Sina kosa ila nimepewa barua kazini! Kuna mtu ananitakia mabaya? Nifanyeje sasa?

Kuna baadhi ya wafanyakazi kazini ni kama wanakinga , hawaguswi hata wakikosea vipi. Wanafanya makosa ya wazi, lakini hawaguswi. Lakini wewe ukisema tu kitu kidogo, unaandikiwa barua.

Nilikuwa na mtu mmoja kazini ambaye nilimwamini sana. Nilimchukulia kama dada. Nilimueleza changamoto zangu, hata stress ninazopitia. Siku nyingine nilimwambia, “Leo sijisikii kuja kazini, ngoja nidanganye kuwa naumwa,” nikidhani ni mtu wa kuelewa.

Kumbe hiyo taarifa alienda kuichongea kwa uongozi.
Mwisho wa siku nikaambiwa nimepewa barua ya disciplinary hearing na natakiwa kuhudhuria kikao Jumatatu.

Wakati huo huo, huyo mtu amekuwa na tabia nyingi za hovyo kazini, anapiga simu binafsi muda wa kazi, anaondoka bila ruhusa, lakini hajawahi hata kuitwa kuhojiwa.

Nimeduwaa. Kusema kweli nimevunjika moyo sana. Hivi niende kwenye hicho kikao au niandike barua tu ya kuresign ?

Hii hali ya unafiki na upendeleo kazini inaumiza. Unafanya kazi kwa juhudi lakini watu wa fitna wanakuzidi kete.

Wenzangu, hivi ukiona mazingira ya kazi yako ni sumu kiasi hiki, uamuzi bora ni kuondoka au kupambana hadi mwisho?

Maoni yenu yatanisaidia sana😔😭
Una utoto mwingi kichwani mwako.. 🙂 🙂
 
Ndugu usiende mtaani bila kazi kule ni hatari kuliko kukaa kwenye kazi yenye changamoto.

Kwa hili Naona shida unajitafutia mwenyewe.

Umeenda kazini hujafuta urafiki pale,kazini ni uwanja wa Vita pambana
Ukiacha Kazi nitakuona hamnazo, unashindwa kumdharau huyo mtu? Unataka kumpa umuhimu kiasi kwamba unataka kuacha Kazi?
 
Ukiwa kiazi kila pahala utaona unaonewa.

Kuna watu makazini ni wanafki sana, wewe ukijifanya kuwaamini na kuwaambia ukweli wako, jinsi unavyopiga madili, jinsi ulivyo mvivu, huipendi kazi, unafanya ili mradi liende, wenzio wanakuchora tu, huku wao wakikwambia wanafanya mabaya zaidi yako. Yaani wewe sio mvivu wao ni wavivu pro, ni wapiga dili hatari, na bosi hawamuheshimu hata kidogo.

Sasa wewe ukiwa kiazi ukawaamini ukidhani ndio ujanja, kumbe wenzio wananogesha story ili waonekane wakaidi (kibongobongo hii ni sifa nzuri sana), ukijiingiza mkenge inakula kwako dadeki 😀😀.

Kama ni watu wa kuhudumia wateja, basi watakwambia jinsi wanavyowajibu shit wateja, jinsi walivyo wakali kwa wateja hata bosi akiwa mbele yao, aloo kumbe ni uongo, ni wanyenyekevu vibaya mno 😂😂.
 
Hii
Kuna baadhi ya wafanyakazi kazini ni kama wanakinga , hawaguswi hata wakikosea vipi. Wanafanya makosa ya wazi, lakini hawaguswi. Lakini wewe ukisema tu kitu kidogo, unaandikiwa barua.

Nilikuwa na mtu mmoja kazini ambaye nilimwamini sana. Nilimchukulia kama dada. Nilimueleza changamoto zangu, hata stress ninazopitia. Siku nyingine nilimwambia, “Leo sijisikii kuja kazini, ngoja nidanganye kuwa naumwa,” nikidhani ni mtu wa kuelewa.

Kumbe hiyo taarifa alienda kuichongea kwa uongozi.
Mwisho wa siku nikaambiwa nimepewa barua ya disciplinary hearing na natakiwa kuhudhuria kikao Jumatatu.

Wakati huo huo, huyo mtu amekuwa na tabia nyingi za hovyo kazini, anapiga simu binafsi muda wa kazi, anaondoka bila ruhusa, lakini hajawahi hata kuitwa kuhojiwa.

Nimeduwaa. Kusema kweli nimevunjika moyo sana. Hivi niende kwenye hicho kikao au niandike barua tu ya kuresign ?

Hii hali ya unafiki na upendeleo kazini inaumiza. Unafanya kazi kwa juhudi lakini watu wa fitna wanakuzidi kete.

Wenzangu, hivi ukiona mazingira ya kazi yako ni sumu kiasi hiki, uamuzi bora ni kuondoka au kupambana hadi mwisho?

Maoni yenu yatanisaidia sana😔😭
Hii ilishanikuta nilimwamini staff mwenzangu kila kosa ninalofanya mimi akawa anampelekea boss mazingira ya kazini yalikuwa magumu sana hatimae wote tumesimamishwa kazi!
 
