butron
JF-Expert Member
- Jun 3, 2013
- 5,640
- 7,943
Bajeti ya Kilimo Trilioni 1,alafu tunataka kufanya mageuzi?Mapinduzi ya kilimo Chawa.
Tanzania haina kilimo cha maana na kinacho tufanya tuonekane tunalima ni kwa sababu tunazungukwa na nchi zote zinazo lima lima, Hatuna uwezo wa kulisha nchi moja full.
Hakuna Mapinduzi ya kilimo bila mapinduzi ya elimu, vipi usha wahi tembelea shule zilizo kuwa za mchepuo wa kilimo? usha wahi zitembelea hivi karibuni ujioneee zilivyo kwa sasa? sasa hayo mageuzi yanatoka wapi?
Usha wahi tembelea vyuo vya kati vya kilimo uone vilivyo na hali mbaya? majengo yamekaa kama mabaki ya kambi za wapiganaji wa vita za Veitanam?Hayo mageuzi yanatoka wapi kama vyuo vya kilimo viko vile?
Kanda ya ziwa Pamba inashuka uzalishaju kila mwaka na watu walisha acha kulima hilo unalijua?Kahawa isha kufa na kuzikwa Kilimanjaro na Arusha, Unazungumzia mapinduzi yapi?
Kule Arusha yale majengo ya TFA kwa sasa ni madula ya vitu kutoka nje unazungumzia kilimo kipi?
Unajua wakulima wengi nikiwemo hata mimi huwa napambana kulima mwanzo mwisho hakuna hata asilimia 1 ya sapoti naipata kutoka Serikalini?
Kuna mageuzi ya kilimo bila mageuzi ya viwanda vya kilimo vikiwemo vya kusindika na pia vya kuzalisha pembejeo?
Usha wahi tembelea Super Market kubwa uone vyakula vingi vinatoka nje?
Inaonekana nyie CCM mna definition yenu kuhusu mageuzi ya kilimo.
70% ya bajeti inapelekwa kwenye matumizi ya ovyo!