Single mother utalindaje ndoa yako kama hili likitokea kwenye mahusiano yako mapya?

S
Habari wana JF.

Nina ndugu yangu mmoja upande wa mama, yeye KE.

Miaka kama 10 hivi iliyopita alikuwa ba mahusiano na Jamaa mmoja hivi, walikaa mda tuu mpaka mahusiano yao yakazaa mtoto. Lkn baada ya kujifungua Jamaa alimkwepa sister.

Si unajua wanaume wa kukimbia watoto wapo. Jamaa akawa hata huduma hatoi wala nini, ila mtoto anamtaka kumuoa kuna wakati alikuwa anajitokeza hata baada ya 3 month mara 1 tuu kumuona mtoto hatoi chochote. Baadae katokomea kabisa.

Sasa sister angu huyu akakutana na jamaa mwingine kipindi mtoto wake alikuwa na umri wa miaka 3 kwenda min.

Jamaa hakuwa tayari kuwanae siunajua single mother wanaume hatupendi sana, ila sister alijaribu kumshawishi mpk kukubali. Na alimueleza kila kitu kuhusu Baba mtoto.

Jamaa akasema kwa vile Baba mtoto kasepa kapotea basi tutakuwa fresh, ila alitoa sharti hataki kuona Baba mtoto anajitokeza au mama anajipendekeza.

Wakafanikiwa kufunga ndoa.
Na kuchukua mtoto wakawa wanakaa nae ndogo alipofikisha miaka 6 akampeleka shule mzuri ya 2million per year akawa anasoma huko.

Sasa Baba mtoto aliposikia bibie kaolewa si akarudi bwana kuanza kutaka mtoto. Sister akagoma kabisa tena bila kumwambia mume wake . Na arirudi kipindi sister anawatoto wadogo mapacha aliyezaa ba mume wake.

Waliangaishana kama mwaka 1 hivi. Sister alikataa kabisa kumpa dogo.

Sasa kipindi mtoto kafikisha miaka 8. Jamaa si akaenda ustawi wa jamii kwa lengo la kuchukua mtoto, sister kweli aliitwa ustawi wa jamaii na alienda tena bila kumwambia mume wake. Yeye alieleza kwao na kwao waligoma na kumwambia asiende. Ila ustawi wa jamii walilazimisha na kumwambia Mtoto anahaki ya kumjua Baba yake halisi. Hio ni haki ya mtoto.

Sasa mume wake baada ya kujua hilo akachachamaa kabisa ukawa ni ugomvi sana kati ya yeye na mke wake.
Mume wake akaamini kuwa Sister alimficha au niseme alimdanganya jamaa kakimbia kumbe laa. Waligombana sana.

Sasa jamaa akafanikiwa mpk kubadilisha jina mtoto la mwisho maana sister aliandika jina la kwao la mwisho la mtoto.
Jamaa akaweka jina la kwao. Na jina lake kwenye cheti cha kuzaliwa. Maana sehemu ya Baba ilikuwa empty nafikili.

Mume wake baada ya kuona hivyo akamwambia kuwa kuhusu kitu chochote cha mtoto wake asimwambie mpk ada. Na mtoto aende kwa Baba yake pale home kwake amtaki tena.

Sister akaona kwa vile anataka kuokoa ndoa yake ampeleke mtoto kwa Baba yake. Sasa ishu kule kwa jamaa , dogo alikuwa anasoma shule ya over 2 million per year. Jamaa wa kawaida tuu.

Kwa kifupi dogo baada ya kwenda kwa Baba mawasiliano yakazidi kupelekea mpk mume wake kuanza kugombana. Sister akasema yule mwenzie anamsumbua sana na anamfanya mtoto kama kung'ang'ania kumuona mama yake, mda wote.
So anajikuta mda mwingi anakuwa anawasiliana upande mwingine.

