X factor
JF-Expert Member
- Dec 18, 2022
- 1,436
- 2,298
Ikiwa ni kweli wewe 👇
•Umefungua nchi kutoka kwenye ban za kutosha ,umeifanya iaminike kimataifa na Sasa tunakopesheka wakati wowote tunapohitaji,na umedhihirisha Hilo kwa vitendo na Sasa deni la taifa ni T 107.7 na bado ni stahimilivu.
•Umeleta 4R na umezitekeleza Kwa vitendo ukishirikiana na vyombo vyako vya dola na mihimili mingine.
•Umeendeleza Amani uliyoikuta na umeizidisha sana,Kila mtu anakusifu Kwa Hilo.
•Umejenga na kuendeleza miradi mikubwa kama vile SGR,BWAWA LA KUFUA UMEME RUFIJI,DARAJA LA KIGONGO- BUSISI nk
•ATCL inafanya vizuri hatuna shaka na Hilo
• Bandari zetu umezikodisha Ili kuongeza ufanisi na kuongeza mapato,pesa tunaiona unaisimamia ipasavyo.
•Wamasai umetutoa porini ngorongoro,umetupa nyumba nzuri huku msomera na fidia juu,tupate wapi Rais mwenye huruma kama wewe?
•umetumia raslimali za nchi vizuri katika kuboresha maisha ya Kila mtanzania,(afya,Elimu,maji,makazi nk)
• Umeweza ku control mfumuko wa Bei za bidhaa kama vile chakula,mafuta,vifaa vya ujenzi nk,hatukuwahi kupata bei tunazomudu kama hizi
Ikiwa ni kweli, Wewe kama kiongozi mkuu wa nchi pamoja na chama chako chenye wanachama wengi kuliko vyama vingine vyote mmesimamia haya na mengine mengi mazuri ndiyo maana mnasifiwa sana,Tena sifa zenu zinaimbwa kimataifa Sasa.
Lakini wananchi tunaomba mtufanyie takwa letu moja tu nalo ni mabadiliko ya Sheria za uchaguzi, tusiende kwenye uchaguzi mkuu 2025 bila mabadiliko, sikiliza sauti za unaowaongoza.
hili Kwa Sasa siyo takwa la chama Fulani Cha siasa ni Takwa la wananchi wote wenye Nia njema na nchi Yao Tena Kwa faida ya vizazi vyote kuanzia hiki Cha Sasa Hadi vijavyo.
Itaongeza uwazi wa uchaguzi,kuimarisha utawala Bora,kukuza demokrasia na kuondoa malalamiko wakati na baada ya uchaguzi.
Utaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu nzuri kama utaweza kutimiza hili wewe na wasaidizi wako lakini pia utaingia kwenye kumbukumbu mbaya Kwa kushindwa kulifanya hili wakati huu wa utawala wako kwani ndiyo kipindi ambacho reforms zinahitajika sana huwenda kuliko wakati wowote ule,maoni ya wengi yanathibitisha hili.
Huwenda MUNGU anataka kukutumia wewe kulivusha hili taifa kwenye mambo ya hovyo,wizi wa kura na mengineyo yanayochukiza,kwenda kinyume na lengo la muumba ni kujipalia makaa kichwani.
Sioni haja ya wewe kuogopa Uchaguzi huru na wa haki ikiwa umefanya mengi mazuri kama nilivyoeleza hapo juu na mengine sijaandika hapo labda kama una hofu kwamba uliboronga katika hii miaka minne ya moto .
Una mtaji mkubwa sana wa watu (Chawa)wa kutosha wengine hata huwajui Kwa majina, wengine wapo humu JF Wana fake ID na hujawahi hata kuwapa buku ya bando lakini wanaimba sifa zako njema,kwanini uogope uchaguzi huru na wa haki? Binafsi Nina Imani Hawa waimba pambio wanaimba nyimbo za uongo na kukuvusha kilemba Cha ukoka.
Wanaokushauri ukatae kufanya Reforms Kuna kitu kikubwa sana wananufaika kabla hujakaa kwenye hicho kiti na watanufaika huwenda hata baada ya wewe kuondoka hapo,Tena huwenda wewe hunufaiki sana kuwazidi.
Madaraka Yananoga sana lakini lazima yatafikia ukomo na hata upewe kuutawala ulimwengu wote bado unahitaji kuisikiliza sauti ya MUNGU,sauti ya watu ni sauti ya MUNGU lakini wewe usiutafute ukuu sana ambao utakupa hasara ya nafsi yako
Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake? Marko 8:36-37
Fanya reforms Kisha twende kwenye uchaguzi huru na WA haki Ili wananchi wawe na uhakika wa kupata kiongozi waliyemchagua kwenye box la kura na siyo kulazimisha wizi wa kura mnajipalia makaa kichwani nyinyi wenyewe Kwa tamaa ya Madaraka.
Nimetimiza wajibu wangu kama mtanzania mwenye Nia njema na mapenzi kwa nchi yangu
Ova