Single fathers and mothers njooni tujenge familia

Single fathers and mothers njooni tujenge familia

Tushatulia na kiranga kimetuisha
Ni vizuri kama mmetulia sio kila mwaka mtt anaona baba mpya.


Mimi nimelala na mwanangu hapa kaniwekea mguu kama enzi za utoto haamini kama nipo likizo siondoki leo
 
Ila mimi sipendi hii sentensi, "Afadhali kuwa single mother kuliko hao mlionao huko mtaani wanaotoa mimba au walioolewa na ni wagumba!"

Sitaki kumtetea mtu lakini ifike mahali tukiri kuwa wengi wa hawa wazazi (wa kike na wa kiume) walikosea katika maisha yao. Sawa walifanya maamuzi ya kutozitoa mimba lakini isiwe sababu ya kumuona aliyetoa kuwa ana makosa. Nyote mlikosea kuzini kabla ya ndoa (wengi wanaotumia hiyo sentensi ni wale waliozaa nje ya ndoa).

Mimi ni Mkristo ninayeamini katika neema ya Mungu. Sote tumetenda makosa huko nyuma lakini siwezi kuja mentor mimi nikasema afadhali mimi huwa najeruhi, kuna wengine huwa wanaua. Haifanyi dhambi yangu kuwa afadhali. Besides, kuna waliozaa kwa kuwa tu dawa za kuzuia mimba ziligoma na hata alipojaribu kuitoa mimba ikagoma.

Ushauri wangu kwenu wadada (single mothers) - na hapa naongea na hawa waliozaa nje ya ndoa: Kuwa a single parent ni jukumu kubwa na linatosha kuonesha how strong you are...jamii nzima inajua hilo. Tuache kuwaponda wenngine ili kuonesha unafuu wenu.
Natamani mngeongelea jinsi ambavyo mnakiri mlikosea, mmejirekebisha na mmetulia kulea watoto wenu. Jamii kamwe haitaacha kuwasema hata mwisho wa dunia (mnakumbuka enzi za Yesu? aliletwa mwanamke aliyezini...mwanaume aliyezini naye hakuwepo).

So acheni kupigana hii vita ya kijamii. Jamii itaendelea siku zote kuwasema vibaya. Ila katika yote, "Ni kweli nilikosea huko nyuma, nilipogundua nimepata mimba nikaamua kuilea na kumlea mwanangu hadi hivi alivyo. lakini, baada ya kutenda kosa hilo nilibadilika, nilikuwa mwerevu zaidi, nilitubu na neema ya Mungu imenifanya kuwa kiumbe kipya. Na sasa nipo hivi nilivyo na mwanangu. Haijanifanya kuwa bora kuliko wengine. Ila imenifanya kuwa wa thamani kwa Mungu wangu. Nimeweza kusamehe na ku-move on."


La muhimu zaidi: nyie muwe chachu kwa mabinti wadogo kuwaelimisha jinsi gani isivyopendeza kujiingiza kwenye hayo mahusiano yasiyo na mbele wala nyuma. Jinsi gani isivyo na faida kufanya ngono zembe. Maana ukweli ni kwamba jamii itaendelea kuwasema leo 2017, 2018, 2020 hata 2055..." Wajiepushe na ngono na kwa kuwa kizazi hiki ndo vile tena basi wajiepushe na ngono zembe"

Huwa ninasema, ni kweli it takes two to tango lakini ilikishatokea la kutokea nyie dada zangu ndo mnaobaki na mzigo mkubwa. Ni wakati sasa kusimama na kuwa na maamuzi inapofika kwenye masuala ya ngono. Tumia kinga, ujue mzunguko wako sawasawa, yaani BE IN CONTROL of your sex life.

naumia sana jamii inavyowasema vibaya lakini kwa kuwa hatuwezi kubadili mtazamo wa jamii (ambao sio wa makosa pia) ni rahisi kuwaelimisha wadogo zenu wengine wasijedumbukia kwenye mzigo mliopo nyie.

Nimekutana na single mothers wengi na wanapenda sana ku-potray kuwa they are strong and prod etc etc (ni sawa) lakini hawawi wazi kuelezea changamoto na ku-discourage wengine wasiingie huko.

Mentor namalizia kwa kusema: Wadogo zangu na dada zangu wa kike ambao bado hamjajifungua...kwa mtini mjifunze. Angalieni jamii inavyowasema vibaya hawa dada zenu na muamue leo kuwa in control of your bodies! Usiruhusu mapenzi yakufunike macho. Utaachwa ukilia usiku kila siku.

Dah mentor naumia ila ndo nifanyaje sasa...
Pole sana mentor

You are really mentor!
 
Mpaka leo mwanangu sijawahi kumtambulisha baba mpya. Anaona marafiki zangu tu wa kiume ila sio boyfriend.
Ebu chukulia na wewe usingepata fursa ya kumjua baba yako kama unavyomficha mwanao ungejisikiaje?
 
Back
Top Bottom