Sina kosa ila nimepewa barua kazini! Kuna mtu ananitakia mabaya? Nifanyeje sasa?

Strong and Fearless

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2017
Posts
895
Reaction score
2,218
Kuna baadhi ya wafanyakazi kazini ni kama wanakinga , hawaguswi hata wakikosea vipi. Wanafanya makosa ya wazi, lakini hawaguswi. Lakini wewe ukisema tu kitu kidogo, unaandikiwa barua.

Nilikuwa na mtu mmoja kazini ambaye nilimwamini sana. Nilimchukulia kama dada. Nilimueleza changamoto zangu, hata stress ninazopitia. Siku nyingine nilimwambia, “Leo sijisikii kuja kazini, ngoja nidanganye kuwa naumwa,” nikidhani ni mtu wa kuelewa.

Kumbe hiyo taarifa alienda kuichongea kwa uongozi.
Mwisho wa siku nikaambiwa nimepewa barua ya disciplinary hearing na natakiwa kuhudhuria kikao Jumatatu.

Wakati huo huo, huyo mtu amekuwa na tabia nyingi za hovyo kazini, anapiga simu binafsi muda wa kazi, anaondoka bila ruhusa, lakini hajawahi hata kuitwa kuhojiwa.

Nimeduwaa. Kusema kweli nimevunjika moyo sana. Hivi niende kwenye hicho kikao au niandike barua tu ya kuresign ?

Hii hali ya unafiki na upendeleo kazini inaumiza. Unafanya kazi kwa juhudi lakini watu wa fitna wanakuzidi kete.

Wenzangu, hivi ukiona mazingira ya kazi yako ni sumu kiasi hiki, uamuzi bora ni kuondoka au kupambana hadi mwisho?

Maoni yenu yatanisaidia sana😔😭
 
Kazini kwako hukuenda na mtu yyt kipindi unaiitwa kwaio Fanya kazi lipwa pesa yako nenda nyumbani huko ndio kuna ndg zako. Sijui vijana wa siku waambiwe waelewe kila unaemuona kazin anatafuta ugali wake aidha kwa uwezo wake, uchawi na ndulele au kunafikia wenzake ili aonekane bora. Na kosa sio lake wewe ndio mwenye kosa hapo mdomo wako umekuponza. Solution usije ukathubutu kumuuliza chochote just nenda siku ulioitwa baada ya hapo kaa kimya soma mazingira
 
Nenda kajitetee, maana inaonekana bado haujajipanga kuacha kazi...ukifanikiwa kurejea kazini fanya kilichokupeleka kazini ondoka, huu ushoga na ushkaji mnaoleta makazini unawa cost na mbaya zaidi unaanika privacy zako...nani kakwambia Kuna rafiki wa kumuamini zama hizi?
 
Kuna baadhi ya wafanyakazi kazini ni kama wanakinga , hawaguswi hata wakikosea vipi. Wanafanya makosa ya wazi, lakini hawaguswi. Lakini wewe ukisema tu kitu kidogo, unaandikiwa barua.

Nilikuwa na mtu mmoja kazini ambaye nilimwamini sana. Nilimchukulia kama dada. Nilimueleza changamoto zangu, hata stress ninazopitia. Siku nyingine nilimwambia, “Leo sijisikii kuja kazini, ngoja nidanganye kuwa naumwa,” nikidhani ni mtu wa kuelewa.

Kumbe hiyo taarifa alienda kuichongea kwa uongozi.
Mwisho wa siku nikaambiwa nimepewa barua ya disciplinary hearing na natakiwa kuhudhuria kikao Jumatatu.

Wakati huo huo, huyo mtu amekuwa na tabia nyingi za hovyo kazini, anapiga simu binafsi muda wa kazi, anaondoka bila ruhusa, lakini hajawahi hata kuitwa kuhojiwa.

Nimeduwaa. Kusema kweli nimevunjika moyo sana. Hivi niende kwenye hicho kikao au niandike barua tu ya kuresign ?

Hii hali ya unafiki na upendeleo kazini inaumiza. Unafanya kazi kwa juhudi lakini watu wa fitna wanakuzidi kete.

Wenzangu, hivi ukiona mazingira ya kazi yako ni sumu kiasi hiki, uamuzi bora ni kuondoka au kupambana hadi mwisho?

