Legrema2050
JF-Expert Member
- Jun 5, 2021
- 606
- 708
Ukatunduze maana yake niniUkatunduze ndio Siri Yao..asikudanganye mtu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukatunduze maana yake niniUkatunduze ndio Siri Yao..asikudanganye mtu.
Ni mjinga alafu anaona watu wengine ambao sio matajiri ni wajinga wanamatumiz mabaya ya ela, yaan jamiiforum imekua na wajinga wengi na washabiki wengiUnaongea vitu as if hakunaga makosa, hakunaga biashara kubuma ikakosa wateja...hakunaga kutapeliwa...
Yaan unaongea as if biashara ni rahisi kufanya
Biashara yoyote inaihitaji discipline ya pesa na uaminifu, kwa mwenyewe wataje wako, (clients ) na washiriki wako, makabila makubwa wengi hawaminiani kusaidiana na ushindani ni wingi miongoni mwao, wa chagga wa miaka ya 70s sio sawa na wa chagga wa siku hizi hawaminiani tena na hawasaidiani, wahaya hawapendani kwenye biashara wanapenda kushindana tu, kwa hiyo sio muujiza kwa kabila dogo kama wakinga kufanikiwa kwenye biashara za kwa miniana wala sio uchawi au ulozi wanajua kanuni za biasharaNi jamii ambayo ilikuwa haijulikani lakini hivi karibuni kutoitambua ni sawa na kusema hakuna kitu kwenye chumba mlichomo na tembo, hata kwa wanaofunga mizigo yao soko kubwa kuliko yote nchini pale kariakoo ni mashuhuda, hawa watu ni kama wameimeza kariakoo.
Sio mbinu ya wakinga, wao walichofanya ni kuiga tu, mbinu hii hutumika sanasana na wasomali ambao nao waliiga sehemu.
Mbinu ni nyepesi mno na ninahofia endapo kabila kubwa likiiga basi litakuwa mbali sana kimafanikio, mbali sanaaaa!!
Kinachofanyika ni swala la kuwa na umoja unaowaunganisha wakinga waliofanikiwa kuinuana.
Kunakuwa na umoja kwa mfano wanakuwa wakinga 500, kinacofanyika ni kwamba kila mwezi kila mtu awe mfanyabashara au kaajiriwa inabidi atoe elf 50, laki, laki 2, n.k kutokana na status yake, hata ukitoa M ni wewe tu.
Hapo kila mwezi huwa inapatikana takribani milioni 50
sasa kitachofanyika hapo, hio pesa wataikopa bila riba familia ambayo wanaona inaweza kuhimili biashara, huwa wanakopa familia na sio mtu binafsi kwasababu familia ina nguvu kazi na inawajibika zaidi kuliko mtu binafsi.
Katika familia hio kuna mtu moja wao anaenda jiji la Guangzou huko China, huu ni mji mkubwa wa kibiashara wenye bandari na kuna wakinga wengi sana kuliko kabila lolote linalotokea hapa kwetu, hivyo mwenzao akifika huko inakuwa rahisi kuwa na wenyeji, wenzake watampiga shule ayajue machimbo ya huko Guangzhou ya kununua bidha, watamfundisha kujitahadhari na utapeli, watampa connections, watamfundisha jinsi ya kusafirisha bidhaa kwa wenzake wa bongo, n.k.
akimaliza mafunzo atapokea ile hela waliyochangiwa ili anunue mzigo ausafirishe kuja huku bongo, uzuri ni kwamba wana kampuni yao ya kusafiisha inaitwa mapembelo cargo, mzigo ukifika huku bongo basi wenzake wa upande wa huku kwetu ndio watakuwa wanashughulika na kuuza .
Familia hiyo iliyochangiwa nayo itakuwa mwanachama mpya wa umoja wa kuchangiana kila mwezi huku wakiwa wanalipa marejesho ya ule mkopo, ndio maana wengi inabidi wajibane matumizi kisawasawa, si ajabu kukuta mtu ana duka kubwa limejaa ila anagonga kande.
