Sioni ni kwanini askari wasizime vurugu za Oktoba 29, 2025 kwa risasi. Ningewashangaa


Yaani kazi yao ilikuwa ni kuua tu siku hiyo. Mbona hawakukamata mtuhumiwa hata mmoja?
 
Punguza ujuaji, kutuliza vurugu na kuua watu wapi na wapi? Mtaani kwetu hakukuwa na maandamano watu walisusa tu kupiga kura. Lakini polisi walikuja wakapiga shaba za kutosha tena usiku wa manane tukiwa tumelala na watu kadhaa waliuwawa akiwemo mtoto mchanga aliyekufa baada ya risasi kupigwa dirishani. Mbaya zaidi ilikua ijumaa yake yaani siku 3 tokea maandamano ya tarehe 29 kufanyika!! Je kulikua na vurugu gani siku hiyo?

Ni ajabu mtanganyika unashabikia watanganyika wenzako kuuwawa na mzanzibari.
 
Hivi vyombo vya ulinzi na usalama hasahasa polisi na jeshi mkiendelea na trend hii ya kutumia nguvu nyingi na akili kidogo, mtazidi kutengeneza uadui na haohao raia mnaoishi katikati yao. Umeshafikiri madhara yake yatakuwa ni nini🤔
 
Ni aibu sana kutetea mtu anayemnyima raia haki ya kuishi.
 
Punguza ubishi, kule kibaha nina ndugu yangu amepanga, polisi waliingia na kutaka vijana wa kiume watoke nje (wakiwa ndani) wale jamaa wawili walivyotoka nje walikula shaba za vichwa. Hizo picha nikikuonyesha unaweza pata PTSD, alafu unaongea nini hapa? Hakuna aliyekua salama whether upo nje au ndani na tume ilikiri hilo.
 
Wazazi tuambiane ukweli: Kama wewe mzazi hujui kama mwanao amealikwa kwenye vurugu za kuichoma TRA na mwendokasi unaopanda kwenda feri kuchukua samaki wa kuuza mtaani kwako utakuwa hufanyi kazi yako sawasawa. TRA, vituo vya polisi na bank ni maeneo ambayo yanalindwa na askari wenye bunduki, kama mwanao alikubali kwenda kuchoma moto vituo hivyo unamlaumu nani akirudi hana jicho?

Silaha na sare za jeshi vikiibiwa lazima zipatikane hata ikibidi kwa kuuchoma mtaa mzima unaohisiwa kumficha mwizi wa silaha na sare hizo.

Kwanini hushangai watoto wa viongozi wa chadema wote hakuna aliyeuawa kwenye vurugu?
 
Mpango wa kuwamaliza nyumbu , yaani wanapanga mipango ya kijasusi tena Tiktok kabisa , watu walishajipanga ..Wanaowachochea , wamejiandaa wakifa iwe agenda ya kisisa , leo KItima anaongelea waliokufa badala ya maandamano kama mara ya kwanza
 
Hiyo sio kweli, kama ilitokea hivyo hapo ujue kuwa polisi walikuwa na taarifa kamili kuhu hao dogo. Yale magari ya deraya mapya ya polisi yana kamera kali kabisa zinazoweza kuzoom na kutambua sura za watu. Inawezekana walifanya tukio wakakimbilia humo ndani.

Kwani ile mitungi ya gesi waliyoiba wafanya vurugu si waliwapekelea mama zao majumbani? Isivyo bahati na mama zao nao wakaipokea kwa mikono miwili na kuificha mfunguni.
 
Kuna mtoto wa kiongozi wa CCM aliyeuwawa kwenye hizo vurugu?Zaidi mliwapeleka kwenye kambi za jeshi na sehemu salama ili wakati mnatekeleza ile amri ya shoot to kill wasijepitiwa kwa bahati mbaya kama watoto wengine wa malofa ambao mliona ni halali wauwawe!
Endeleeni kuligawa taifa,siku Moja mtalipia kwa udhalimu wenu!
 
Mpango wa kuwamaliza nyumbu , yaani wanapanga mipango ya kijasusi tena Tiktok kabisa , watu walishajipanga ..Wanaowachochea , wamejiandaa wakifa iwe agenda ya kisisa , leo KItima anaongelea waliokufa badala ya maandamano kama mara ya kwanza
Wanalalamikia walikoangukia badala ya walikojikwaa. Kaka ndio maana hata ICC hawaji kwa tukio hili la kipuuzi. Pesa za kugharamia mpango huu nyingine zilitoka kwa mwanachama wa EU mmojawapo. Na huyo ndiye anaefanya lobbing EU kuhusu Tz ikose hiki na kile kutoka EU.
 
