Amani na mafanikio ni vitu viwili tofauti, ndio nilichojifunza, siku ukiamua kutafuta amani hutobughuziwa na changamoto za mafanikio, maana hakuna waliofanikiwa wakafanikiwa, maana hata walipodhani wamefanikiwa walianza kulinda mafanikio Yao na hawajafanikiwa Hadi Leo kuwa na uwakika kwamba wameweza kulinda mafanikio Yao, hawalali mapema, wakilala hawalali usingizi ,ila wanajilaza tuu, hata kifungo kikidondoka wanajua wamevamiwa
Umasikini siyo mzuri,ila wale wenye mahitaji ya wastani, yaani chakula, mafadhi na makadhi Tena ya kawaida na nauli ya kuendea kwenye mihangaiko ,Wana amani sanasana,japo hawana mafanikio kama matajiri ,wanalala na kuamshwa kwa alarm, akilala hata umwite hashituki maana Hana Cha thamani zaidi ya nafsi yake mwenyewe,
Sisemi tuwe wavivu, hapana ,ila tuache kupaniki, tutafuteni amani kwanza ,mafanikio yanaweza maliza amani yetu, hivo ni vyema tukayaendea kwa hekima,. Under 30's angalia vitu unavovipenda kwanza, ie epuka projects ambazo zitakutesa, mf kipato chako kwa mwezi ni laki Tano, unaanzisha ujenzi wa nyumba ya kukaa yenye thamani ya mil 40, jilani Yako nae ana project kama Yako ila kipato Chake kwa mwezi ni mil 2, wote mnalingana umri, ukiona anaenda mbio kwa Nini usipaniki ! Usipange mipango kwa fashion,angalia Hali Yako, classmates wanapost magari kwenye group lenu la shule, na wewe unataka uwe kama wao, uta-R.I.P