Kwa ufupi ni ujinga.
Walio wengi hatupendi na hatuna muda wa kujua ndiyo maana tunapata madhara, why?.
Sabuni ya unga inapaswa kuwekwa kwenye maji kwa kipimo kulingana na wingi wa nguo, kisha fikicha kuunda povu hadi zile chenga ziyeyuke, povu litapanda ndiposa unaweka nguo.
Kila sabuni ya unga ina maelekezo yake ila nyingi zinakutaka uache nguo kwa 30dkk ni hadi povu liishe, ndipo unaanza kufua.
Ipo hivi, kuungua/kuchubuka kwa viganja kunatokana na kuweka sabuni ya unga na muda huo huo unaanza kufua, sabuni ya unga siyo maalum kwa matumizi hayo.
Hivyo basi ukiona mtu anatumia sabuni ya unga na kipande ni MJINGA, hajui na analazimisha kutoa uchafu kwenye nguo badala ya kutakatisha.
Mwisho, ukiloweka nguo na sabuni ya unga kwa muda huo hapo juu, hutotumia nguvu kufua nguo zako sababu tayari sabuni inakuwa imenyonya uchafu na inasuburi kuufikicha na kuukamua.
ONYO: Unapoloweka nguo zako usichanganye na zinazotoa rangi.
Asante.