Sintofahamu ya mpaka sasa Serikali haijawalipa watumishi mshahara wa mwezi wa mwezi Mei

Sintofahamu ya mpaka sasa Serikali haijawalipa watumishi mshahara wa mwezi wa mwezi Mei

Mpaka sasa si WAALIMU, MATABIBU wala MAAFISA WA JESHI waliopokea mishahara yao ya mwezi Mei 2023.

Hazina ya serikali inahitaji wastani wa bilioni zaidi ya mia sita kila mwezi kwa mishahara ya watumishi wa umma na nyingine zaidi ya bilioni 8 bilioni kwa malipo ya pensheni.

Watalaam mbalimbali wa mambo ya uchumi wanadai kuwa kuchelewesha kwa haki ya watumishi na wastaafu kwa ujumla inasababishwa na mipango duni pamoja matumizi makubwa yasio na tija kiuchumi. Viashiria vyote vinaonesha kuwa tatizo hili linaweza kuendelea kwa miezi kadhaa.

Vilevile imetajwa ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali fedha kama sababu kuu zinazolifanya taifa hili kukosa fedha kuwalipa wafanyakazi wake kwa wakati.

Sababu nyingine ya kucheleweshwa kwa mishahara ya watumishi wa umma ni kukosa vipaumbele kwa masuala muhimu na badala yake kuwaridhisha baadhi ya viongozi wake na wabunge ambao muda wao wa kupiga kelele Bungeni ni wa muda mfupi tofauti na mtumishi wa umma ambae anafanya kazi kwa zaidi ya miaka 30.

Kwa kipindi kirefu serikali imekuwa ikijigamba kuwa kupitia Mamlaka ya Ukunyaji Kodi (TRA) inakusanya Zaidi ya Trilinioni mOja kwa mwezi Swali la kujuliza ni je fedha hizo zimekuwa zikitoweka kutoka chanzo chake ambacho ni mamlaka ya TRA, ama hupotea zinapowasili katika wizara au sababu zote mbili?

Hivi karibuni wafanyabiashara katika soko lakimataifa la karikakoo waligoma kutokana na kuongezeka kwa mienendo ya rushwa na kubambikiwa kodi zisizo na muelekeo katiak sehemu zao za biashara.

Haya yanajiri huku watumishi wa umma wakisubiri mshahara yao hatua ambayo inaweza kuweka huduma za serikali kwa umma katika hali tete.

WASWAHILI SIKU ZOTE WANAMSEMO USEMAO KIKULACHO KI NGUONI MWAKO.
Acha kukurupuka wewe kwani mwisho wa mwezi umefika?

Kawaida serikali huanza kulipa mishahara kuanzia tarehe 25 ya kila mwezi sasa kama uliwahi kulipwa kabla ya hapo basi ilikuwa ni kwa sababu maalum na hasa sikukuu za kitaifa.
 
Back
Top Bottom