Sintofahamu ya mpaka sasa Serikali haijawalipa watumishi mshahara wa mwezi wa mwezi Mei

Sintofahamu ya mpaka sasa Serikali haijawalipa watumishi mshahara wa mwezi wa mwezi Mei

Pesa imeshakwapuliwa,unaanza mtindo wa wafanyabiashara kuikopesha serikali fedha ilipe mishahara,hili lilitokea awamu ya nne,linajirudia tena ya sita,

Serikali inawekwa mifukoni na baadhi wenye ukwasi
sure awamu YA NNE walikuwa wanakopa mishahara ya watumishi wa umma kwa Bakhresa , ila kwa sasa mfano mishahara ya mwezi April ilikopwa kwa GGM
 
Jf nayo uhuru umezidi Sana mishahara imeshalipwa lakini uzi unaachwa tu duh kipindi cha dicteta Magufuli huu uzi usingezagaa hapa
sure awamu YA NNE walikuwa wanakopa mishahara ya watumishi wa umma kwa Bakhresa , ila kwa sasa mfano mishahara ya mwezi April ilikopwa kwa GGM
 
Haijawahi kutokea nyuzi za mshahara zikadumu zaidi ya siku mbili, hali ni tete....
 
Watumishi semeni kitu hapa, mambo yametiki?

Sisi tulikataa kuajiriwa tuko paleeee, tunasubiri mpate mitaani kuchangamke
 
Kuna watumishi wa umma hawajapokea mshahara hadi sasa?
 
Ni k
Watumishi semeni kitu hapa, mambo yametiki?

Sisi tulikataa kuajiriwa tuko paleeee, tunasubiri mpate mitaani kuchangamke
Ni kweli kabisa watumishi ndio wanaozungusha pesa mtaani , mshahara ukitoka mitaa yote uchangamka wafanyabiashara nao wanapata ridhiki zao , kilio cha kuchelewa kwa mishahara maumivu si kwa watumishi tuu , kuanzia taasisi za kifedha na wafanyabiashara wa aina zote , yaani ipo hivi kiutaratibu ni kwamba HAZINA YA TAIFA ndio inayotoa pesa za mzunguko , ukiona HAZINA haina hela jua nchi inapumilia mashine .
 
Mpaka sasa si WAALIMU, MATABIBU wala MAAFISA WA JESHI waliopokea mishahara yao ya mwezi Mei 2023.

Hazina ya serikali inahitaji wastani wa bilioni zaidi ya mia sita kila mwezi kwa mishahara ya watumishi wa umma na nyingine zaidi ya bilioni 8 bilioni kwa malipo ya pensheni.

Watalaam mbalimbali wa mambo ya uchumi wanadai kuwa kuchelewesha kwa haki ya watumishi na wastaafu kwa ujumla inasababishwa na mipango duni pamoja matumizi makubwa yasio na tija kiuchumi. Viashiria vyote vinaonesha kuwa tatizo hili linaweza kuendelea kwa miezi kadhaa.

Vilevile imetajwa ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali fedha kama sababu kuu zinazolifanya taifa hili kukosa fedha kuwalipa wafanyakazi wake kwa wakati.

Sababu nyingine ya kucheleweshwa kwa mishahara ya watumishi wa umma ni kukosa vipaumbele kwa masuala muhimu na badala yake kuwaridhisha baadhi ya viongozi wake na wabunge ambao muda wao wa kupiga kelele Bungeni ni wa muda mfupi tofauti na mtumishi wa umma ambae anafanya kazi kwa zaidi ya miaka 30.

Kwa kipindi kirefu serikali imekuwa ikijigamba kuwa kupitia Mamlaka ya Ukunyaji Kodi (TRA) inakusanya Zaidi ya Trilinioni mOja kwa mwezi Swali la kujuliza ni je fedha hizo zimekuwa zikitoweka kutoka chanzo chake ambacho ni mamlaka ya TRA, ama hupotea zinapowasili katika wizara au sababu zote mbili?

Hivi karibuni wafanyabiashara katika soko lakimataifa la karikakoo waligoma kutokana na kuongezeka kwa mienendo ya rushwa na kubambikiwa kodi zisizo na muelekeo katiak sehemu zao za biashara.

Haya yanajiri huku watumishi wa umma wakisubiri mshahara yao hatua ambayo inaweza kuweka huduma za serikali kwa umma katika hali tete.

WASWAHILI SIKU ZOTE WANAMSEMO USEMAO KIKULACHO KI NGUONI MWAKO.
Tunagawa milioni 20 Kwanza mwenye timu za mipira.Wafanyakazi wasubiri
 
Fedha za magoli na za kuwapa wasani + wakata mauno zipo

Ova
 
Back
Top Bottom