Sipendi na sitaki ukaribu wala shobo na wanawake wenye vijitabia vya feminism

Sipendi na sitaki ukaribu wala shobo na wanawake wenye vijitabia vya feminism

Sawa sasa kama hapo nani kaharibu? Muda umepata mke anaenyenyekea obviously utampelekesha unavyotaka. Na akili ya kuomba talaka huwa haipo anaamini ndoa ni uvumilivu kwasababu akijitetea tayari anaitwa feminist. Nyumba amejenga na dada yangu mbona dada alimwachia akaondoka. Hadi leo anaishi na huyo mwanamke wake. So nguvu ya dada yangu yote ilipotea. Na dada angesema ajenge Kivyake bado angeitwa feminist hamshirikishi mmewe, amejenga nae amemdhulumu. Mnaona ubinafsi wenu ulipo? Bora mwanamke ajipambanie tu.
mbona huyo anaeishi nae hajamfukuza? au dadaako ndio alikua nashida? kamadadako alitoa jasho yake kwenye kujenga nyumba angefata sheria hio nyumba wangegawana. ndio Mana mwanaume anae jielewa hamruhusu mkewe apeleke hata chakula kwamafundi ujenzi ukiwa unaendelea kwasababu mkigombana akaenda kusema mahakamani kua alishiriki kuwapa chakula mafundi wakati waujenzi anapata hakiyake hionyumba itauzwa wagawane au mwanaume amjengee mwanamke yakwake ndio waachane
 
Tunarudi kule kule. Mnawatupia lawama wanawake always kwamba labda yeye ndo chanzo. So solution alotumia mwanaume mwenzenu kumpeleka mchepuko hapo ndo sawa? Inamaana siku mwanaume ataamua tu amfukuze mkewe amuweke mchepuko. Na hali hiyo amejenga nae.

Ukiwakuta hawa ambao hawataki mwanamke afanye kazi. Anaamka siku kashikwa na mchepuko anamfukuza mkewe ataenda wapi?
Akili za hichi kichwa zinawaza mwanaume ndio atatangulia kufa...

Na urithi tu [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Brainless akiwemo mama yako mzazi au?
Simulizi za kutunga ni nyingi sana jf kama una muda unaweza kupita pita na kufurahia vipaji kuntu vya utungaji wa riwaya. Unasoma simulizi na unaona ni porojo la kutunza A to Z.

Zamani jf ilikua home of thinkers siku hizi imekua saluni ya mama Kimbo yote shukrani kwa the brainless gender.
 
Afanye anachotaka. Alokwambia kuna mwanaume hana mchepuko nani? Ila wenzenu wanafanya kwa akili hawanyanyasi wake zao. We niite majina yote ila upumbavu wa kusema eti mume atanihudumia kila kitu ni NO! Wewe unaesema umejengea wake zako kama ni kweli hata, kuna wenzio uwezo wa kujenga tu hana ila hataki mwanamke afanye kazi kwasababu anaogopa atampanda kichwani.

Na unaposema siku ananiongezea mwenzangu, dini yetu hairuhusu kuoa wake wawili. Huko nje hata awe nao mia sisi tushajiwekea mikakati ya maendeleo. Yeye anasimamia hiki mimi kile. Mahesabu jioni tunafanya maendeleo. mi sikusomeshwa na wazazi wangu eti nije kuwa golikipa. Kwanza mume wangu alishasema tangu zamani hataki mwanamke asiejituma, na wanaume siku hizi hawaoi magolikipa labda nyie wenye inferiority complex mnataka mvimbe mda wote

Jeuri iendane na kipato. Muachishe mkeo kazi huku una uwezo wa kumuhudumia.
kwani nimekuambia hawafanyi kazi? kazi wanafanya lakini siwezi kukaanao chini nianze kuwauliza wameingiza kiasi gani tupange mipango hio siwezi helazao wanunue mahitaji yao wanayo mudu mengine nafanya mwenyewe.
 
