Sina raha, wasiwasi wa maisha unanisumbua

Gol D Roger

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2023
Posts
2,316
Reaction score
6,082
Nasumbuliwa sana na wasiwasi wa maisha, mwanzoni nilikuwa naona kawaida ila kwa hali yangu ya sasa naona it's too much.

Ngoja niwaelezee kidogo jinsi ilivyo, mfano nikitoka kazini nikirudi home kupumzika, mawazo yananijia kuna vijana wenzangu bado hawajarudi ghetto bado wapo mtaani wanapambana, bac nakosa raha kabisa, naanza kuona kama napoteza muda kupumzika.

Hata nikijifunza new skills ambazo naona kabisa hizi zitani-boost kiasi flani kazini bado kuna kitu nafsini mwangu kinaniambia wewe bado sana.

Kila nalofanya naona kama si kitu, siipendi hii hali, nataka initoke.

Juzi kati mm na mshkaji wangu tumetoka kupiga project flani ivi tumepiga hela nzuri tuu ila nilivoipata tuu ile hela mawazo yakanijia kuna vijana wenzako wanapata hii within a day, mimi imenichukua takribani mwezi mzima, bac furaha yote ikaisha. Hapo ndo nikaanza kujitathmini na kuona kwamba hii hali sasa inaninyima raha na inabidi nitafute ushauri au counselling.

Hata nikiwaza niende kuongeza elimu kuna mawazo yananijia kuna watu wameishia darasa la saba na wana biashara zimesimama hapa mjini unataka uongeze elimu ili iweje, bac najikuta naghairi na kuona kama naenda kupoteza hela na muda.

Yaan ni kama vile nashindana na watu alaf hao watu wenyew siwaoni, nawabuni tu kichwani mwangu.

Inaboa sana hii hali, kuna muda natamani nisikie furaha, hata kama ni hatua ndogo kiasi gani nimepiga ila wapi.

Hivi ni mimi tuu ninayesumbuliwa na hii hali?

Hebu tushauriane, mlioweza kuondokana na hii hali mliwezaje?
 
Nenda taratibu kijana, usijifananishe, tumia hicho hicho ulichoko nacho kuongeza kipato usihofu kila mtu na wakati wake. Kila zama na majira yake. Shukuru Mungu kwa hicho unachokipata unavyitamani vya watu kuna watu wanatamani ulichonacho.
kwan unafanya kazi gan mkuu
 
ushapona Mkuu, hilo ni tatizo lakini pia si tatizo kwakuwa ushalijua, sijui tulipe jina gani lakini sio ishu, hapo kitu muhimu ni afya Mkuu, alafu acha kujilinganisha na wengine, bali jiwekee malengo ya wewe wa baadae, kimbizana na vile unataka wewe uwe, na kwa uandishi wako inaonekana bado huna familia, Muda bado uo upande wako, una kitu Mzee Future hako haitaki uwe mzembe, usirudi gheto kupumzika wakati bado kuna kitu umekiacha mtaani na ni cha kwako ndio maana nafsi inasema na wewe
 
Nrnda taratibu kijana, usijifananishe, tumia hicho hicho ulichoko nacho kuemongeza kipato usihofu kila mtu na wakati wake. Kila zama na majira yake. Shukuru Mungu kwa hicho unachokipata unavyitamani vya watu kuna watu wanatamani ulichonacho.
kwan unafanya kazi gan mkuu
Ahsante sana mkuu.
 
ushapona Mkuu, hilo ni tatizo lakini pia si tatizo kwakuwa ushalijua, sijui tulipe jina gani lakini sio ishu, hapo kitu muhimu ni afya Mkuu, alafu acha kujilinganisha na wengine, bali jiwekee malengo ya wewe wa baadae, kimbizana na vile unataka wewe uwe, na kwa uandishi wako inaonekana bado huna familia, Muda bado uo upande wako, una kitu Mzee Future hako haitaki uwe mzembe, usirudi gheto kupumzika wakati bado kuna kitu umekiacha mtaani na ni cha kwako ndio maana nafsi inasema na wewe
Thank you for these kind words brother
 
Duniani kila mtu ana wasiwasi na lake hakuna aliyemaliza hata unaotegemea tukushauri kuna namna fulani fulani na sisi tumetingwa ila vibaya tu usiutamani wasiwasi wa mwenzako situation unayoipitia mleta mada.

Mfano mkuu wewe umeshapewa hesabu yako ya siku unaenda tena kuwawazia ambao hawajalala wa kazi gani?mimi nitakushauri kila unachokipata jitahidi ukiwekeze mahali either kiwe kinazalisha au ni asset ambayo hata kesho ukiwa haupo ktk nafasi uliyo nayo leo ujifariji nacho in short wewe unayaogopa maisha na ili upate utulivu lazima umiliki kitu.
 
