Sina furaha kwenye ndoa yangu, nahisi nilikurupuka

Tajiri wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,079
Reaction score
2,947
Wakuu nakiri kabisa from heart ya kwamba hii ndoa yangu nilikurupuka sana yapata takribani mienzi minne ya ndoa yangu sina hisia ya mapenzi na nahisi kujuta sana kwenye maisha yangu na sina furaha kabisa.

Yaani sina furaha kabisa wakuu yaani najuta kuoa mwanamke wa chop money yaani yeye ni kula tu na kulala na ni mvivu sana na mbaya zaidi kinachoniuma nimetoa mahari nyingi sana lakini binti ni mvivu sana na nahisi majukumu yamenielemea kabisa.

Tafadhali naombeni ushauri wenu wakuu na nataka nimrudishe mazima kwao ili nikeep furaha yangu.

Msinipopoe wakuu
 
Pole sana mkuu.

Huwenda uliyaona hayo yote kabla ila ukajipa moyo atabadilika.
Hakunaga kubadilika kwenye ndoa zaidi ya kuwa mshenzi zaidi.

Yaani 95% ya watu ndoa inawabadilisha na kuwa washenzi zaidi.
So suala la kubadilika kwenye ndoa tusilichukukie poa.

Chagua mwenza mwenye tabia ambazo yuko nazo wakati huo ambazo unahisi utaziridhia kwenye ndoa akiwa nazo,then ishi naye, mbali na hapo ni betting.

Asante sana.
 
Ukiona muda wa breakfast mwanaume unawazia ndoa yako kweli umekamatika..

Pole mkuu ila jaribu kuongea nae kama ni muelewa maana naamini, hadi unafikia kumuoa, lazma ulikuwa na strong reasons za kufanya hivyo. Kwa hiyo katika sehemu uliyofikia ambayo unaliona dhaifu moja la mtu, usijisahaulishe mengine yote uliyoyaona kwa kulinganisha na ndoa za wengine au matarajio yako

Naamini bado unaweza kuongea nae mkuu maana mti usiokupa matunda unaweza usiukate kwa sababu unakupa kimvuli.. Msemo wa zamani nilipewa 😁

Pole mkuu
 
Kumbadilisha tabia mtu mzima ni jambo gumu sana unless yeye mwenyewe ajitahidi kufifisha tabia zake ili zisikuathiri..

Mungu amtie nguvu tu maana utamrudisha mke kwao kwa ajili ya uvivu na baadae upate huyo mchakarikaji lakini akawa hana adabu na msaliti. Kwa hiyo kama ulivyosema, ni lazma ujue mazuri na madhaifu ya mtu kabla ili ujue kama utaweza kuyabeba au la
 
Tako analo?? kama hana basi umekula hasara mara 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…