mbona huyo anaeishi nae hajamfukuza? au dadaako ndio alikua nashida? kamadadako alitoa jasho yake kwenye kujenga nyumba angefata sheria hio nyumba wangegawana. ndio Mana mwanaume anae jielewa hamruhusu mkewe apeleke hata chakula kwamafundi ujenzi ukiwa unaendelea kwasababu mkigombana akaenda kusema mahakamani kua alishiriki kuwapa chakula mafundi wakati waujenzi anapata hakiyake hionyumba itauzwa wagawane au mwanaume amjengee mwanamke yakwake ndio waachane
Mbona hueleweki sasa. Mara hamtaki wanawake wa kugawana nao mali. Mara akadai haki yake. So which is which? kama kaishi na dada yangu miaka yote hiyo na manyanyaso. Huyo anaekaa nae tutajuaje? So dada yangu ana matatizo ila kwenye kupokonywa nyumba mwanaume ndo mwamba au sio. Ila wanaume shkamoo. Nyie viumbe mmetisha
 
kwani nimekuambia hawafanyi kazi? kazi wanafanya lakini siwezi kukaanao chini nianze kuwauliza wameingiza kiasi gani tupange mipango hio siwezi helazao wanunue mahitaji yao wanayo mudu mengine nafanya mwenyewe.
Hivi umepitia thread za wanaume wenzio humu? Wanasema hawataki mwanamke anaefanya kazi maana hiyo ndo feminism ya 50/50 wanayoisema wao. Kwamba kwanini mwanamke usikae nyumbani. sijui kama mko kwenye page moja au vipi. Hawataki kwasababu wanaogopa wataanza ujeuri. Sasa mwanamke anaefanya kazi anapata milioni tatu kwa mwezi hutaki akusaidie maendeleo wala hutaki kujua hela yake inaenda wapi. Sawa, basi anaamua kujenga vitega uchumi hata viwasaidie baadae bado mtaibuka kusema hawashirikishi. Nlichogundua hamjajua mnachokitaka.
 
Akili za hichi kichwa zinawaza mwanaume ndio atatangulia kufa...

Na urithi tu [emoji16][emoji16][emoji16]
Nimeandika neno kufa hapo au unawashwa? Humu jf kuna waume sampuli ngapi mbona naanza kupata wasiwasi
 
Mimi nimeoa wake wawili nimewajengea kilamtu sehemu yake wanakula vizuri nawanalala pazuri namichepuko ninayo. sasa huyo mumeo sijui Kama anahata huyo mchepuko nasiku akikuambia anataka akuongezee mwenzio nahisi ndio mwisho wandoa yenu kutokana nawewe kua mjuaji sana Bibi 50kwa50.ualabda jama avumilietu afe natai shingoni. raha yamwanaume nikufanya anacho taka sio kupangiwa pangiwa hasa ukiwa nakipato chako
Wanawake wenye akili timamu mnawaita wajuaji ila hayo maboga mnayoyanyanyasa na kuyapiga ndani ndo mnayoyataka. Mnataka wanawake wa kuwageuza mnavyotaka. Wapo mtawapata ila mkikutana na wanaojitambua msiwe mnaishia kuogopa. Jikazeni tu
 
akidai talaka si ndo mnasema role model ni joyce kiria. Mwanamke anatakiwa avumilie. Huyo dada saizi akipata mume mwengine akamwambia acha kujenga njoo tujenge wote unadhani atarudia tena? Nyie
Mbona hueleweki sasa. Mara hamtaki wanawake wa kugawana nao mali. Mara akadai haki yake. So which is which? kama kaishi na dada yangu miaka yote hiyo na manyanyaso. Huyo anaekaa nae tutajuaje? So dada yangu ana matatizo ila kwenye kupokonywa nyumba mwanaume ndo mwamba au sio. Ila wanaume shkamoo. Nyie viumbe mmetisha
Zwanaume mnajiongelea kwa upande wenu. Ila sisi wanawake tunajifunza kutokana na makosa ya wenzetu. Mbona kaondoka kaacha nyumba yake? Kamsumbua nani?
[/QUOTE
Hivi umepitia thread za wanaume wenzio humu? Wanasema hawataki mwanamke anaefanya kazi maana hiyo ndo feminism ya 50/50 wanayoisema wao. Kwamba kwanini mwanamke usikae nyumbani. sijui kama mko kwenye page moja au vipi. Hawataki kwasababu wanaogopa wataanza ujeuri. Sasa mwanamke anaefanya kazi anapata milioni tatu kwa mwezi hutaki akusaidie maendeleo wala hutaki kujua hela yake inaenda wapi. Sawa, basi anaamua kujenga vitega uchumi hata viwasaidie baadae bado mtaibuka kusema hawashirikishi. Nlichogundua hamjajua mnachokitaka.
wee mbona unaongelea maendeleo sana namambo mengine unayaruka. wanaume hatutaki kufatiliwa kila muda Sasa wewe ukitoka kazini unanamfata mumeo muongozane nyumbani kwani nyie mapacha? akitaka kuchepuka atachepukaje naujuaji wako huo siutamfumania Kira mala nandoa ife kifo chamende. mwanamke kwake nyumbani
 
Sasa kaka Fusebox mbona umeikwepa tena mada nliyoiweka. Umeparamia mada ya kufatiliana sijui. Yani mi niwe nasimamia miradi kwengine na ye kwengine ntamfatilia saa ngapi?
Anapofanya kazi na nnapofanya kazi ni tofauti. Anasafiri sana na ye ndo anakazi ya kunilalaMikia kwanini simu zake zikiita huwa sipokei. Nilishajiapiza stress za simu sitaki.

