Sioni ni kwanini askari wasizime vurugu za Oktoba 29, 2025 kwa risasi. Ningewashangaa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Askari wanapopewa ripoti ya uhakika kuwa wafanyavurugu wamevamia vituo vya polisi kuua polisi na kupora silaha na sare za jeshi la polisi unadhani anaepewa ripoti hiyo atatuma askari kwenye tukio la kuzima vurugu waliobeba virungu, filimbi na pingu tu? Hapohapo kumbuka askari wengi walikuwa wamesambazwa kwenye zoezi la kupiga kura. Hivyo unatuma askari wachache kwenda kuzuia vurugu za watu wengi sana waliotawanyika sehemu kubwa ya miji na mikoa.

Ratio ya polisi kwa wafanya vurugu ilikuwa ndogo sana (askari: wafanya vurugu), inaweza kuwa 1:100,000. yaani polisi mmoja kwa wafanya vurugu 100,000. uwiano kama huu bila kutumia risasi za moto ungeweza kusababisha askari wengi kuuliwa na wafanyavurugu na mali nyingi sana za umma na watu binafsi zingeharibiwa nyingi sana.

Kila mtu angemshangaa aliyepeleka askari wachache kinyonge vitani.
 
Mama au baba yako angepigwa risasi usingeandika huu ujinga wako. Kwa sababu kuna ushahidi uliotolewa wa kuonesha wazi siyo watu wote walio uwawa walikuwa ni waandamanaji.
Kama wale waliokuwa kibanda umiza wanaangalia movie,wakashindiliwa wote risasi humo humo!
Huyo mtu ananufaika na Nini hasa mpaka umwagaji damu holela wa wa Tanzania wenzake aone ni jambo la haki na walistahili?
Huenda ni mzanzibar ndio maana anaona safi tu!
 
Unapotumwa kwenda kuzuia vurugu za watu ambao miongoni mwao wana silaha na wamevaa sare za polisi hiyo ni vita ya silaha kaka. Bahati mbaya sana inafahamika tangu kale kuwa vita haina macho. Waliosema vita haina macho walikuwa watu wenye akili zilizokomaa.
Unapomlenga adui kuna kukosa shabaha na kuna risasi kupitiliza. Lakini kuna adui kugeuza ngao watu wema, na kuna adui kukimbilia majumbani na sehemu za mikusanyiko.
 
Askari wanapopewa ripoti ya uhakika kuwa wafanyavurugu wamevamia vituo vya polisi kuua polisi na kupora silaha na sare za jeshi la polisi unadhani anaepewa ripoti hiyo atatuma kwenye tukio la kuzima vurugu askari waliobeba virungu tu? Hapohapo kumbuka askari wengi walikuwa wamesambazwa kwenye zoezi la kupiga kura. Hivyo unatuma askari wachache kwenda kuzuia vurugu za watu wengi sana waliotawanyika pia sehemu kubwa.
Kwa akili hizi CCM watatawala mpaka ufe.
MTU anauwa wewe unaona Jambo la kawaida tuu, ndo maana hamuoni ajabu kuwadhalilisha wananchi makalioni.
 
Askari wanapopewa ripoti ya uhakika kuwa wafanyavurugu wamevamia vituo vya polisi kuua polisi na kupora silaha na sare za jeshi la polisi unadhani anaepewa ripoti hiyo atatuma kwenye tukio la kuzima vurugu askari waliobeba virungu tu? Hapohapo kumbuka askari wengi walikuwa wamesambazwa kwenye zoezi la kupiga kura. Hivyo unatuma askari wachache kwenda kuzuia vurugu za watu wengi sana waliotawanyika pia sehemu kubwa.

View: https://www.facebook.com/reel/1647463820331517
 
Askari wanapopewa ripoti ya uhakika kuwa wafanyavurugu wamevamia vituo vya polisi kuua polisi na kupora silaha na sare za jeshi la polisi unadhani anaepewa ripoti hiyo atatuma kwenye tukio la kuzima vurugu askari waliobeba virungu tu? Hapohapo kumbuka askari wengi walikuwa wamesambazwa kwenye zoezi la kupiga kura. Hivyo unatuma askari wachache kwenda kuzuia vurugu za watu wengi sana waliotawanyika pia sehemu kubwa.
A single condom would have saved us from this idiot
 
