Sio Uchawi, hii ndio mbinu wanayotumia wakinga kuteka biashara kwa spidi kali na mfanikio makubwa, mbinu rahisi ambayo kabila lolote linaweza kutumia

Unaongea vitu as if hakunaga makosa, hakunaga biashara kubuma ikakosa wateja...hakunaga kutapeliwa...

Yaan unaongea as if biashara ni rahisi kufanya
Ni mjinga alafu anaona watu wengine ambao sio matajiri ni wajinga wanamatumiz mabaya ya ela, yaan jamiiforum imekua na wajinga wengi na washabiki wengi
 
Mnawapamba wakinga utafiiiri nini nachoweza kusema wamefanikiwa kwenye biashara ya nguo na vyonbo kariakoo ila wengi hawajafikia level ya kumiliki makampuni makubwa,viwanda mahotel kama unavyoona kwa wahaya na wachaga angalia biashara za mahotel au mashule kumbi bar, viwanda nambie kipi ch mkinga wakinga wapo tu kariakoo na njombe huko kwingine bado sana mnawapaisha tu ila watu washapiga gap kitambo
 
Biashara yoyote inaihitaji discipline ya pesa na uaminifu, kwa mwenyewe wataje wako, (clients ) na washiriki wako, makabila makubwa wengi hawaminiani kusaidiana na ushindani ni wingi miongoni mwao, wa chagga wa miaka ya 70s sio sawa na wa chagga wa siku hizi hawaminiani tena na hawasaidiani, wahaya hawapendani kwenye biashara wanapenda kushindana tu, kwa hiyo sio muujiza kwa kabila dogo kama wakinga kufanikiwa kwenye biashara za kwa miniana wala sio uchawi au ulozi wanajua kanuni za biashara
 
Kariakoo yupo jirani yangu mkinga asubuhi wakija wanakuja na hotpots kubwa chakula kutoka home marufuku kununua chakula.

By the way,ubahili siku zote ndo huifadhi shilingi so wanachokifanya ni sawa.
Kuna rafiki yangu mmoja toka kaskazini, aliniasa Sana kwa kusema " ukitaka kuwa tajiri, shurti uwe bahiri". Na hili nililiona kwani wakati sina hata banda na ninaishi nyumba ya kupanga, mwenzangu ana nyumba na guest house hapa mjini.
 
Wakuu wengi hupenda kuinuana lakini vipapai vipo, kubali au kataa vipo iwe vya kichawi kabisa au wivu tu wa kutotaka mtu azidiwe hivyo kuleta figisi za makusudi kabisa.

Makabila wanayosaidiana nawapongeza sana, lakini makabila mengine watu wao ni wavivu mno, na mtu mvivu huwa anapenda starehe, kumuinua huyo kiumbe ni kazi mnoo, utampa mtaji atakula.

Kama uliloandika ni kweli basi hongera kwao.
 
Niliwahi kibishi na Hawa jamaa ila Kuna vitu niling'amua kutoka kwao...
1. Ni mala chache kuona mkinga akizozana au kupigana na mwenziwe, mke/mume
2. Mkinga rafiki yake ni yule anayefanyanae biashara
3. Mkinga kumkuta kwenye maeneo ya anasa kama bar ni mala chache sana
4. Wakinga Wana umoja sana
5.Mkinga hata kama anaagiza na kuuza Mercedes Benz, chakula chake kinaagizwa Toka nyumbani.. kama nyumbani wanakula mabumunda naye atakula hayohayo na maji, kama kuna kande hivyohvyo.
6. Bora mkinga aagize ulanzi wa buku lakini siyo akanunue wine🤣🤣🤣🤣
 
Yalikua yanatoka mavitu gani mkuu
 
Nadhani nidhamu ndiyo msingi wao.

Wakikopeshana wana nidhamu ya kurudisha

Wakiinuka kwa kuinuliwa wanayo nidhamu ya wao kuwainua wengine pia

Wakiipata pesa wanayo nidhamu ya matumizi yake

Wakiwa na umoja wanayo nidhamu ya masharti yake


Sasa ndugu zangu; kuna mdau humu JF ameandika signature kuwa hakuna nidhamu ya uoga maana nidhamu yenyewe ndio uoga pia😂😂.

