Hakuna Kitendo Kimenishangaza na Kimeniuma kama kuona Juzi CDF na Chief of Staff wake wakienda Kiunyonge na Kiuhuruma kwa Waziri wa Ulinzi Kujitambulisha.
Kumuweka CDF chini ya waziri wa ulinzi ni kuonesha kuwa mamlaka ni ya Raia na si jeshi, Kuonesha Jeshi ni chombo kinachotumika na Raia kwa maslahi yao. Jambo ambalo ni sawa kabisa, Serikali zote za kiraia zinafanya hivi.
Hii ni nchi yenye serikali inayoendeshwa kiraia, kwa maana wananchi ndiyo wenye mamlaka. Mamlaka yao yanawakilishwa na Rais aliyechaguliwa kwa ‘popular vote’.
Waziri wa Ulinzi anateuliwa na Rais (aliyechaguliwa na wananchi) kutoka Bungeni. Huko Bungeni amechaguliwa na wananchi au kuteuliwa na Rais.
Sijawahi kuona popote pale Waziri wa Ulinzi anakuwa Juu ya Jeshi tena Kiprotokali wakati Jeshi ni Serikali Kificho ya Kimedani na inayojitegemea na ambayo ikiamua muda wowote ule ichukue hatamu ya nchi inaweza na huyo ( huyu ) Waziri wa Ulinzi anakuwa si lolote wala si chochote.
Siyo kweli, USA, INDIA na URUSI nimetaja kwa uchache Wizara za Ulinzi ziko juu ya jeshi, kwa maana Jeshi hupokea maelekezo toka wizarani.
Kweli jeshi likitaka shika hatamu linaweza fanya hivyo mifano ni mingi.
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, Hayati Mkapa na kidogo Mzee Kikwete waliwaheshimu mno CDF's wa Vipindi vyao na walihakikisha hawalazimishi Jeshi kuwa ni sehemu ya Siasa na Utawala wa Kiserikali.
Siyo kweli, kwa Tanzania Jeshi limekuwa ni sehemu ya siasa na Utawala kwa kipindi cha Mwalimu, na Jeshi limeendelea kuwa sehemu ya Utawala kwa marais wote waliofuata.
Wakati wa Mwalimu, Ofisi za TANU zilipatikana mpaka kambini! Jeshi lilihimiza kudumu kwa fikra za mwenyekiti kila walipokusanyika.
Wakati wa Mwalimu na marais wengine bado watu kutoka jeshini wanapewa nafasi katika serikali, wanateuliwa kuwa Wakuu wa wilaya, Mikoa na wengine mabalozi.
Hii ina faida sana ktk kuboresha uhusiano wa Jeshi na Serikali na inatajwa kuwa moja ya mbinu inayozuia mapinduzi ndani ya Tanzania.
Mifano:
Balozi wa TZ nchini SA🇿🇦- Meja Gaudence Milanzi (mstaafu)
Aliyekuwa mwaka jana Balozi wa TZ nchini Misri 🇪🇬- Meja Anselm Shigongo (mstaafu)
Mkuu wa mkoa wa Kagera- Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti
Kama kuna Kitu kimenishangaza na naona HATARI fulani mbeleni huko ni kuona Awamu hii ya Rais Samia huyu Waziri wa Ulinzi Bi. Stegormena Tax akipewa Madaraka makubwa juu ya Jeshi na CDF wake kitu ambacho si Kizuri na siyo cha Kiutaratibu kabisa.
CDF ni lazima awe chini ya kiongozi wa kiraia. JESHI NI CHOMBO CHA WANANCHI, SI ‘PARALLEL GOVERNMENT’, hatuwezi kuwa na Dola ndani ya Dola.
JESHI linawajibu kwa Raia-wanaowakilishwa na Rais-anayemteua Waziri wa Ulinzi- anayetoka Bungeni!!
Na Mkurugenzi Mkuu wa TISS anawajibika moja kwa moja kwa Waziri wa Ulinzi.
Kwa Kawaida ilitakiwa baada ya CDF Kuteuliwa basi Kiitifaki Waziri wa Ulinzi ndiyo alipaswa kwenda kwa CDF ila siyo CDF na Chief of Staff kwenda kwa Waziri wa Ulinzi huku wakiwa na Nyuso za Huruma kana kwamba Wameamrishwa na Mtu wakati Wao ndiyo wana Mandate ya Kuamrisha.
Hiki kikitokea jua wazi tunapoteza serikali ya Kiraia. Jeshi litashika hatamu ktk ‘scenario’ mbili tu.
1. Wakati wa dharura (State of Emergency)
2. Wakipindua serikali, hii ni kinyume na katiba.