Kama wale waliokuwa kibanda umiza wanaangalia movie,wakashindiliwa wote risasi humo humo!
Huyo mtu ananufaika na Nini hasa mpaka umwagaji damu holela wa wa Tanzania wenzake aone ni jambo la haki na walistahili?
Huenda ni mzanzibar ndio maana anaona safi tu!
Hakuna askari fala wewe!! Wewe umelala na mkeo ndani unakoroma wakati yeye yuko nje anakimbizana na majambazi wenye silaha. kama wangekuwa mafala wangeuliwa kila siku. Unamkimbiza mtu aliyemuua askari mwenzako halafu mtu huyo anakimbilia kibanda umiza na watu wa kibanda umiza wanamcover na kumuona shujaa, hapo lazima mtasema tu. Watu wakishapora silaha za kijeshi zoezi zima linageuka la kijeshi hadi hapo silaha zote zitakapopatikana zote kwa 100% na adui ku retreat.

Hakuna amani wala maelewano wala kuhoji kama nchi uliyoapa kuilinda inawaka moto kila pahali kila kona. Hakuna muda wa kuchambua aina ya adui na sababu zake as long as nchi inateketea. Hakuna raia mwema anaepora sila na sare za jeshi.
 
Lakini kuna adui kugeuza ngao watu wema, na kuna adui kukimbilia majumbani na sehemu za mikusanyiko.
Unachotetea ni hichi:

Mhalifu anapokimbilia nyumbani ua familia nzima pamoja na huyo mhalifu Sababu ni vita isiyo na macho.

Sikia kavulata, Watu waliouwawa wakiwa majumbani walinyimwa haki ya kuishi hata kama utatetea kwa maslahi unayoyajua wewe.

Achilia mbali ukatili wa kuua mhalifu aliyejificha kwa woga pia hatupaswi kuua raia wema sababu kuna wahalifu katikati yao wamejificha.
 
A single condom would have saved us from this idiot
Sijui wewe ulinusurika vipi mtu wa hovyo kama wewe. Umetuma watoto wa watu wakapambane na makomandoo wanaoilinda nchi, raia na mali zao halafu wewe ukajificha na wanao. Pumbavu
 
Pongezi kwa jeshi la polisi kudhibiti wezi, magaidi na wavunja amani!
 
Hakuna askari fala wewe!! Wewe umelala na mkeo ndani unakoroma wakati yeye yuko nje anakimbizana na majambazi wenye silaha. kama wangekuwa mafala wangeuliwa kila siku. Unamkimbiza mtu aliyemuua askari mwenzako halafu mtu huyo anakimbilia kibanda umiza na watu wa kibanda umiza wanamcover na kumuona shujaa, hapo lazima mtasema tu. Watu wakishapora silaha za kijeshi zoezi zima linageuka la kijeshi hadi hapo silaha zote zitakapopatikana zote kwa 100% na adui ku retreat.

Hakuna amani wala maelewano wala kuhoji kama nchi uliyoapa kuilinda inawaka moto kila pahali kila kona. Hakuna muda wa kuchambua aina ya adui na sababu zake as long as nchi inateketea. Hakuna raia mwema anaepora sila na sare za jeshi.
Ndio maana kundi Moja linatumia nguvu ya Kila namna kuendelea kubaki madarakani!Hofu ni kuwa Kuna watu watawajibishwa kwa maisha ya watu yaliyodhulumiwa!Uzuri Jinai Haina ukomo,siku Moja damu iliyomwagika itakuja kulipwa,sio tu ya 0ct 29 bali hata kabla ya hapo!
Utekaji na mauwaji ya watu wanaotofautiana na serikali ya CCM yatafikia tamati,hiyo siku itakuja na mtu haijalishi ni Mzee,magereza au kunyongwa yatamhusu!
 
Unachotetea ni hichi:

Mhalifu anapokimbilia nyumbani ua familia nzima pamoja na huyo mhalifu Sababu ni vita isiyo na macho.

Sikia kavulata, Watu waliouwawa wakiwa majumbani walinyimwa haki ya kuishi hata kama utatetea kwa maslahi unayoyajua wewe.

