Sio Aibu kwa Tanzania Kuagiza Chakula, Sukari, Mafuta ya Kula,Wakati Tuna Ardhi na Vyanzo Lukuki vya Maji? BigUP Sana Awamu6 Kusisimua Kilimo kwa BBT!

Tatizo ni akili mbovu ndugu, Wala siyo kuwa na rasilimali nyingi.
Unaweza ukawa una rasilimali nyingi sana lakini kama akili yako ni mbovu hizo rasilimali haziwezi kukusaidia kitu chochote kile, badala yake utaendelea kubaki kuwa mtu maskini na fukara wa kutupwa.


"Tuliwakataa, tuliwatenga na kuwaengua kabisa Watu weusi kwenye Mchakato wa maendeleo ya nchi na ujenzi wake kwa sababu HAWANA AKILI NZURI, endapo kama tungewajumuisha basi wangetuharibia mambo yetu mazuri yaliyopo Afrika ya Kusini leo hii."

Pieter W. Botha, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini enzi za Utawala wa ubaguzi wa rangi.
 
Paskali mwambia BASHE aache WEEZY kwa kisingizio cha uhaba wa bidhaa....Mama Kizimkazi kamuumbua majkuzi....Kitendo alicypofanya cha kuwapa wauza simu wa kariakoo kuagiza sukari ni UTAPELI aka MANJEGEKA.
Pascal Mayalla ni mnufaika wa mda mrefu wa mnyororo wa ufisadi wa kimfumo-mtandao wa Tanzania. Ni vigumu sana kumbadilisha mtu wa namna hiyo lakini ana haki ya kutoa maoni yake.

Tumheshimu tu, kwa sababu hajijui na anaamini kuna binadamu watanzania wamezaliwa waishi kwa anasa kwa gharama za watanzania mamilioni masikini. Hiyo ndiyo imani yake na huo ndio uelewa wake.
 
Paschal umeingia leo Tanzania na Afrika ya watu weusi?
Mtu mweusi hajiwezi kwa hiyo ni mtu tegemezi na omba omba.
 

Mayalla maana yake njaa ,basi atakuwa anaendeshwa na jina lake.
 
Umeongea ukweli kabisa ni kilimo chawa kwakweli
 
Acha uchawa wewe baba bbt mpaka sasa imeongeza uzalishaji kiasi gani nchini?
 
Mbona akuna chochote kilichofanyika ni maneno matupu tu...amesema hiki amesema hiki.
Nilijua takwimu hata ya kilimofulani cha kibiashara tumeongoza ukanda flani au Africa...
Tunakazi ya kufanya kwenye kilimo na sio hayo maneno matupu.
 
we acha tu, nigeria wana import refined oil na kuuza nje crude oil, dangote kajenga refinary wamekataa kumuuzia crude oil, ana import
 
Pamoja na kujikomba kote huku lakini bado mkeka ukitoka hola chali cha mende😁😁
 
Pascal wewe ni mwabdishi hujupaswa kusubiria kulishwa matangopori yaliyopikwa na kuwekewa sukari yaani maonyesho ya nane nane.
Je una picha ya shamba la mfano?
 
Tukumbuke wakati wa Magufuli yaliwahi kuletwa matrekta kwa ajili ya kilimo, matrekta hayo walipewa viongozi ambao waliyatumia kukokota matrela ya kubeba makontena bandarini, mengi yalikufa. Nenda Arusha, huko aliwahi kuenda kiongozi mmoja wa safu (cream) ya juu nchini na alikuta matrekta mapya yakiwemo yale yanayofanya kazi zote hukohuko shambani yakiwa yamenyofolewa vipuri! Mhe. Majaliwa aliliona hilo.
Nitakuazima tochi ukavitafute vile viwanda vya zana za kilimo Ubungo, Mbeya, Arusha, Mang'ula na Moshi, najua ukiwasha tochi usiku hautaviona labda uiwashe mchana huenda utabahatika kuyaona majengo yake.
Mvua zilinyesha sana na kusababisha mafuriko lakini zilipokata tukashindwa kuyatumia maji yaliyoanza kupungua mpaka yakakauka kabisa, na hivi sasa mabomba ya mamlaka za maji eti hayana maji huku waziri husika akizitembelea kujua kulikoni na kurudi bila jibu!
Toka kabla ya uhuru kwenye asili ya maonesho ya nanenane huko Nyanza zana za kilimo zimekuwa zikioneshwa na kuleta matumaini ila maonesho yakiisha na matumaini yanaisha. Huenda zana hizo zikiuzwa kwa wakulima haswa badala ya wale wa uzunguni na mambati mavX lavuda yatatumika kwenye kusudio na tukikumbuka kufufua viwanda vya zana za kilimo ambavyo sasa vinatengeneza bisikuti kama kile cha Ubungo huenda tutajaribu kulima na tufungue upatikanaji wa hizo zana kwa wote na bila kuhusisha siasa za kibaguzi.
Tanzania ni yetu sote na isiwe nongwa waziri kutembelea shamba la Zitto.
 
Waliposema unatafuta teuzi nilikuwa siwaelewi kumbe ni kweli bhana bandiko limekaa kichawa chawa
 
Mapinduzi ya Kilimo kwa bajeti ya TShs trilioni 1!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…