Baada ya kuona drama ni nyingi mume alimtimua sister home kwake. Na walisumbuana kama 2 years kutaka kuachana.
Mume wake ni mtu mwenye wivu. Walitaka kusuruhisha kwa kumuita jamaa yule msumbufu ila jamaa aligoma kuja na wala mume wake alikataa kusikiliza suruhisho.
Wiki mbili zilizopita waliachana baada ya purukushani kwa miaka 2.

Alikuwa single mother na kuingia kwenye ndoa na mwishowe kaeudi tena single mother.
Dogo anasoma shule za kawaida tuu hizi japo ni private pia kule kashatoa shule ya bei kubwa.

Hivi ishu kama hii mnaisolve kivipi jamani, IKIJA KWENYE FAMILIA , KARIBUNI.
Sjasoma kbsa lkn kun mamb hayapo sawa 1.jamaa alimpata vip ten huyo dada 2 alijuaje shule anayosoma mtoto 3. Alifanikiwa vip kubadil jina la mtoto
 
Mkuu ukizaa na mwanmake ukamuachia mtoto na unakaa mji mmoja hapa hapa anaolewa hapo hapo mji mmoja .
Utashidwa kujua kweli??

Mtoto kutumia jina la Baba yek ni haki ya mtoto.
 
SIngle mama ukitaka kuolewa uchague kukabidhi mtoto kwa baba yake, ama kukata mawasiliano kabisa na baba mtoto na ndugu zake, kiufupi asijue ulipo.

Ila mimi pangechimbika aisee...mtoto asingempata, hata kama huyo mume angeniacha lkn ningebaki na mtoto wangu katika hali yoyote ile.
 
Mkuu ukizaa na mwanmake ukamuachia mtoto na unakaa mji mmoja hapa hapa anaolewa hapo hapo mji mmoja .
Utashidwa kujua kweli??

Mtoto kutumia jina la Baba yek ni haki ya mtoto.
"Jamaaa altokomea au alkimbia" hicho ndcho cha kusmamia na KUKAZIA whatever baba mzaz au baba mzushi mamb hubadlishwa kwa heshima huyo dada angemuita surname ya mlezi wake over. Kujua baba halis wa nn na alkimbia? Unajua maana ya baba halisi? Baba halisi hawez kimbia
 
I’m a single mama…kitu alichokwama mwenzetu ni kuruhusu mawasiliano ya yeye na mzazi mwenzie moja kwa moja.

kuna wakati hata sisi single moms tunazingua big time[emoji18][emoji18].kulingana na huu uzi..single mom ndie aliyeanza kumkaribisha shetani.unatolea wapi ujasiri wa kwenda ustawi wa jamii bila kwenda na mumeo?huo ni upumbavu mzito na hakuna mwanaume yeyote mwenye kupenda Amani ya moyo angevumilia[emoji174][emoji174]

Hivi unakuwaje na mume kabisa ambae amekukubali wewe na mtoto wako wote kuwalea halafu eti from nowhere ***** unakuja kuwasiliana na mzazi mwenzio just namna hiyo[emoji15]
Aliolewa kwa sababu ya shida. Alizaa kwa sababu ya upendo. Kati ya shida na upendo kipi kinaweza kufuatwa na mwanamke?
 
Hii kesi ni ngumu kama vita ya izrael na gaza ndio maana mama yangu huniambia usioe mwanamke ambae tayari amekwisha zaa na mwingine kabla yako nahisi anaupeo mzuri wa haya mambo mwanamke aliyezaa na mtu mwingine sio wako100% lazima mtashare power ona jamaa kapoteza pesa kias gan kwa huyo mtoto huenda ameacha ata wazazi wake wanashindia ugali na cabbage kijijini.....VERY SAD ni kesi ngumu kuiamua
 
Habari wana JF.

Nina ndugu yangu mmoja upande wa mama, yeye KE.

Miaka kama 10 hivi iliyopita alikuwa ba mahusiano na Jamaa mmoja hivi, walikaa mda tuu mpaka mahusiano yao yakazaa mtoto. Lkn baada ya kujifungua Jamaa alimkwepa sister.

