Uchaguzi 2020 Sina imani na CHADEMA na Lissu tena, hata wakishindwa itakuwa sawa tu

Ukiwa baba nyumbani watoto na mama wanaweza wasikupende lakini shikamoo watakupa. Tena ikiwa muda wote uko nyumbani wanakuwa na hali ngumu. Baba si una mamlaka? na hayo huwatia woga.
Mtu akikutukana hata akiomba msamaha kilichosemwa hakifutiki. Kikibwa tunavumiliana

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Magufuli amewajengea
madaraja
Madarasa
Mahospitali
Mabweni
Mahosteli
Ma apartment
Ma flyover

Sasa kwanini bado hamumtaki ?
 
[
Endelea kuota tu! Hebu cheki kidogo hapa chini kwa TULIA!

View attachment 1568673
Hiyo si issue hawa watu wa ccm wana mbinu nyingi. Natoa mfano wa mgombea mmoja alituma wapambe mitaani kutoa ahadi za mikopo kwa vikundi vya vikoba. yaani wamama hata wababa mamejikusanya na wengine kujazwa majina ingawa si wanavikoba. Watu wana shida vijana hawana ajira wakiahidiwa wataenda tu. Mikutano itajaa tu kwani wanaamini kuna kitu watapata.
Kujaa kwa mikutano si ajabu. Kutoa kura ndio tabu

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Je

Je chama Kama chama hakiwezi kuomba msaada Kama Kuna viashiria vya uonevu kwenye Uchaguzi?
Ona Sasa Zanzibar jinsi Vyombo vya dola vilivyomwagwa.
Je hapo Hakuna maandalizi ya wizi wa kura na uonevu?

Chama kama chama hakiwezi ndugu... ni mtihani mkubwa lakini siku zinavyosongwa, humu duniani, UN itajitishwa jukumu la kusimamia uchaguzi duniani katika kia nchi mwanachama.. maana threat to international peace and security itapewa new meaning. Dunia haiwezi kukaa kimya ikiwa inaona viashiria vya uvunjivu wa amani juu ya mambo ya uchaguzi... yatakuja tu kama Nyerere na Tanzania yetu tulivyo saidia kitu kinachoitwa duniani humu " doctrine of preemptive strike" wakati wa kumuondoa Iddi Amini Dada.

wao ccm waendelee tu kukaa miaka 59 na kuendelea ipo siku dunia itasema sasa Basi...
 
Hii Point ya Makinikia, ina bidi kuitafakari zaidi kwa makada wanao ona mbali zaidi
 
Ni vizuri Chadema na Lissu wakaja na majibu muafaka ya Jambo Hili tusifanye mzaha kabisa ila naona Kuna follow up kali sana kutoka international organizations .
 
Naomba mnisaidie.
Binadamu tunataka nini hasa???
Tumeshakuwa na Kiongozi mwenye Diplomasia na Demokrasia ya hali ya Juu sana(JK) lakini alitukanwa mpk basi.
Ameingia JPM ambaye ni hard core-Yeye anaongea ukweli Mchungu-Ameenda mbali kiasi cha kutubadilisha fikra zetu especially yale mambo ya kuamini misaada-Hakuna Misaada bali viini macho inayoitwa Misaada-Anaipiga Vita sana na bora afanye hivo.

Lisu ni Mkosoaji si msikilizaji-Yeye ni Mr Right.
Hajapata kufanikiwa mtu anayekosoa tu bila kusikiliza na kushirikisha wengine.
Mimi Namuombea Lisu Uwaziri tena hasa wa Sheria na Katiba.

Ana akili nyingi za kutengeneza sheria-Atumiwe hivo hata kama ni Mpinzani.

Marafiki zangu wa Chadema wana nadharia nyingi sana.Na kwa mpango wanaoongelea maana yake wataenda huko nje kuomba misaada-Hapana huko si kwa kwenda tena,Wazungu siyo kabisa.

JPM akirudi safari hii naamini ataongeza tax base Rafiki na tena kistaarabu na kujenga mazingira wezeshi kwenye sekta binafsi na ikiwezekana kuinua uwezo wa wenye viwanda vikubwa na vya kati kimkakati-Hiyo itamsaidia kutengeneza Middle earners.

Ninaamini ataweka nguvu kubwa kwenye Kilimo na Mifugo-Modenized Farming-Hii itainua haraka sana uchumi wa wananchi wengi na ataongeza ajira vile vile.