Achilia mbali ukatili wa kuua mhalifu aliyejificha kwa woga pia hatupaswi kuua raia wema sababu kuna wahalifu katikati yao wamejificha.
sikia wewe jamaa, hata mimi na wanangu tulikuwa mitaa hiyohiyo waliokufa watu, mimi na wanangu tulitii amari ya kubaki ndani ya nyumba hata kama tulikuwa na shida ya kutoka nje. Hii ilinifanya mm na wanangu hakuna aliyeguswa hata mmoja. Kama askari walikuwa wanaingia tu kila nyumba kuua watu basi hata mmi na wanangu tungekufa, maana tulikuwa tunawaona aaskari wakipita mitaani wakikimbizana na wafanya vurugu.
 
Mimi sijafa, familia yangu haikufa, sisi kuwa hai haimaanishi tusilaani matumizi mabaya ya silaha yaliyotokea. Kufanya hivyo ni kutowatendea haki raia walionyimwa haki ya kuishi sababu sisi hatukufikiwa.

Mimi nafahamu aliyekufa na hakuwa akiandamana. Tena ni mzee, alikuwa nyumbani kwake. Kuna mazingira hata ya video tumeshuhudia askari angeweza kupiga risasi hewani na watu wakaendelea kutawanyika sababu raia walikuwa wakikimbia ila askari akachagua kuelekeza bunduki kwenye mwili wa binadamu, halafu unamtetea askari wa aina hiyo?

Kesho huyu askari akiwa anakabiliana na mhalifu bila ulazima akaelekeza risasi kwenye mwili wa mmoja wa familia yako na kumnyima haki ya kuishi majirani waliobaki hai wamtetee Sababu hawajauliwa?

Utamaduni uwe ni waliobaki hai kutetea collateral damage hata ambayo inazuilika sababu huwajauliwa?

Kuna mambo tunatakiwa tuache tofauti zetu na tuyalaani kwa pamoja.

Halafu, Kati ya wewe na tume iliyotoa ripoti ya uwepo wa matumizi mabaya ya silaha nani muongo? Kwanini imeundwa tume ya jinai? Usitetee uhalifu, kama ambavyo unapinga uhalifu wa kuchoma vituo unapaswa kupinga uhalifu wa kuua raia wema.
 
Ndio maana kundi Moja linatumia nguvu ya Kila namna kuendelea kubaki madarakani!Hofu ni kuwa Kuna watu watawajibishwa kwa maisha ya watu yaliyodhulumiwa!Uzuri Jinai Haina ukomo,siku Moja damu iliyomwagika itakuja kulipwa,sio tu ya 0ct 29 bali hata kabla ya hapo!
Utekaji na mauwaji ya watu wanaotofautiana na serikali ya CCM yatafikia tamati,hiyo siku itakuja na mtu haijalishi ni Mzee,magereza au kunyongwa yatamhusu!
Wazazi wameshindwa malezi ya watoto wao hadi watoto wao ikawa rahisi kudanganywa na akina Mangi Kimambi ambao hawako hapa. Mzazi ukishindwa kumlea mwanao subiri vilio nyumbani kwako. Wewe hushangai watoto wa Lissu, Heche, Mnyika, Lema, Sugu, Mbowe, Mbatia, Mpina, Warioba hakuna hata mmoja aliyeshiriki kwenye vurugu zile. Ni watoto wa wazazi malofa tu.
 
Hizo ni kauli za mtu aliyelewa madaraka au mnufaika wa mfumo!Mfumo kandamizi ndio unawafanya kuwa na jeuri ya kuona maisha ya binadamu ni kama ya nzi,tena mnasema hadharani kabisa bila hofu!
Lakini mkae mkijua Yana mwisho,mnakiri mmeua watoto wa malofa!Kama vile ni jambo halali kabisa!
Uzuri mnajua mnaongoza watu wenye chuki na ninyi!Mnaongoza watu wasiowapenda,mmebaki na kikundi Cha wanufaika wachache!
 
Wewe hujui tabia za askari wa Tanzania...

Walipopewa order ya shoot to kill...walifanya mazoezi ya kujifunzia shabaha...

Au nikutumie picha za watu wapo grocery wanakunywa ...Kisha wakapigwa risasi...

Au kwa vile watu wamekaa kimya ? Magomeni mtaa wa Mikumi Polisi waliuwa watu makusudi... Walipogundua Kuna nyumba kama 3, Zina CCTV... Wakaenda kuzitoa kwa nguvu...

Sasa kama watu walikuwa na silaha kwanini waondoe CCTV na mfumo wote ? Si waache ili uwe ushahidi mzuri ..
 
Back
Top Bottom