Si unajua wanaume wa kukimbia watoto wapo. Jamaa akawa hata huduma hatoi wala nini, ila mtoto anamtaka kumuoa kuna wakati alikuwa anajitokeza hata baada ya 3 month mara 1 tuu kumuona mtoto hatoi chochote. Baadae katokomea kabisa.

Sasa sister angu huyu akakutana na jamaa mwingine kipindi mtoto wake alikuwa na umri wa miaka 3 kwenda min.

Jamaa hakuwa tayari kuwanae siunajua single mother wanaume hatupendi sana, ila sister alijaribu kumshawishi mpk kukubali. Na alimueleza kila kitu kuhusu Baba mtoto.

Jamaa akasema kwa vile Baba mtoto kasepa kapotea basi tutakuwa fresh, ila alitoa sharti hataki kuona Baba mtoto anajitokeza au mama anajipendekeza.

Wakafanikiwa kufunga ndoa.
Na kuchukua mtoto wakawa wanakaa nae ndogo alipofikisha miaka 6 akampeleka shule mzuri ya 2million per year akawa anasoma huko.

Sasa Baba mtoto aliposikia bibie kaolewa si akarudi bwana kuanza kutaka mtoto. Sister akagoma kabisa tena bila kumwambia mume wake . Na arirudi kipindi sister anawatoto wadogo mapacha aliyezaa ba mume wake.

Waliangaishana kama mwaka 1 hivi. Sister alikataa kabisa kumpa dogo.

Sasa kipindi mtoto kafikisha miaka 8. Jamaa si akaenda ustawi wa jamii kwa lengo la kuchukua mtoto, sister kweli aliitwa ustawi wa jamaii na alienda tena bila kumwambia mume wake. Yeye alieleza kwao na kwao waligoma na kumwambia asiende. Ila ustawi wa jamii walilazimisha na kumwambia Mtoto anahaki ya kumjua Baba yake halisi. Hio ni haki ya mtoto.

Sasa mume wake baada ya kujua hilo akachachamaa kabisa ukawa ni ugomvi sana kati ya yeye na mke wake.
Mume wake akaamini kuwa Sister alimficha au niseme alimdanganya jamaa kakimbia kumbe laa. Waligombana sana.

Sasa jamaa akafanikiwa mpk kubadilisha jina mtoto la mwisho maana sister aliandika jina la kwao la mwisho la mtoto.
Jamaa akaweka jina la kwao. Na jina lake kwenye cheti cha kuzaliwa. Maana sehemu ya Baba ilikuwa empty nafikili.

Mume wake baada ya kuona hivyo akamwambia kuwa kuhusu kitu chochote cha mtoto wake asimwambie mpk ada. Na mtoto aende kwa Baba yake pale home kwake amtaki tena.

Sister akaona kwa vile anataka kuokoa ndoa yake ampeleke mtoto kwa Baba yake. Sasa ishu kule kwa jamaa , dogo alikuwa anasoma shule ya over 2 million per year. Jamaa wa kawaida tuu.

Kwa kifupi dogo baada ya kwenda kwa Baba mawasiliano yakazidi kupelekea mpk mume wake kuanza kugombana. Sister akasema yule mwenzie anamsumbua sana na anamfanya mtoto kama kung'ang'ania kumuona mama yake, mda wote.
So anajikuta mda mwingi anakuwa anawasiliana upande mwingine.

Baada ya kuona drama ni nyingi mume alimtimua sister home kwake. Na walisumbuana kama 2 years kutaka kuachana.
Mume wake ni mtu mwenye wivu. Walitaka kusuruhisha kwa kumuita jamaa yule msumbufu ila jamaa aligoma kuja na wala mume wake alikataa kusikiliza suruhisho.
Wiki mbili zilizopita waliachana baada ya purukushani kwa miaka 2.

Alikuwa single mother na kuingia kwenye ndoa na mwishowe kaeudi tena single mother.
Dogo anasoma shule za kawaida tuu hizi japo ni private pia kule kashatoa shule ya bei kubwa.

