Habari zenu wanajukwaa hili.
Nimekaa nimefanya utafiti usiohusisha njia zote za research lakini nimetumia njia ya ukusanyaji wa takwimu ujulikanao kama "Observation method" na kubaini kwamba kuna tatizo kubwa sana linatengenezwa katika jamii ya sasa hasa upande wa malezi. Suala la Single mothers katika nyakati za sasa limekuwa kama fashion kabisa sijui shetani ametuzidi nguvu kiasi kwamba tunaona ni burudani tu au tunajua kuwa ni tatizo na tunapaswa kulitatua?
Leo naomba nizungumzie malezi ya watoto wa kiume. Kwa single mothers ambao wanalea watoto wa kiume. Jitahidi sana mtoto wako wa kiume achanganyike na wanaume kwa gharama yoyote ile. Mtafute ndugu au rafiki yako wa kiume ambae unamwamini sana.
(Namaanisha unaemwamini sana pia awe na hofu ya Mungu) awe anatumia muda mrefu kuwa nae hata siku za weekend ambazo haendi shule. Mruhusu aende nae sehemu ambazo atakutana na wanaume mbalimbali na atashuhudia jinsi wanaume wanavyotakiwa ku behave, ajifunze mwanaume anazungumzaje, ana react vipi, anafikiri vipi, anaamuaje mambo? Anaongeaje, anatumiaje maneno, anatembeaje? Anajenga vipi hoja zake.
Mtoto wa kiume aliyelelewa mazingira ya jinsia ya kike tu kuanzia mtoto hadi anapokuwa mtu mzima huwa anatabia tofauti na watoto wa kiume waliolelewa na familia zenye wazazi wa kiume na kike ,kwa upande wa asilimia kitabia huwa anauwezekano wa kuwa na tabia za kike hadi asilimia 60-70 za kike tu.
Kuanzia kuongea, kutembea, kubehave, kufanya maamuzi, ku react katika changamoto za maisha. Kitu ambacho kina leta changamoto katika kupambana katika maisha yake na kujikuta anaona ni bora awe upande wa wanawake kwasababu ndyo sehemu pekee anajiona yupo salama na anaendana nao.
Kuna tatizo tunalitengeneza ambalo tutashindwa kulitatua baadae kuhusu hawa watoto wa kiume. Tuwe makini sana.