haya ndio matatizo ambayo wanaume tunayaepuka "kushirikiana na mwanamke kwenye mipango"kinacho takiwa mwanaume Jenga nyumba yako ndio mwambie mkeo au michepuko ahamie. hapo hawezi kuleta kiburi kwasababu hajui hata garama ulizo tumia kujenga zaidi yayeye kukaatu tena kwaadabu zote. akiweza kufanya hivyo vibiashara vya kununulia poda nachipsi afanyetu hakuna shida.au Kama amesoma nayeye fresh mshara wake atajua kwakuupeleka
Dada yangu alipata mume wa design yako, ameishi nae miaka 9 kwenye ndoa walijenga nyumba na mwanaume akaandika majina yake na akaishia kumfukuza dada alirudi nyumbani kuanza upya.
Kwakuwa mwanamke hatakiwi kuwa na sauti dada yangu aliolewa alipotoka form six so kweli hakuwa na kazi wala future. Mume alikua ana mnyanyasa kama mnyama. Anampiga mbele ya watoto kisa dada ameenda kanisani. Anamwambia we umekuja na nini hapa takataka huna mbele wala nyuma. Unajifanya unaenda kusali jumapili kumbe huna lolote.
Awamu ya pili dada alipigwa kisa amechelewa kuanua nguo za mumewe mvua ikanyesha akamwambia wewe unajua hata bei ya hii suruali. Kwenu mnayo? Alimpiga dada akazimia akapelekwa hospitali.
Gharama za hospitali mume akamwambia sina hela waambie ndugu zako. ni nesi ndo akamsaidia akapona. Kuna Binamu yetu Akamwambia kwanini usirudi chuo kusoma upate na kazi siku nyingine ukipigwa uwe hata na ela ya kujihudumia. Ni kauli kali ila ina ujumbe.
Dada akamuomba mumewe akasome chuo mume akamwambia baki hapa lea watoto mimi sina uwezo wa kuweka housegirl. Kumbuka dada ndo alikua mkubwa na nyumbani walikua wanamtegemea, sisi tulikua primary kipindi hicho. Mama aliumwa hadi anakuja kupona alichangiwa na majirani maana ndugu zake walishafariki. Msaada aliokua anautegemea ni dada ambae alimsomesha kwa shida sana.
Kufupisha story, mume ilifika hatua akamwambia dada amechoka kukaa na mzigo hivyo aondoke. dada akarudi nyumbani akapata ufadhili kanisani akasomea unesi. Miaka miwili. Akapata kazi kwenye hospitali ya kanisa. Mume alivoskia mkewe kapata kazi akaenda kwa mama akamwambia mke wangu sikuachana nae kwa talaka nataka turudiane.
Dada na upole wake akakubali. Wamekaa baada ya mwaka mwanaume anamwambia acha kazi ntakulea na watoto. Dada akasema mama na wadogo zangu wananitegemea mwanaume akaanza kumpiga tena anasema kwanini anamdharau au kisa amepata kazi. Na wakati hajarudiana na mumewe dada akawa ameshaanza msingi wa nyumba ya vyumba viwili kijijini huko. Mwanaume kuskia hivyo akasema kwanini hakumshirikisha. Akamwambia bora waweke nguvu wajenge wote mjini. Dada akakubali maana angekataa ni vipigo tena.
Nyumba ya mjini ilivyoisha mwanaume akaandika tena majina yake na safari hii akaoa na mke wa pili. Akamwambia dada kama huwezi kukaa hapa ondoka urudi kwenu au kubali kuwa na mke mwenzio. Manyanyaso yalizidi yani story ni ndefu. Ila mimi hakuna mwanaume atakae niambia eti mwanamke akae tu nyumbani amuhudumie nikaelewa. Nyinyi mnaukatili mkubwa sana mwanamke asipokua na chochote. Hivi nnavyokwambia dada amerudi kijijini. Ilibidi aanze upya. Hadi sisi tunakuja kupata kazi na kuanza kumshika mkono keshachakaa na hiyo ndoa na mateso.
Wanaume nyinyi mnaoteteana sijui mwanamke usimshirikishe nyinyi ndo wabinasfi wakubwa mnafanya hivyo ili muweze kuwa control wakina mama.