Hivi ishu kama hii mnaisolve kivipi jamani, IKIJA KWENYE FAMILIA , KARIBUNI.
Kwanza dada anamakosa makubwa sana ambayo atayajutia maisha yake yote. Amepata mume anayempenda alafu anaanza kufichaficha suala la jamaa kudai mtoto. Bora angemwambia kuwa familia ya mtoto inamsumbua inataka mtoto jamaa angelizima faster Hilosuala.

Kuna jamaa alikutana na suala kama Hilo ambalo ni baya zaidi yaani mke wake alimdanganya kuwa ujauzito ni wakwake wa mtoto wa kwanza, asee baada ya mtoto kuzaliwa jamaa alishtuka lakini alitulia baada ya kuja kuzaliwa mtoto wa pili jamaa aliona watoto specie tofauti kabisa. Alichoamua ni kwamba olewake mtu aje aseme anadai mtoto atammaliza jumlajumla. Mpaka Leo kimyaaa.

Sasa dada alishindwaje kumwambia jamaa jambo dogo Hilo. Pia alishindwa kutii ushauri wawazazi wake wa kutokwenda ustawi wa jamii. Haya sasa kawa single mother marambili.
 
Aaa mimi kuna rafiki yake Dada mmoja alikuwa na jamaa mmoja hivi baadae si akabeba ujauzito jamaa akakimbia.
Alipojifungua akajifungua watoto mapacha 2 tena wakike tupu.

Yule Dada aliangaika nae ustawi wa jamii kudai child support, jamaa alikuwa kaajiriwa serikalini.
Mwishowe jamaa alionga maafisa ustawi wa jamii. Na kukana watoto si wake kule kule ustawi wa jamii.

Watu wakamwambia wa ustawi wa jamii kuwa jamaa kaonga pesa hutashida.
Yule dada anaondoka zake. Mama yake alifaliki siku nyingi tuu.
Baba yake akamwambia kuwa utakaa hapa hapa home kwa sasa nagalia jinsi ya kuwalea watoto wako.

Yule dada alipata shida mpk akawa yupo stable kipesa. Kwa sasa watoto wanaumri wa miaka 6 anawasomesha shule mzuri tuu ya over 1miilion per year. Anaishi kigamboni.

Alimtembelea sister angu siku moja alimpelekea zawadi kibao.

Jamaa nasikia kuna kipindi alikuwa anamtafuta wayamalize , alikuwa anaomba msamaha kwa baby mama. Ila kagoma kabisa na alimblock.

Nafikili jamaa huyu itakuwa ngumu kwenda tena ustawi wa jamii, maana alikana kule kule watoto. Sasa naona itakuwa ngumu kwake.
Nafikili anaumia sana moyoni jamaa.
Anavuna matunda ya ukatili aliomfanyia huyo dada. MUNGU wakwetu site
 
Kosa la kwanza alilofanya dada yako ni kutomshirikisha mume wake kuanzia mwanzo Hilo ni kosa kubwa Sana alilofanya angemshirikisha tangu awali jamaa angejua apambane vipi kiume na Kama jamaa yupo vzr kiuchumi angempeleka hata nje ya TZ mtoto akaishi

Anyway pole yake
Sahihi kabisa. Yaani angemshughulikia huyo jamaa mpaka aombe poo! Yaani kama Mimi ningesema mtoto ni wakwangu full stop. Alafu ningesema jamaa anaingilia ndoa yangu na nilikuwa namtafuta kitambo sana Kwa kuvuliga ndoa. Aloo! Angekiona Cha mtemakuni.
 
Mtu mpaka anakubali kuingia gharama zakukulelea mtoto wako Kama wake means jamaa kashamchukulia kuwa ni sehemu ya maisha yake,na Kama mtoto ni wakike basi naamini Wana bond kubwa sana na huyo jamaa na anaumia pia

Single mother wasio na akili ndo wanasababisha wanawake wengine tutukanwe Kila uchwao
 
Back
Top Bottom