Nenda taratibu ndugu hao unao waona kuna ambao vipato vyao vinatokana na masharti ambayo kipato Chako unapata kwa haki cha msingi Kila mwaka weka lengo ufikie hatua gani , fungua akaunti mbili , Moja weka "standing order" hela flani ikiingia kwenye akaunti nyingine ni ya kutimiza malengo yako kiasi kingine fanyia matumizi yako ya Kila siku. Dunia hii ina mambo mengi kwenye mafanikio taratibu ndio mwendo Tafadhali pata na muda wa kusoma kitabu hichi
 
Attachments

Kwanza ngoja nikuchambue....
Wewe ni aina ya vijana ambao ni wakimya na hawapendi kujichanganya.
Haunywi pombe na nina uhakika hauvuti sigara.
Hauna marafiki na unapenda kujishauri mwwnyewe kwa mambo yanayo kusumbua.
Una mahusiano lakini nikama yanakuboa, na mpenzi wako yupo nawewe lakini hafurahii mahusiani yenu.
Umekulia kwenye imani ya dini, lakini nikama umeanza kuvunjika na umekua na ham ya kwenda kwa waganga wa kienyeji.
Narudi kuendelea....
 
Nimekuelewa mzee, ushauri mzuri
 
Nishakidownload kaka ntajaribu kukipitia
 
Kwanza ngoja nikuchambue....
Wewe ni aina ya vijana ambao ni wakimya na hawapendi kujichanganya.
Haunywi pombe na nina uhakika hauvuti sigara.
Hauna marafiki na unapenda kujishauri mwwnyewe kwa mambo yanayo kusumbua.
Una mahusiano lakini nikama yanakuboa, na mpenzi wako yupo nawewe lakini hafurahii mahusiani yenu.
Umekulia kwenye imani ya dini, lakini nikama umeanza kuvunjika na umekua na ham ya kwenda kwa waganga wa kienyeji.
Narudi kuendelea....

Duh! Kumbe tuko wengi
 
Kote umepatia, ila hapo kwa waganga wa kienyeji hapana kwa kweli, mimi na Yesu na Yesu na mimi.

Umejuaje hayo mambo mengine??
 
Mkuu kwanza hongera kwa namna ulivyo lidescribe tatizo lako vizuri mno
Nachokiona Mimi ni kwamba unajifahamu kabisa u have so much potential in you ila hauitumii ipasavyo, Kuna mdau kashauri unahitaji kumiliki kitu Ili upate usawaziko wa akili that's a good move, but that's the end of the process. What u need is the happiness that comes with the process for now..
Nachoweza kurecommend Kwa Sasa ni
  • Weka malengo ya kiuchumi ambayo yanasisimua akili Yako katika mfumo pendwa wa " SMART"
  • Anza kuweka action plans A mpaka Z kufikia malengo Yako uliojiwekea
  • Anza ku execute daily plans zako na uzidi kuziboresha kutokana na experience unayoipata field
  • Jifunze Kwa wengine wenye mafanikio unayoyataka ikiwezekana omba ushauri kwa wao hao
  • Never look back

Watu Kama nyie mpo Duniani Kwa kusudi maalum.. huwezi pata amani bila kutimiza Ilo kusudi

Ngoja ni screenshot huu ushauri na mm nikaufanyie KAZI
 
Achana na nimejuaje, nitakuelezea siku nyingine.
Sasa fanya hivi:-
1. Tafuta rafiki ama ndugu ama mpenzi ambae utamuamini kati ya hao, then tengeneza urafiki mpya na hakikisha unamjua huyo mtu wako wa karibu mpya "ikiwezekena jipe muda".
2. Anza kujitoa kwa mtu huyo utakae mchagua, hakikisha kila tatizo lako unaongea nae na anashiriki kikamilifu hasa kwenye mambo yako ya maendeleo.
3. Kwakua mtu wa karibu atakua ni mpya, basi jitahidi usifunguke kwake sana hadi pale utakapo mfaham vyema na ujiridhishe kwamba pia anaweza akawepo na kusimama na we wakati wote utakapokua kwenye shida na raha.
4. Tafuta mwanamke uoe, lakini hakikisha unajipa wakati mwingi ili umjue vizuri "maana watu wa aina yako hua wanakua na shida sana na wanafeli kupata mke anaefaa".
5. Kama mzazi wako yupo, basi jitahidi sana kuwa karibu na mzazi wako na mshirikishe katika kila jambo na atakushauri vyema (ingawa nahisi pengine hauna mahusiano mazuri na mzazi wako "hapa nakushauri samehe hata kama alikukosea na futa kilakitu uanze maisha mapya).
Nitakuja kuendelea......
 
Mkuu kwanza hongera kwa namna ulivyo lidescribe tatizo lako vizuri mno
Nachokiona Mimi ni kwamba unajifahamu kabisa u have so much potential in you ila hauitumii ipasavyo, Kuna mdau kashauri unahitaji kumiliki kitu Ili upate usawaziko wa akili that's a good move, but that's the end of the process. What u need is the happiness that comes with the process for now..
Nachoweza kurecommend Kwa Sasa ni
  • Weka malengo ya kiuchumi ambayo yanasisimua akili Yako katika mfumo pendwa wa " SMART"
  • Anza kuweka action plans A mpaka Z kufikia malengo Yako uliojiwekea
  • Anza ku execute daily plans zako na uzidi kuziboresha kutokana na experience unayoipata field
  • Jifunze Kwa wengine wenye mafanikio unayoyataka ikiwezekana omba ushauri kwa wao hao
  • Never look back

Watu Kama nyie mpo Duniani Kwa kusudi maalum.. huwezi pata amani bila kutimiza Ilo kusudi

Ngoja ni screenshot huu ushauri na mm nikaufanyie KAZI
Brother sijui niseme nn, ahsante sana hayo mengine ntajiongea
 
Back
Top Bottom