Halafu pia silaha yao kuu huwa ni kuuza kwa faida ndogo, bidhaa aliyoagiza kwa elf 50 yupo radhi auze hata kwa faida ya elf 52, hiki ndio kitu kilichowanya hata wachaga wapungue pale kariakoo maana ukienda duka la mchaga nataka faida kubwa.
sasa sipati picha kabila kama wasukuma, wachaga, wanyakyusa, wahaya, hawa wenye idadi ya watu milioni 2 na zaidi wajikusanye wawe na umoja wa watu hata elf 10 tu wawe wanachangiana hata elf 50 kila mwezi,
watu elf 10 x shilingi 50,000 = milioni 500 pesa taslimu
kiasi hicho kwe kinagawanywa shilingi milioni 50 kwa watu 10 kila mwezi sawa na wati 120 kila mwezi, kati ya hao 120 wafanikiwe hata 50 tu kila mwezi.... sijui hata nguvu ya kulinganishana nao mtu ataitoa wapi.
Kuna rafiki yangu mmoja toka kaskazini, aliniasa Sana kwa kusema " ukitaka kuwa tajiri, shurti uwe bahiri". Na hili nililiona kwani wakati sina hata banda na ninaishi nyumba ya kupanga, mwenzangu ana nyumba na guest house hapa mjini.Kariakoo yupo jirani yangu mkinga asubuhi wakija wanakuja na hotpots kubwa chakula kutoka home marufuku kununua chakula.
By the way,ubahili siku zote ndo huifadhi shilingi so wanachokifanya ni sawa.
Nafikiri mtu asiyejua kuwa kuna ushirikina na uchawi duniani mtu huyo hajitambui kabisa.Mtu anayeamini kuna ushirikina karne hii ni zwazwa.
Yalikua yanatoka mavitu gani mkuuKafara za wakinga sii za leo, ni za kitambo ila kwa siku za usoni wamezihuisha na kuziboresha zaidi.
Ukienda makambako na mwanjelwa ukapata fursa ya kuingia ktk maduka yao utajifunza kitu.
Mimi niliona kwa macho yangu wakati mwanjelwa ilipoungua yaliyokuwa yanatoka mle madukani Mungu ndoa ajuaye
Sasa wanafanikiwaje kwa faida ndogo hivyo ya laki kwa elfu 5?? Unless uniambie Wana volume Kubwa sana ya sales..Wafanyabiaashara wengi walikimbia kariakoo kwasababu ya huu mtindo wao, mtu alizoea kuuza kitu cha laki 1 kwa faida ya elf 30 ila mkinga alipofika anauza kwa faida ya elf 5, kiukweli wengi walikata tamaa.
Mkinga naye anaishi wapi? Kiukweli discipline ya fedha huwa hatuna, angalia wafanyakazi wengi hapa nchini, wengi utawaona na vibegi wamebeba lakini huwezi kukuta kabeba mayai 2 ya kuchemsha, mkate slace 3, au maandazi/vitumbua na chungwa/ndizi mbivu from home... Yeye anataka saa 4 akagonge supu na chapati na chai (hapo elfu 3 mpaka 5 anakata)... Mchana hapo bado.. So waweza kukuta daily anatumia elfu 7 mpaka kumi wengine, na hapo mshahara labda ni laki 7 mpaka milioni moja. Sasa bado mambo ya nyumbani na maendeleo mengine... Hapo hakuna kutoboa aiseeeeLocation ndio factor, unakuta naishi kivule frel kumi uko Alaf muhind yeye yupo barabara ya pili tu apo
Usipofunguka ndiyo watu wataendelea kupinga, Weka wazi soko lilipoungua nini vilitoka.. [emoji23]Kafara za wakinga sii za leo, ni za kitambo ila kwa siku za usoni wamezihuisha na kuziboresha zaidi.