Hiyo sio kweli. Polisi wa Tanzania ni watoto na wapya zetu hawahawa tuliowazaa wenyewe na kusoma kwenye shule zetu hizihizi ulizosoma wewe. Hawawezi kuwa makatili kwa ndugu zao watanzania hivihivi tu bila sababu ya msingi. Tatizo hata hao polisi walikuwa wanawindwa wauawe na wengine waliuawa hadharani na mbele ya kamera. Polisi wanapojikuta kwenye hali hiyo lazima wajitetee kwanza kabla ya kutetea wengine (care of the carer). Hata kama ungekuwa wewe lazima ungeitumia silaha yako kwa kazi tatu; kujilinda, kulinda askari wenzio na kulinda raia wema na mali zao.
 
Maandamano yalifanyika terehe 29 tu. Kulikuwa na haja gani siku zilizofuata askari kuingia mitaani na kuanza kupiga watu risasi
 
Ninachotetea sio hicho kabisa, bali natetea askari wachache kabisa wanaotumwa kwenda kutuliza ghasia zinazofanywa na watu waliopora silaha na sare za jeshi waliotawanyika kila mtaa wa kila mkoa. Kumbuka siku ile uchaguzi ulitapakaa nchi nzima kwenye kila mtaa na kitongoji cha nchi hii, na kila kituo cha kupigia kura kuna askari analinda usalama wa wapiga kura na wasimamizi, kura na mali nyingine. Ghafla wakati huohuo unapata habari kuwa vurugu nchi nzima zimezuka, wafanya vurugu wanapora silaha na sare za wanajeshi kwenye vituo vya polisi, wengine wameshika mawe, mapanga, fimbo, viberiti na madumu ya petroli wanachoma kila kitu na kuua kila askari wanaemuona mbele yao. Sasa wewe maandazi unataka hao polisi wachache walioko vituoni watumwe kuzuia ghasia hizo kwa virungu na pingu mikononi. Ushindwe na ulegee!!

Hebu tuache utani hii ni nchi yetu sote, hata hawa askari polisi ni watanzania na watoto wetu pia ambao hawastahili kuuliwa na watanzania wenzao wakati wanatimiza majukumu ya ajira zao. Yaani unataka kumlinda raia asife kwa kumuua askari. Raia kapora silaha na kuvaa sare ya polisi utajua nani ni nani hapo?

Mzazi sema na mwanao ili akitumwa kufanya kitu chochote na yeyote achanganye na akili zake. Mfano, unahitaji kuwa kichaa au mtumia madawa ya kulenya ili Mange Kimambi akushawishi uchome kituo cha polisi au mwendokasi unaoutumia wewe mwenyewe mkazi wa mbagala.
 
Hizi kelele za uwajibikaji si za askari waliokuwa wakituliza ghasia ni za askari walioua pasipo ulazima wa kuua.
 
Sema Uzuri na wewe utakufa Mungu ndo alipanga wafe ivyo Kifo chako kinaweza kua kibaya sana kuzidi hao wa October 29 maisha usidharau watu
 
Sawa endeleeni na kejeli zenu lakini hakuna damu ya tarehe 29 itaenda bure, kuna ndugu, marafiki, majirani waliuwawa tena wengi tu hawakuandamana. So chekeleeni maana utawala ni wenu kwa sasa, ila huko mbeleni (ambako sio mbali sana) kila damu iliyomwagwa itatolewa hesabu!!
 
Risasi inasafiri kaka, ikiikosa target itatua popote na kokote na kwa yeyote anaefuata kwenye uelekeo wa risasi. Kule Gaza walikuwa wanakufa hata watoto wadogo, mama wanaojifungua na wengine wasiohusika na wanajeshi wa hamas. Kule Iran bomu la marekani na Israel lilitua kwenye shule na kuua watoto zaidi ya 200; huko DRC na sudan hivyohivyo risasi zinaua hata wasiohusika. Hapa kwetu ajabu iko wapi kuona watu 2 au 5 wamekufa bila ya kuhusika? Kaka ndiyo maana ICC hawakuja na hawana mpanga wa kuja kwasababu ya mauaji yale. ICC ina uzoefu wa mauji mengi ya makusudi kabisa. Haya mauaji ya kwetu hayakuwa ya makusudi kwa viwango vyao. Ni wahuni waliotaka kuipindua serikali waliowahiwa.
 
Reactions: Tsh
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…