Kuna baadhi ya wafanyakazi kazini ni kama wanakinga , hawaguswi hata wakikosea vipi. Wanafanya makosa ya wazi, lakini hawaguswi. Lakini wewe ukisema tu kitu kidogo, unaandikiwa barua.

Nilikuwa na mtu mmoja kazini ambaye nilimwamini sana. Nilimchukulia kama dada. Nilimueleza changamoto zangu, hata stress ninazopitia. Siku nyingine nilimwambia, “Leo sijisikii kuja kazini, ngoja nidanganye kuwa naumwa,” nikidhani ni mtu wa kuelewa.

Kumbe hiyo taarifa alienda kuichongea kwa uongozi.
Mwisho wa siku nikaambiwa nimepewa barua ya disciplinary hearing na natakiwa kuhudhuria kikao Jumatatu.

Wakati huo huo, huyo mtu amekuwa na tabia nyingi za hovyo kazini, anapiga simu binafsi muda wa kazi, anaondoka bila ruhusa, lakini hajawahi hata kuitwa kuhojiwa.

Nimeduwaa. Kusema kweli nimevunjika moyo sana. Hivi niende kwenye hicho kikao au niandike barua tu ya kuresign ?

Hii hali ya unafiki na upendeleo kazini inaumiza. Unafanya kazi kwa juhudi lakini watu wa fitna wanakuzidi kete.

Wenzangu, hivi ukiona mazingira ya kazi yako ni sumu kiasi hiki, uamuzi bora ni kuondoka au kupambana hadi mwisho?

Maoni yenu yatanisaidia sana😔😭
Kuwa na discipline ya maisha.
Kwanza kazi si mama yako, fanya kazi yako kama inavyokukabili bila kumtazama mtu mwingine.
Pili, kuwa na malengo.
Unafanya kazi ili iweje?
Kazi inakuingizia kipato cha kukutosha?
Kama ndiyo fanya kazi kwa bidii, na kama sivyo aidha tafuta kazi kwingine au dunduliza mtaji ujiajiri.
 
Kuna baadhi ya wafanyakazi kazini ni kama wanakinga , hawaguswi hata wakikosea vipi. Wanafanya makosa ya wazi, lakini hawaguswi. Lakini wewe ukisema tu kitu kidogo, unaandikiwa barua.

Nilikuwa na mtu mmoja kazini ambaye nilimwamini sana. Nilimchukulia kama dada. Nilimueleza changamoto zangu, hata stress ninazopitia. Siku nyingine nilimwambia, “Leo sijisikii kuja kazini, ngoja nidanganye kuwa naumwa,” nikidhani ni mtu wa kuelewa.

Kumbe hiyo taarifa alienda kuichongea kwa uongozi.
Mwisho wa siku nikaambiwa nimepewa barua ya disciplinary hearing na natakiwa kuhudhuria kikao Jumatatu.

Wakati huo huo, huyo mtu amekuwa na tabia nyingi za hovyo kazini, anapiga simu binafsi muda wa kazi, anaondoka bila ruhusa, lakini hajawahi hata kuitwa kuhojiwa.

Nimeduwaa. Kusema kweli nimevunjika moyo sana. Hivi niende kwenye hicho kikao au niandike barua tu ya kuresign ?

Hii hali ya unafiki na upendeleo kazini inaumiza. Unafanya kazi kwa juhudi lakini watu wa fitna wanakuzidi kete.

Wenzangu, hivi ukiona mazingira ya kazi yako ni sumu kiasi hiki, uamuzi bora ni kuondoka au kupambana hadi mwisho?

Maoni yenu yatanisaidia sana😔😭
Chawa ana nguvu hasa kwa bosi mjinga
 
Una jina kubwa lakini hauna hata mada moja inayoendana nalo,ni heri ujiite "SIKUJUA".
 
Maoni yenu yatanisaidia sana😔😭
kama umeitwa kwenye hearing hopefully mna chama cha wafanyakazi,
hakikisha una docs zinazoonyesha ulikuwa unaumwa. kama vile ED kutoka kwa daktari.
Ikitokea akawa shahidi kwamba uliongea naye ili wakufukuze kazi,mkatalie kwamba ametunga uongo
kwa kufanya hivyo utapona.
 
Mdomo wako ndo umekuponza mwenyewe

Watu hamna koromeo kila kitu mnasema tuu

Usiache kazi ndugu endelea kupambana ila utakua ushajua namna ya kuishi na watu kazini

Kazini kwako kuna kazi
 
Hakuna rafiki kazin...fanya kilichokupeleka...set standard na uweke mipaka
 
Unajiita strong and fearless alafu unakua mzembe hivyo apo wewe pambana tu na kazi akuna kuweka stor za maisha yako fika ofisin salam kazi nyumban iyo ndy life style ya kaz me niko hivyo na kama awanishirikishi mambo yao napotezea
 
Back
Top Bottom