Mkuu we bisha tu lakini ukweli ndio huo,
Ccm imekita mizizi yake mbali kwanza kwa kutumia mtaala ya elimu mibovu ambayo haitoi Cha maaana zaidi ya kujua kusoma na kuandika, ikawaaminisha kuwa bila ccm eti nchi haitawaliki,
Ikawafukarisha ili Kila siku wawe wanawaza watakula Nini badala ya kuwaza mstakabali wa nchi Yao,
Ikatengeneza vyama vya upinza fake ambavyo vimekuwa kama wake wenza vinashindana kunengua mbele ya bwana wao ccm ili vipendwe na vipate matumizi zaidi kwa ajili kusukuma siku,
Ccm itatoka tu madarakani siku wananchi maumivu ya mateso ya kufukarishwa kwa lazima yakifika mwisho wakashindwa kutofaitisha kuwa hai na kufa. Tofauti na hapo sioni dalili, ni Heri hata suala la viongozi wa kitaifa wangekuwa wanapatikana kama makocha wa timu ya taifa tungeleta kiongozi kutoka hata Croatia huko.