Nipo jirani na msikiti,
Kuanzia saa 10 alfajiri,
Kuna shehe huyo amekuwa mtangazaji wa muda,
"Sasa hivi ni saa 10 dakika 20 ewe muislamu jiandae kuamka,
Swala swala,!
Na anaendelea kutaja muda mpaka inafika saa 11 alfajiri.."
Kwakweli hebu tunaomba msaada wenu,
Ni kweli hakuna namna ya kuamshana nyie tu bila kutukera sisi?
Au nchi hii yenu pekee yenu?
Kwani hamuwezi kutegesha alarm mkaamka wenyewe mpaka mpigiwe kelele za kuamshwa kutokea mbali?
Yaani tunatafuta pesa kwa shida,
Usingizi unakuja kwa shida,
Na asubuhi asubuh ukianza kupata usingizi mtamu unaamshwa kwa lazima
Nisameheni sana lakini mnakera walah wabilah!