Maoni yenu yatanisaidia sana😔😭
Kweli wanawake wakiwezeshwa wanaweza.
 
Onyo...Onyo....Onyo...

Usijaribu Ku resign utakuwa umempa adui point tatu na magoli matatu..

Mtu anayekufitini na kukuchongea lengo lake ni wewe ukabiwe kwa juu ili hatimaye ukate tamaa na kuacha kazi...tena usishangae tayari ameshaandaliwa mtu wa ku replace nafasi yako..sasa wewe ukifanya maamuzi ya kukurupuka utakuwa umemsaidia adui kutimiza lengo...

Pia unatakiwa ujifunze na kujizoeza na kujiambia wewe mwenyewe kila siku ya kwamba "SIJAZALIWA KUPAMBANA NA MAMBO MEPESI...PIA SIJAJA DUNIANI KUJA KUCHEKA NA WATU NA KUTAFUTA MARAFIKI,...BALI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO NGUMU ZILIZOWASHINDA WENGINE..

Pambana dada usikae kwa kudeka kazini ukifikiria kuna mtu anakuhurumia...jikaze vumilia ..endelea na kazi...ukisubiria na kufikiria kuna siku mambo yatakuwa rafiki na kila mtu atakuwa rafiki yako labda ni siku ukienda Mbinguni ila duniani ni Vita..

Ukiacha kazi ni ujinga wako mwenyewe..ila hapo hamna cha kukufanya uache kazi..
 
Ajira ni utumwa, kama una akiba ya kutosha anzisha shughuli zako binafsi zitakazokuingizia kipato
msi mjaze mihemuko mapema hii, kuji ajiri sio Kwa ajili ya kila mtu.

biashara Ina hatua kuanzia mwanzo, kukomaa hadi ukuaji, je yeye akale wapi wakati huo?.

Biashara ina hesabu au sayansi yake, na sio tu uki jisikia waweza fanya.
 
Unajiita strong and fearless halafu jambo dogo hivyo linakupa headache?
 
Kuna baadhi ya wafanyakazi kazini ni kama wanakinga , hawaguswi hata wakikosea vipi. Wanafanya makosa ya wazi, lakini hawaguswi. Lakini wewe ukisema tu kitu kidogo, unaandikiwa barua.

Nilikuwa na mtu mmoja kazini ambaye nilimwamini sana. Nilimchukulia kama dada. Nilimueleza changamoto zangu, hata stress ninazopitia. Siku nyingine nilimwambia, “Leo sijisikii kuja kazini, ngoja nidanganye kuwa naumwa,” nikidhani ni mtu wa kuelewa.

Kumbe hiyo taarifa alienda kuichongea kwa uongozi.
Mwisho wa siku nikaambiwa nimepewa barua ya disciplinary hearing na natakiwa kuhudhuria kikao Jumatatu.

Wakati huo huo, huyo mtu amekuwa na tabia nyingi za hovyo kazini, anapiga simu binafsi muda wa kazi, anaondoka bila ruhusa, lakini hajawahi hata kuitwa kuhojiwa.

Nimeduwaa. Kusema kweli nimevunjika moyo sana. Hivi niende kwenye hicho kikao au niandike barua tu ya kuresign ?

Hii hali ya unafiki na upendeleo kazini inaumiza. Unafanya kazi kwa juhudi lakini watu wa fitna wanakuzidi kete.

Wenzangu, hivi ukiona mazingira ya kazi yako ni sumu kiasi hiki, uamuzi bora ni kuondoka au kupambana hadi mwisho?

Maoni yenu yatanisaidia sana😔😭
Wewe unaacha kazi umeshapata nyingine?
Wewe nenda usikie wanasemaje?
Km Kuna chance ya kuomba msamaha omba,then ishi na wenzako kwa umakini,ukiendelea kujipanga ujiajiri mwenyewe
 
Wafanyakazi wenzio sio rafiki zako.

Muambiwe mara ngapi?
 
1. Dogo nenda kwenye hicho kikao usiache kazi mtaani ni pagumu sana.
2. Huyo manzi unaemwita dada fanya juu chini umtombe upunguze machungu tena mnywee vant mixer mkongo.
3. Punguza shobo, mazoea na kujieleza sana kazini share stories za kazi na mpira tu.
 
Back
Top Bottom