Ukienda makambako na mwanjelwa ukapata fursa ya kuingia ktk maduka yao utajifunza kitu.
Mimi niliona kwa macho yangu wakati mwanjelwa ilipoungua yaliyokuwa yanatoka mle madukani Mungu ndoa ajuaye
Wewe ni mfanyabiashara mkuu??Mimi ni mkinga,Uliloliongea kuhusu kafara sio wote,ila ni imani za koo na mambo ya mtu binafsi ambayo hupatikana kila kabila.Binafsi sijawahi shuhudia kafara miaka yangu yote.Ila wengi tunadumisha tu mila za kuwaenzi mababu zetu na asili yetu.Kumbuka tulikuwa na dini zetu kabla ya dini hizi za wazungu na waarabu.
Bado haiondoi ukweli kwamba hiki ni kitendo ambacho kinapaswa kuwa mfano kwa wengine. Nimesoma makala moja ya bbc kuhusu kabila moja huko Nigeria (wa Igbo nadhani) wana mfumo huu huu ila approach tofauti... Wao wanawachukua vijana wa kabila lao toka kijijini na kuwaleta wawe wanauza kwenye biashara zao kwa kipindi cha kati ya miaka 3 mpaka 5. Baada ya hapo yule kijana akionekana amekomaa kibiashara bosi wake anamfungulia biashara yake na wanaachana. Bosi anaenda kijijini kuchukua mwingine na mzunguko unaendelea. Pia wana umoja wao maalumu kwa kusaidiana kwenye majanga mfano masoko yanavyoungua, au kuibiwa, kufiwa nk... Mpaka wana SACCOS zao na Vicoba vyao... Kwa ujumla wameendelea sana kwenye biasharaKama idadi ya wanachama wanaochangia mfuko ni 10,000 na kama wanaogawiwa fedha ya biashara kwa mwezi ni 10 itachukua miaka mingapi kwa wanachama wote kuwa wamechangiwa?
Sahihi,kama ID yangu inavo nitambulishaWewe ni mfanyabiashara mkuu??
Ni kabila linaloongoza kuchukiwa Nigeria kwasababu ya kuwa na mafanikio makubwa sana na muungano wa kuinuana (apprenticeship), Nigeria kulikuwa na vita dhidi ya hili kabila mwaka 1968 hadi 1970 , waliuwawa watu milioni 2 wa hili kabila, huko mji wao waliharibu kila kitu na miundombinu, kali kuzidi yote wale wafanyabiashara wakubwa akaunti zao zilifirisiwa...... jeshi la Nigeria walidhani wamewaweza ila kwa mfumo wao huo wa kuinuana ilichukua miaka 30 tu kusimama upya, kwa sasa ndilo kabila linaloongoza kwa kuwa na mafanikio makubwa lakini ni kabila hili hili liliathirika na vita, bila hio vita wangeuwa mara 4 ya hapaBado haiondoi ukweli kwamba hiki ni kitendo ambacho kinapaswa kuwa mfano kwa wengine. Nimesoma makala moja ya bbc kuhusu kabila moja huko Nigeria (wa Igbo nadhani) wana mfumo huu huu ila approach tofauti... Wao wanawachukua vijana wa kabila lao toka kijijini na kuwaleta wawe wanauza kwenye biashara zao kwa kipindi cha kati ya miaka 3 mpaka 5. Baada ya hapo yule kijana akionekana amekomaa kibiashara bosi wake anamfungulia biashara yake na wanaachana. Bosi anaenda kijijini kuchukua mwingine na mzunguko unaendelea. Pia wana umoja wao maalumu kwa kusaidiana kwenye majanga mfano masoko yanavyoungua, au kuibiwa, kufiwa nk... Mpaka wana SACCOS zao na Vicoba vyao... Kwa ujumla wameendelea sana kwenye biashara
Kwa nini mkuuUkiwa nae hakikisha hutembei nje ya ndoa.