Kama ambavyo waisraeli wanamuogopa Mungu mmoja aliyejuu yao bila unafiki[Nidhamu] na wanapata maendeleo makubwa.

Basi vivyo hivyo tukifanikiwa kujenga nidhamu tutaendelea..... iwe ni kuogopa Mungu mmoja, Kuogopa mababu wamoja, kuogopa umoja mmoja, serikali moja[Japan] chochote kile. Nidhamu, nidhamu, nidhamu. Mnaosema makafara yanawasaidia, mimi nitamodify na kusema ni nidhamu [ilitokana na chochote ikiwamo kafara, kama ni kweli] inayowasaidia👊💪
 
Wafanyabiaashara wengi walikimbia kariakoo kwasababu ya huu mtindo wao, mtu alizoea kuuza kitu cha laki 1 kwa faida ya elf 30 ila mkinga alipofika anauza kwa faida ya elf 5, kiukweli wengi walikata tamaa.
Sasa wanafanikiwaje kwa faida ndogo hivyo ya laki kwa elfu 5?? Unless uniambie Wana volume Kubwa sana ya sales..
 
Location ndio factor, unakuta naishi kivule frel kumi uko Alaf muhind yeye yupo barabara ya pili tu apo
Mkinga naye anaishi wapi? Kiukweli discipline ya fedha huwa hatuna, angalia wafanyakazi wengi hapa nchini, wengi utawaona na vibegi wamebeba lakini huwezi kukuta kabeba mayai 2 ya kuchemsha, mkate slace 3, au maandazi/vitumbua na chungwa/ndizi mbivu from home... Yeye anataka saa 4 akagonge supu na chapati na chai (hapo elfu 3 mpaka 5 anakata)... Mchana hapo bado.. So waweza kukuta daily anatumia elfu 7 mpaka kumi wengine, na hapo mshahara labda ni laki 7 mpaka milioni moja. Sasa bado mambo ya nyumbani na maendeleo mengine... Hapo hakuna kutoboa aiseeee
 
Usipofunguka ndiyo watu wataendelea kupinga, Weka wazi soko lilipoungua nini vilitoka.. [emoji23]
 
Wewe ni mfanyabiashara mkuu??
 
Kama idadi ya wanachama wanaochangia mfuko ni 10,000 na kama wanaogawiwa fedha ya biashara kwa mwezi ni 10 itachukua miaka mingapi kwa wanachama wote kuwa wamechangiwa?
Bado haiondoi ukweli kwamba hiki ni kitendo ambacho kinapaswa kuwa mfano kwa wengine. Nimesoma makala moja ya bbc kuhusu kabila moja huko Nigeria (wa Igbo nadhani) wana mfumo huu huu ila approach tofauti... Wao wanawachukua vijana wa kabila lao toka kijijini na kuwaleta wawe wanauza kwenye biashara zao kwa kipindi cha kati ya miaka 3 mpaka 5. Baada ya hapo yule kijana akionekana amekomaa kibiashara bosi wake anamfungulia biashara yake na wanaachana. Bosi anaenda kijijini kuchukua mwingine na mzunguko unaendelea. Pia wana umoja wao maalumu kwa kusaidiana kwenye majanga mfano masoko yanavyoungua, au kuibiwa, kufiwa nk... Mpaka wana SACCOS zao na Vicoba vyao... Kwa ujumla wameendelea sana kwenye biashara
 
Ni kabila linaloongoza kuchukiwa Nigeria kwasababu ya kuwa na mafanikio makubwa sana na muungano wa kuinuana (apprenticeship), Nigeria kulikuwa na vita dhidi ya hili kabila mwaka 1968 hadi 1970 , waliuwawa watu milioni 2 wa hili kabila, huko mji wao waliharibu kila kitu na miundombinu, kali kuzidi yote wale wafanyabiashara wakubwa akaunti zao zilifirisiwa...... jeshi la Nigeria walidhani wamewaweza ila kwa mfumo wao huo wa kuinuana ilichukua miaka 30 tu kusimama upya, kwa sasa ndilo kabila linaloongoza kwa kuwa na mafanikio makubwa lakini ni kabila hili hili liliathirika na vita, bila hio vita wangeuwa mara 4 ya hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…