Mleta mada anataka tushirikishane changamoto ila naona wengi mmeenda nje ya mada. Am single dad with two kids mkubwa ni wakike mdogo ni wakiume, changamoto kubwa naipata kwa huyu wa kike hapendi kula kabsa tangu akiwa mdogo now ana 5 yrs, kuna wakati ili ale inabdi nimuimbie wimbo anaoupenda ndio atakula na hapo mpatane idadi ya vjiko atakavyokula na inabdi nitumie ujanja wa kuchota kijiko kilichojaa vzuri ili angalau ashibe. Then ni mtoto wa baba kwelikweli nikiwa safari au nikichelewa kurudi toka kazini anaweza kugoma kabsa kula mpaka nirudi so nikiwa safari inabdi nipge sim kabla ya saa za kula niongee nae na kumuhaidi kumletea zawadi nzuriii kwa maelewano kuwa asipokula simletei zawadi.
Huyu mdogo issue ya kula hasumbui kabsa kila msosi anagonga ila shida yake ni ubabe 2 yrs now ila ni bondia wa hatari,hapendi mtu ashike kitu changu chochote,huyo hana muda na mimi ila nikikaa wiki moja bilakua home basi akiona mwanaume yoyote yeye anaita baba! !!
For sure am happy with my kids, wao kwangu ni kilakitu
Sent using
Jamii Forums mobile app