Nyie kubalini mnaishi kikoloni of which kama wake zenu wameridhia hewala. Mume wangu ndo ameamua hizi terms. Si mnaweza kuona design ya wanaume waliopo. Kuna nyie af kuna wanaojielewa. Usawa huu wa kutamani mtoto apate elimu nzuri ada kwa mwaka milioni tano. Muwe na watoto watatu. Yote hiyo anaitafuta mtu mmoja. Bado miradi ya maendeleo. Bado yeye kusaidia kwao. Si atapata stress za kufa mtu.

Sisi tumelenga kuwa na maisha ya aina flani ndo maana tunajishughulisha hata watoto wetu wako inspired. Sasa sijui kwanini mnalazimisha kila mwanamke awe zamwamwa
 
Wanawake wenye akili timamu mnawaita wajuaji ila hayo maboga mnayoyanyanyasa na kuyapiga ndani ndo mnayoyataka. Mnataka wanawake wa kuwageuza mnavyotaka. Wapo mtawapata ila mkikutana na wanaojitambua msiwe mnaishia kuogopa. Jikazeni tu
Nisha kwambia zama hizi ukiona mwanaume anampiga mwanamke ujue hanaakili. sasahivi wanaume tunaishi kwasheria ukiona mwanamke haendani nasheria zako unaacha unaoa mwingine. watuwenyewe mshakua wajuaji mtu ukimpiga ngumi moja tayari ashaenda kukushtaki unaacha kazi zako unafatilia kesi isio nakichwa Wala miguu.
 
Dada yangu alipata mume wa design yako, ameishi nae miaka 9 kwenye ndoa walijenga nyumba na mwanaume akaandika majina yake na akaishia kumfukuza dada alirudi nyumbani kuanza upya.

Kwakuwa mwanamke hatakiwi kuwa na sauti dada yangu aliolewa alipotoka form six so kweli hakuwa na kazi wala future. Mume alikua ana mnyanyasa kama mnyama. Anampiga mbele ya watoto kisa dada ameenda kanisani. Anamwambia we umekuja na nini hapa takataka huna mbele wala nyuma. Unajifanya unaenda kusali jumapili kumbe huna lolote.

Awamu ya pili dada alipigwa kisa amechelewa kuanua nguo za mumewe mvua ikanyesha akamwambia wewe unajua hata bei ya hii suruali. Kwenu mnayo? Alimpiga dada akazimia akapelekwa hospitali.

Gharama za hospitali mume akamwambia sina hela waambie ndugu zako. ni nesi ndo akamsaidia akapona. Kuna Binamu yetu Akamwambia kwanini usirudi chuo kusoma upate na kazi siku nyingine ukipigwa uwe hata na ela ya kujihudumia. Ni kauli kali ila ina ujumbe.

Dada akamuomba mumewe akasome chuo mume akamwambia baki hapa lea watoto mimi sina uwezo wa kuweka housegirl. Kumbuka dada ndo alikua mkubwa na nyumbani walikua wanamtegemea, sisi tulikua primary kipindi hicho. Mama aliumwa hadi anakuja kupona alichangiwa na majirani maana ndugu zake walishafariki. Msaada aliokua anautegemea ni dada ambae alimsomesha kwa shida sana.

Kufupisha story, mume ilifika hatua akamwambia dada amechoka kukaa na mzigo hivyo aondoke. dada akarudi nyumbani akapata ufadhili kanisani akasomea unesi. Miaka miwili. Akapata kazi kwenye hospitali ya kanisa. Mume alivoskia mkewe kapata kazi akaenda kwa mama akamwambia mke wangu sikuachana nae kwa talaka nataka turudiane.

