Sipendi ugali kabisa na ninaishi

Sipendi ugali kabisa na ninaishi

Hata hivyo Ugali umedumaza sana Ubongo za watu wengi na jinsi ulivyo wengi wanaamini ni chakula ya Mtu mweusi kumbe nayo ilililetwa na Mabeberu zipo Nchi nyingi Afrika Ugali sio kipaumbele chao kama hapa kwetu...
Unakuta watu wanadanganyana eti ugali una nguvu😂😂 mafundi ujenzi wanaenda kula ugali dagaa wakiona unakula wali wanashangaa kumbe Ni umasikini wao ..wanasema chips hazina nguvu kumbe Wana compare ugali wa buku na chips za buku hawajui kwamba chips Ni gharama ili upate zenye uzito sawa na ugali wa buku jero inabidi u pay more around 4k ..na pesa hawana wanakazania kusema ugali una nguvu😂😂
 
Aah! basi watu tunatofautiana sana

Kiukweli Mimi nisipokuta ugali(nguna) nyumbani siwaelewi kbs, wapike vyakula vyao wanavyotaka lkn ugali wa baba huo lzm uwepo.

Ugali dagaa, ugali samaki, ugali nyama choma hapo hunitoi mzee. Nakula hata mwaka mzima bila kubadili na sioni noma yoyote.
Na unaonekana kweli hamnazo
 
Hata sisi tulao Ugali tunawashangaa ninyi mnaopitisha siku zaidi ya mbili bila kula ugali. Eti zipite siku 2 huku nikila sijui ndizi, sijui wali n.k haiwezi tokea labda niwe sina mbadala.
 
Wali nikiula siku mbili mfulululizo huwa nakinai .

Vyakula vya ngano nikivila huwa vinanikereketa na kusababisha kutibuka kwa tumbo.

Ugali sijawahi kuukinai kiasi kwamba hata kipindi cha ramadhan namwambia wife anipikie ugali kama futari au daku.
 
Kitambi chako kinaendeleaje?
Ugali fulani hv laini, nyama choma nusu kilo, pilipili nyingi sana mixer ndimu, maji ya kunywa lita moja ya baridi. Baada ya hapo nikianza kufungua vizibo sasa naweza nikakata kreti la Kilimanjaro lager aisee.
 
Ugali wa mahindi mswahili yeyote ukisema ugali anajua wa mahindi...ngano na mtama Nchi nyingi wanalima na kutumia hizo nafaka hata kichwani wapo sawa tofauti na wala ugali harafu wanauamini balaa huwezi kuwaambia kitu kwa sababu washadumazwa...
Wewe kama ulizaliwa kilaza utaendelea kuwa kilaza tu sio kwasababu ya kula ugali. Mahindi kihistoria yalilimwa hata katika dola ya misri enzi za nabii yusuf mtoto wa Yakobo.
 
Semeni hampendi kula Mahindi na sio ugali naona wengi mnatumia neno Ugali tofauti na inavyotakiwa.

1.Ukutwanga ndizi,ukapata unga wake unaweza kutengeneza ugali
2.Ukisaga Mchele unaweza kutumia kupija ugali,
3.Ukitwanga au kusaga mtama/ulezi/unaweza kuutumia kuyengeneza ugali
4.ukisaga uele mhogo unaweza kupata unga ukaautumia kupata ugali.
5.Kuna jamii pia zinatumia ngano kutengeneza ugali
Hivyo vyakula vyote vinaweza kukupa unga na ukapata uji mzito au ugali.

Issue hapo ni kutumia mahindi na sio neno ugali.
 
Katika vyakula ambavyo huwa sivishobokei ni Ugali mimi siupendi kabisa yaani sina stim nao kabisa.

Sazingine huwa nakula tu ndo wife au beki3 kaandaa lakini kiukweli ugali sio chakula nachokipa thamani japo familia yangu mke na watoto wanaupenda balaa.

Ni mara kibao nikirudi nyumbani nikikuta wamepika ugali nitapitiliza tu chumbani kulala au nitaomba wanitafutie mbadala.

Na mara nyingi wakiwa wanaandaa huwa wanajua kabisa kwahiyo mbadala lazima iwepo.

Sazingine huwa nakula tu ili siku ipite lakini ni chakula cha hovyo kabisa, mimi naweza kukaa hata mwaka nisile ugali na nikaona fresh kabisa.

Ni kawaida kwangu siku hizi kukaa wiki au wiki mbili bila kuutia ugali mdomoni.

Kuna kitu huwa kinanishangaza sana, kuna watu wanakula ugali mchana na usiku tena siku 7 za wiki duuuh tena ugali na yale madagaa ya ziwa victoria!! Sio kwa nia mbaya au nina ego hapana mimi ugali hapana bora nile ndizi mwezi nzima lakini sio ugali.
Mtu na akili zako timamu unaanzaje kula ugali?
 
Back
Top Bottom