G'taxi
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 6,625
- 8,639
Wanawake wa namna hyo nawajua sana mkuu,wana matusi na kashifa za kijinga kweli utadhani hakujua kua anashika mimba na hajaolewa,pale wanapoanza kutukana wanaume kwa njia za simu wanapaswa kufikishwa mahakamani ili wajutie matusi yao,kumekua na hiyo tabia hapa nchini imekithili sana sana,na wanaume kwa mioyo migumu na kuwahurumia hawa wanawake hua wanaamua kukaa kimya tu ila ukweli wanawake hawa wana tatizo kubwa sanaTuseme tu ukweli kuna wadada wengi au wamama siku hizi
wanaamua kuzaa tu.....hasa umri fulani ukifika
na wengine wanaamua kuzaa kabla hata wa kuzaa nae hajatokea...
Sasa kimbembe kinaanza anaposhika mimba....au akishazaa
na mtu ambae si ajabu hakuwa na mipango ya kuzaa na huyo mwanamke
Wadada wengine wanaamua kutumia mimba kulazimisha commitment
au ndoa......Asipopata hiyo ndoa au hiyo commitment ni kumlaani huyo
mwanaume na kutumia mimba au mtoto kama njia ya kumkomesha huyo mwanaume..
Siku hizi unakuta vilio vya wadada kuwa 'wanaume hivi na wanaume vile'
lakini ukweli sio wote walidanganywa wataolewa au waliahidiwa commitment
Wengine kupata mimba na kuzaa ilikuwa ni mipango yao binafsi..lakini wakishazaa
wanaanza kubadili maneno...utasema waliahidiwa kweli kuolewa
au waliahidiwa matunzo ya mtoto in the first place kabla hawajashika mimba...
Ni busara kwa kila mwanaume kushiriki matunzo ya mimba inayomhusu
na matunzo ya mtoto wake......lakini wote tunajua busara sio kila mtu anayo
na wadada wanaojichukulia maamuzi binafsi ya kuzaa ni busara pia wakaacha
kulialia.....kama vile maamuzi hayo yalikuwa ya watu wawili
na wengine husingizia kwa ndugu kuwa waliahidiwa ndoa...kumbe
ni maamuzi yake binafsi kuzaa.......dunia imebadilika....
tupunguze lawama tukabili changamoto za maamuzi yetu...