ni zao la Katiba iliyochakaa. Kilichonishagaza sana ni kwamba baada tu ya bei mpya kutangazwa vituo vyoote vikaanza kuuza mafuta. Hii inamaanisha nini? Wahusika wa usimamiaji wa maswala ya nishati hiyo ni watu wasiokua na maadili kiasi kwamba wanawataarifu wafanyabiashara mapema kwamba wanafanya mchakato wa kupandisha bei? Usalama wa nchi unaweza kuharibiwa na/au kuchafuliwa na tabia kama hizi. And they walk free?
Ni aibu na hatari sn
 
Back
Top Bottom