Sioni umuhimu wa kutafuta au kumiliki hela

Sioni umuhimu wa kutafuta au kumiliki hela

Kwa sababu mahitaji yangu yote nayapata kutoka shambani na ufugaji, sasa hela ya nini?

Nikitaka kula nyama, naingia bandani nachinja kuku au naingia zizini nachinja mbuzi.

Nikitaka unga wa mahindi, nasaga mahindi niliyovuna nakula mwaka mzima.

Nikitaka mchele, nakoboa mpunga niliolima nakula mwaka mzima.

Nikitaka matunda, naingia bustanini navuna.

Sasa hela ina umuhimu gani kwangu, kama kila ninachohitaji ninapata kutoka mashambani, mabandani n.k?

Nilichogundua wale wanaotafuta hela sana, ni wavivu wakulima na kufuga.​
umepigaje apo gentleman?🔥👊
 
Duh mkuu umefikilia tofauti na uhalisia ila nadhani hela haikwepeki, Kuna kutibu mifugo, mazao, ukarabati na matumizi mengine yenye kusaidia
 
Kuna ule msemo "kupanga ni kuchagua", ni wewe unayechagua maisha yako uyaendeshe vipi, wako wengine wanapanga kwenda vaccay, recreational centres ambalo huko zitahitajika pesa nyingi kidogo.. lakini kwako umechagua uliyochagua; uko sahihi sana. Ungekuwa sahihi zaidi kama ungetuambia kiasi gani cha pesa unachokizungumzia wewe. Ukisema tu hauoni haja ya kutafuta pesa kwasababu kila kitu unakipata shambani na bistani kwako wako watakaokuuliza Hilo shamba haujatumia pesa kulihudumia? Huko mashineni hautoi hela? Na kadhalika.. you'd clarify how much money exactly are you talking about.
 
Back
Top Bottom