Sio rahisi kufanya biashara ukiwa umeajiriwa, mnaoweza mnamtumia njia Gani?

Sio rahisi kufanya biashara ukiwa umeajiriwa, mnaoweza mnamtumia njia Gani?

Private sector mkuu
Kwa private sector ni sahihi nilitaka niseme hiyo mishahara ni ya private sector.

Una option 2 tuu kama uko mjini na umeoa.
1.Uwekezaji wa mifuko isiyo yenye hasara kidogo sana(almost haipo) mutual funds eg UTT,Faida Fund nk hapo utanunua Kila mwezi vipande kulingana na bei iwe ndio njia Yako kuu ya biashara. Au Kuweka pesa Wekeza ya Vodacom.

Hasara ni kwamba hupati hela Bali unawekeza ya baadae japo una nafasi ya kuchukua hela Yako ukitaka.

2 .Kama una Mke sio Mwajiriwa basi huyo ndio mfanye mipango awe anasimamia biashara yenu mda wewe Ukiwa kazini kama anaelewa maana ya biashara lakini ila kama huna Mke basi ufanye biashara mwenyewe angalia kulingana na mazingira,hapa nilipo Kuna Mwalimu Huwa anafungua akitoka kazini kuamiza saa tisa Hadi saa 3 usiku.
 
huwajui vijana wewe
kama una mastore ukategemea camera tu
kimekulamba vibaya mno

Sio kutegemea camera peke yake. Unatakiwa ukague phyisical ila sio kushinda pale masaa yote.

Kuna namna nying tu ya kufanya hivyo.
 
Sio kutegemea camera peke yake. Unatakiwa ukague phyisical ila sio kushinda pale masaa yote.

Kuna namna nying tu ya kufanya hivyo.
dear
ndo maana baresa kaweka watoto wake kwenye vitengo vyote muhim na kisha ndugu zake
.....hizi biashara zetu ndogo ndogo
zina changamoto sana

naona uvivu tu kuandika ni kwa namna gani kijana anavyoweza take advantage ukiwa haupo mara kwa mara
kwanza kubadilishana namba na wateja
kijana wako kama anakua ndo ana total ya control ya wateja wako
anaweza asiguse bidhaa ila akaamua na yeye kufungua biashara kma yko
pembeni yako na akabeba wateja wooote
 
Ujariliamali na iwekezaji zote ni biashara, lakini ningumu kufanikiwa ujasiriamali pasipo uwepo wako wakati nirahisi kufanikiwa uwekezaji pasipo uwepo wako
 
Sasa hivi technologia imekua sana, Mifumo mingi ipo ya kusimamia biashara, CCTV camera zipo.

Huwezi kushindwa kufanya biashara kisa tu umeajiliwa.
utafeli vibaya sana. Hzo tech unazosemea zmetengenezwa na binadamu, udhaifu kibao. Umeme tu ukikatika watu wanakupga kama ngoma.
 
Oa kwanza afu hyo biashara mfungulie wife usiogope kutongozewa then usmchekee yaan mwambie kabisa hyo kazi ulomfungulia n yake akuibie kidogo akimtumia mamake maisha yasonge. Usije kuogopa kufanya jambo ati lazma uwepo wako ndo lisonge. Nimeenda kujinywagiza kwanza.
 
Me ajira yangu ata nikipotea week hamna anaejua. Tatizo waajiri wengi wanajipa umuhimu kazini ndio maana do 2 usipoonekana kila mtu anabwabwaja.
 
Shida wizi kwa watanzania ni kama upo kwenye DNA. Sasa kwa mfano mafisadi wana njaa Gani? Mbona hawaachi kuiba??
Hapo ndipo shida ilipo maana hawa mafisadi pesa walizonazo wanaweza kutumia miaka 100 kisha kuwaachia wajukuu ,vitukuu hadi vilembwe lakini hawatosheki.
 
Hapo ndipo shida ilipo maana hawa mafisadi pesa walizonazo wanaweza kutumia miaka 100 kisha kuwaachia wajukuu ,vitukuu hadi vilembwe lakini hawatosheki.
Sasa hao mafisadi wanaaksi tabia za watanzania, Tamaa, uchu na kutaka mafanikio ya haraka haraka. Mtu anaajiliwa serikalini mwaka mmoja tu anataka awe na nyumba Kali, gari Kali pisi Kali, avimbe Kila kiwanja wamjue
 
Back
Top Bottom