Dada na upole wake akakubali. Wamekaa baada ya mwaka mwanaume anamwambia acha kazi ntakulea na watoto. Dada akasema mama na wadogo zangu wananitegemea mwanaume akaanza kumpiga tena anasema kwanini anamdharau au kisa amepata kazi. Na wakati hajarudiana na mumewe dada akawa ameshaanza msingi wa nyumba ya vyumba viwili kijijini huko. Mwanaume kuskia hivyo akasema kwanini hakumshirikisha. Akamwambia bora waweke nguvu wajenge wote mjini. Dada akakubali maana angekataa ni vipigo tena.

Nyumba ya mjini ilivyoisha mwanaume akaandika tena majina yake na safari hii akaoa na mke wa pili. Akamwambia dada kama huwezi kukaa hapa ondoka urudi kwenu au kubali kuwa na mke mwenzio. Manyanyaso yalizidi yani story ni ndefu. Ila mimi hakuna mwanaume atakae niambia eti mwanamke akae tu nyumbani amuhudumie nikaelewa. Nyinyi mnaukatili mkubwa sana mwanamke asipokua na chochote. Hivi nnavyokwambia dada amerudi kijijini. Ilibidi aanze upya. Hadi sisi tunakuja kupata kazi na kuanza kumshika mkono keshachakaa na hiyo ndoa na mateso.

Wanaume nyinyi mnaoteteana sijui mwanamke usimshirikishe nyinyi ndo wabinasfi wakubwa mnafanya hivyo ili muweze kuwa control wakina mama.
Hii movie inaitwaje
 
wee mbona unaongelea maendeleo sana namambo mengine unayaruka. wanaume hatutaki kufatiliwa kila muda Sasa wewe ukitoka kazini unanamfata mumeo muongozane nyumbani kwani nyie mapacha? akitaka kuchepuka atachepukaje naujuaji wako huo siutamfumania Kira mala nandoa ife kifo chamende. mwanamke kwake nyumbani

Sasa kaka Fusebox mbona umeikwepa tena mada nliyoiweka. Umeparamia mada ya kufatiliana sijui. Yani mi niwe nasimamia miradi kwengine na ye kwengine ntamfatilia saa ngapi?
Anapofanya kazi na nnapofanya kazi ni tofauti. Anasafiri sana na ye ndo anakazi ya kunilalaMikia kwanini simu zake zikiita huwa sipokei. Nilishajiapiza stress za simu sitaki.

Nyie kubalini mnaishi kikoloni of which kama wake zenu wameridhia hewala. Mume wangu ndo ameamua hizi terms. Si mnaweza kuona design ya wanaume waliopo. Kuna nyie af kuna wanaojielewa. Usawa huu wa kutamani mtoto apate elimu nzuri ada kwa mwaka milioni tano. Muwe na watoto watatu. Yote hiyo anaitafuta mtu mmoja. Bado miradi ya maendeleo. Bado yeye kusaidia kwao. Si atapata stress za kufa mtu.

Sisi tumelenga kuwa na maisha ya aina flani ndo maana tunajishughulisha hata watoto wetu wako inspired. Sasa sijui kwanini mnalazimisha kila mwanamke awe zamwamwa
hahaha haya umeshinda. ila sijajua mumeo ana akili na msimamo kiasi gani Hadi akaweza kuamua kuishi nawewe Mana sizani Kama anaweza kukudanganya kitu ukakubali bila kumhoji(kwasababu sisi tunapenda kudanganya wanawake) sijajua anaishi nawewe vipi.atakua Hana mambo mengi Kama sisi
 
Simulizi za kutunga ni nyingi sana jf kama una muda unaweza kupita pita na kufurahia vipaji kuntu vya utungaji wa riwaya. Unasoma simulizi na unaona ni porojo la kutunga A to Z.

Zamani jf ilikua home of thinkers siku hizi imekua saluni ya mama Kimbo yote shukrani kwa the brainless gender.
Mwanaume unapata mda wa kuangalia mama kimbo. Mimi tu siifatilii. Ndo naanza kuelewa tabia zenu. Hizi fake IDs zinawafanya mjione miamba kumbe chenga
 
Akili za maskini wa fikra utazijua tu. Ukija kupata mtoto wa kike akaolewa kisha siku unaletewa yupo kwenye jeneza kisa mmewe kampiga ndo utaelewa. Akiwa wa mwengine wala haiumi ila akiwa wa kwako ndo mishipa huwa inawasimama
sipendi kuona mwanamke ana nyanyaswa kwasababu namimi nina dadazangu nao wameolewa pia wameajiriwa. ila kilamara nawaambiaga kazizao zisilete kiburi kwawaume zao wataachwa nastara yamwanamke nindoa tu.
 
Back
Top Bottom