Sio ujinga kutumia sabuni ya unga na kipande kwa pamoja wakati wa kufua nguo?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Huwa naona watu wanatumia sabuni za aina mbili katika kufua, mtu analoweka nguo kwa sabuni ya unga kisha baadaye anatumia sabuni ya kipande wakati anazifua!

Sasa hii maana yake huwa ni nini? Kwamba sabuni ya unga haitoshi kutakatisha nguo wakati wa kufua? Sijawahi kuolewa mantiki ya hili jambo.
 
haha! mi nafikiri inategemea na nguo za nani! kama za mtoto sawa maana watoto kwenye kuchafua tu mh! wako njema lkn mtu mzima unavaa siku moja ama masaa tu umevua sabuni mbili zanini...????

nishasahau hata kama hua kuna sabuni za kipande!!
 
Kwa ufupi ni ujinga.

Walio wengi hatupendi na hatuna muda wa kujua ndiyo maana tunapata madhara, why?.

Sabuni ya unga inapaswa kuwekwa kwenye maji kwa kipimo kulingana na wingi wa nguo, kisha fikicha kuunda povu hadi zile chenga ziyeyuke, povu litapanda ndiposa unaweka nguo.

Kila sabuni ya unga ina maelekezo yake ila nyingi zinakutaka uache nguo kwa 30dkk ni hadi povu liishe, ndipo unaanza kufua.

Ipo hivi, kuungua/kuchubuka kwa viganja kunatokana na kuweka sabuni ya unga na muda huo huo unaanza kufua, sabuni ya unga siyo maalum kwa matumizi hayo.

Hivyo basi ukiona mtu anatumia sabuni ya unga na kipande ni MJINGA, hajui na analazimisha kutoa uchafu kwenye nguo badala ya kutakatisha.

Mwisho, ukiloweka nguo na sabuni ya unga kwa muda huo hapo juu, hutotumia nguvu kufua nguo zako sababu tayari sabuni inakuwa imenyonya uchafu na inasuburi kuufikicha na kuukamua.

ONYO: Unapoloweka nguo zako usichanganye na zinazotoa rangi.
Asante.
 
Ukiitumia sabuni ya unga, inatakiwa uloweke nguo kwa takribani dk. 30 +.

Watu wengi hatuloweki na kusubiri.
Tunaanza kufua kabla ya uchafu kulegea. Unakuta sabuni ya unga haijafanya kazi yake, hivyo tunatumia ya kipande maana ina instant impact ya kuondoa uchafu bila kusababisha joto na michubuko mikononi kama sabuni za unga.

Kisha inakuwa mazoea.
 
Sabuni nyingi za unga povu lake linaisha mapema wakati mwingine inabidi kutumia na sabuni ya kipande.
ya kweli aya mkuu au unatumia maji ya chumvi?
maana mimi ufuaji wangu natumia sabuni ya unga na likija swala la kusuuza nguo lazima utumie maji mengi maana sabuni inakuwa nyingi sana imebaki kwa nguo
 
Huwa naona watu wanatumia sabuni za aina mbili katika kufua, mtu analoweka nguo kwa sabuni ya unga kisha baadaye anatumia sabuni ya kipande wakati anazifua!

Sasa hii maana yake huwa ni nini? Kwamba sabuni ya unga haitoshi kutakatisha nguo wakati wa kufua? Sijawahi kuolewa mantiki ya hili jambo.
Haujawahi kukutana na maji magumu mpaka ukiweka mkono hivi unahisi kabisa hapa sabuni ya kipande inagonga mwamba , sasa kulainisha ndo unaweka ya unga yakishakuwa soft unapiga na ya kipande .

Hope umepata kitu.
 
Hapana sijapata kitu, sijaelewa hii concept, ninachofamu maji magumu wengi huwa wanatumia sabuni za magadi mengi.
 
Sio mpenzi kabsa wa kutumia sabuni za unga,,, yaani nitatafta sabuni ya kipande yenye povu jiiiingi,, kwaio sijui kama ni ujinga au werevu
 
Kwa ufupi ni ujinga.

Walio wengi hatupendi na hatuna muda wa kujua ndiyo maana tunapata madhara, why?.

Sabuni ya unga inapaswa kuwekwa kwenye maji kwa kipimo kulingana na wingi wa nguo, kisha fikicha kuunda povu hadi zile chenga ziyeyuke, povu litapanda ndiposa unaweka nguo.

Kila sabuni ya unga ina maelekezo yake ila nyingi zinakutaka uache nguo kwa 30dkk ni hadi povu liishe, ndipo unaanza kufua.

Ipo hivi, kuungua/kuchubuka kwa viganja kunatokana na kuweka sabuni ya unga na muda huo huo unaanza kufua, sabuni ya unga siyo maalum kwa matumizi hayo.

Hivyo basi ukiona mtu anatumia sabuni ya unga na kipande ni MJINGA, hajui na analazimisha kutoa uchafu kwenye nguo badala ya kutakatisha.

Mwisho, ukiloweka nguo na sabuni ya unga kwa muda huo hapo juu, hutotumia nguvu kufua nguo zako sababu tayari sabuni inakuwa imenyonya uchafu na inasuburi kuufikicha na kuukamua.

ONYO: Unapoloweka nguo zako usichanganye na zinazotoa rangi.
Asante.
Nadhani,, Tuishie Hapa.
 
Back
Top Bottom