Single mother utalindaje ndoa yako kama hili likitokea kwenye mahusiano yako mapya?

Single mother utalindaje ndoa yako kama hili likitokea kwenye mahusiano yako mapya?

Sisemi single mother wabaya sometimes wanakuwaga wamekomaa kiakili ila haya matatizo ni wanayatengeneza sana huyu kazingua mwenyewe hata kama ni mimi tupa kuleee

Issue fupi tu si ulishaachana nae, akitaka kumuona mtoto awasiliane na mimi nimpe muda wa kuja kwangu ,
 
Cha msingi ni kuwa na mkakati unahakikisha 💯 mumeo ndie awasiliane na mwanaume mwenzie kwa swala la mtoto ful stop
Exactly otherwise unarudi ulikotoka
Kuna mijitu hufanya makusudi pengine mlishaachana hivyo anafanya makusudi akuharibie ulipofika Yani hata bado unateseka yeye anaona una amani
 
Habari wana JF.

Nina ndugu yangu mmoja upande wa mama, yeye KE.

Miaka kama 10 hivi iliyopita alikuwa ba mahusiano na Jamaa mmoja hivi, walikaa mda tuu mpaka mahusiano yao yakazaa mtoto. Lkn baada ya kujifungua Jamaa alimkwepa sister.

Si unajua wanaume wa kukimbia watoto wapo. Jamaa akawa hata huduma hatoi wala nini, ila mtoto anamtaka kumuoa kuna wakati alikuwa anajitokeza hata baada ya 3 month mara 1 tuu kumuona mtoto hatoi chochote. Baadae katokomea kabisa.

Sasa sister angu huyu akakutana na jamaa mwingine kipindi mtoto wake alikuwa na umri wa miaka 3 kwenda min.

Jamaa hakuwa tayari kuwanae siunajua single mother wanaume hatupendi sana, ila sister alijaribu kumshawishi mpk kukubali. Na alimueleza kila kitu kuhusu Baba mtoto.

Jamaa akasema kwa vile Baba mtoto kasepa kapotea basi tutakuwa fresh, ila alitoa sharti hataki kuona Baba mtoto anajitokeza au mama anajipendekeza.

Wakafanikiwa kufunga ndoa.
Na kuchukua mtoto wakawa wanakaa nae ndogo alipofikisha miaka 6 akampeleka shule mzuri ya 2million per year akawa anasoma huko.

Sasa Baba mtoto aliposikia bibie kaolewa si akarudi bwana kuanza kutaka mtoto. Sister akagoma kabisa tena bila kumwambia mume wake . Na arirudi kipindi sister anawatoto wadogo mapacha aliyezaa ba mume wake.

Waliangaishana kama mwaka 1 hivi. Sister alikataa kabisa kumpa dogo.

Sasa kipindi mtoto kafikisha miaka 8. Jamaa si akaenda ustawi wa jamii kwa lengo la kuchukua mtoto, sister kweli aliitwa ustawi wa jamaii na alienda tena bila kumwambia mume wake. Yeye alieleza kwao na kwao waligoma na kumwambia asiende. Ila ustawi wa jamii walilazimisha na kumwambia Mtoto anahaki ya kumjua Baba yake halisi. Hio ni haki ya mtoto.

Sasa mume wake baada ya kujua hilo akachachamaa kabisa ukawa ni ugomvi sana kati ya yeye na mke wake.

Mume wake akaamini kuwa Sister alimficha au niseme alimdanganya jamaa kakimbia kumbe laa. Waligombana sana.

Sasa jamaa akafanikiwa mpaka kubadilisha jina mtoto la mwisho maana sister aliandika jina la kwao la mwisho la mtoto.

Jamaa akaweka jina la kwao. Na jina lake kwenye cheti cha kuzaliwa. Maana sehemu ya Baba ilikuwa empty nafikili.

Mume wake baada ya kuona hivyo akamwambia kuwa kuhusu kitu chochote cha mtoto wake asimwambie mpk ada. Na mtoto aende kwa Baba yake pale home kwake amtaki tena.

Sister akaona kwa vile anataka kuokoa ndoa yake ampeleke mtoto kwa Baba yake. Sasa ishu kule kwa jamaa , dogo alikuwa anasoma shule ya over 2 million per year. Jamaa wa kawaida tuu.

Kwa kifupi dogo baada ya kwenda kwa Baba mawasiliano yakazidi kupelekea mpk mume wake kuanza kugombana. Sister akasema yule mwenzie anamsumbua sana na anamfanya mtoto kama kung'ang'ania kumuona mama yake, mda wote. So anajikuta mda mwingi anakuwa anawasiliana upande mwingine.

Baada ya kuona drama ni nyingi mume alimtimua sister home kwake. Na walisumbuana kama 2 years kutaka kuachana.

Mume wake ni mtu mwenye wivu. Walitaka kusuruhisha kwa kumuita jamaa yule msumbufu ila jamaa aligoma kuja na wala mume wake alikataa kusikiliza suruhisho. Wiki mbili zilizopita waliachana baada ya purukushani kwa miaka 2.

Alikuwa single mother na kuingia kwenye ndoa na mwishowe kaeudi tena single mother. Dogo anasoma shule za kawaida tuu hizi japo ni private pia kule kashatoa shule ya bei kubwa.

Hivi ishu kama hii mnaisolve kivipi jamani, IKIJA KWENYE FAMILIA , KARIBUNI.
Ukute ulikua ww alafu hutwambii🤣
 
Sijawahi fIcha kinihusucho Kwa mwenzangu aisee
Kuna wenzenu u-single mom wanautaka kwa nguvu yaani kwa kulazimisha.
Unamuangalia binti wa watu, unamuonea huruma na unamtengenezea mazingira 100% kwa ajili yake lkn hataki.
Yeye anachoamua ndicho kiwe. Sasa mtu kama huyo akiolewa ndiyo si anakuwa mwiba kabisa.
Mtoto ni wa baba (mwanaume) ila yeye amebeba jukumu la mwanaume kwa lazima na mama yake.
Inatia hasira sana
 
Yaani unawasiliana na baba mtoto bila kumshirikisha mumeo na unajua msimamo wake juu ya mawasiliano na baba mtoto apo ndio tatizo linapoanzia inaonekana dada bado alikua anampenda baba mtoto na sio mumewe iyo ni dharau mbaya na ndipo usingle mama unapoonekana jau
 
Back
Top Bottom