Ni JPM tena!
Haina ubishi
 
Ni kweli Lissu ameshashinda kabla ya uchaguzi je Chadema tuna backup ya kuhakikisha kura zinalindwa? Isije kuwa yale yale ya Lowasa alitwambia eti pigeni kura swala la kutangazwa niachieni mimi. Yule mzee mwongo sana atakuja kufa vibaya
 
We ni kada usio ona mbali kwa vizazi vyako vijavyo. Ni bora kusema Ukweli ulio kuwa moyoni mwako, bila kusifu na mapambio angalia hali ya sasa vijana walivyo kata tamaa na kupiga kura, Utatumia mbinu zipi ili waweze kuamini kwa miaka mitano ijayo walisoma kwa Pesa za mikopo na wakakosa ajira na Mitaji, na kukosa mwelekeo leo hii Vijana kama hawa Utawarudisha vipi kwenye kundi la kuamini unacho kisema
 
Ni kweli Lissu ameshashinda kabla ya uchaguzi je Chadema tuna backup ya kuhakikisha kura zinalindwa? Isije kuwa yale yale ya Lowasa alitwambia eti pigeni kura swala la kutangazwa niachieni mimi. Yule mzee mwobgo sana atakuja kufa vibaya
Wewe sinui ndi Gekulu una madeni hadi unadai ulipiwe na Bashiru
 

Sina hakika na usemayo, lakini nina hakika kuwa siku moja nitakufa. Na sasa nina hakika kuwa Kilimanjaro imeenda CCM watu wa mkoa wa kilimanjaro tuna hakika hiyo.

Mwende mkatafute kura za Lissu na upinzani huko Geita, Shinyanga na Mwanza. Tubadilishane ukaaji bungeni upinzani umekwisha tuchosha.

Kila kukicha hali inakuwa wazi zaidi, tunaelekea Kibra naona tanakwenda Kusilim.
 
Saccos ina wenyewe. Kuweka imani kwenye ka kikundi hako ni kutojitambua potential yako kama mtanzania. Mlie, mnune huo ndio ukweli.
 
Sawa kwa hizo points ulizo toa kwenye reli na Nishati na madini, Je kwa hawa watu ambao hawajapitiwa na hiyo reli ya mwendo kasi itawasaidia vipi katika kujikwamua kwa Uchumi, Ikiwa nchi yetu imeingia kwenye Uchumi wa kati ila kiharisi wananchi hawaishi kwa Uchumi huo, Na kwenye nishati na Uchukuzi unafanya kazi yake vizuri kiasi chake Je utawaaminisha vipi wananchi kwa hali hiyo ikiwa hata baadhi ya maeneo ya mijini wanakosa nishati ya Umeme una katika bila sababu maalumu na kukosesha pato la nchi katika muda amabao nishati ya Umeme imekuwa kikwazo kwa Wananchi wanao ishi eneo Hilo?
 
Hivi unajua jimboni kwake maji na barabara vimepatikana baada ya kuondoka T.A.L bungeni.
 

Mtaani kwangu na vijiwe navopita ni watu wamechafukwa
 
Mamilioni ya kura yatoke wapi? Lissu akipata kura laki tano akachinje ng'ombe kujipongeza
 
Nenda TRA kaone idadi ya watu waliofunga biashara zao, kisha uje tuendelee na mjadala.


Kuna uwezekano mkubwa magufuli akawa anapambania uchumi wa nchi nyingi afrika indirectly, of which cdm hawajui lolote linaloendelea dunia hii wao wakishachangisha wanachama basi wamemaliza kila kitu!

- Kwa uchaguzi wa mwaka huu then its 100% on sure that chadema is gone and haitarudi tena ( and there is nothing you can do about it)
- wanachama wengi wa cdm hawajaenda shule kuanzia mwenyekiti na hoja zao zote ni za kupiga kelele wakati wa kampeni huezi skia what they really mean

- Magufuli is the next nyerere after all the initialized projects begin operations officially
- Hakunaga ukombozi wa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja duniani, kila sehem rule inaotumika ni survival for the fittest
- ccm is here to stay mpaka 2100 as to polepole himself! na sio kwamba hatujui wanaiba kura but we support them because bado upinzani ni uchwara nchi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…