Shadeeya
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 49,759
- 118,798
Mmmh. Huyo kazidi sasa.Unakuta mpenzi wako anakuja nyumbani kukusalimia kabeba pochi utadhani kakubebea zawadi ,kumbe kajaza hayo ma make up tu ,na akifika tu mbio kwenye dressing table
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mmmh. Huyo kazidi sasa.Unakuta mpenzi wako anakuja nyumbani kukusalimia kabeba pochi utadhani kakubebea zawadi ,kumbe kajaza hayo ma make up tu ,na akifika tu mbio kwenye dressing table
[emoji23][emoji23][emoji23]cole acha kunijazaMake up zako za ki asili ndiyo zinanipagawisha
Mwanamke huyo bhana.Hapo kuna mwanaume na mwanamke
Ndo mlivo kweliMmmh. Huyo kazidi sasa.
Kwani Mkuu na wewe unatumiaga hizo mamboMmmh. Huyo kazidi sasa.
Umeonaeeee. Sema na wewe mwaya.[emoji23][emoji23][emoji23]
Tena hawa wanaosema hawawapendi wanawake wanaojipaka make up utakuta wake zao wana kila aina ya make up kwenye dressing table,wakija hapa kazi tukusimanga tu.
Tuma picha yako original nikuone[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kweli mkuu,wengine hatuna ujasiri wa kutoka bila hiyo kitu kwakweli
Hiyo inaitwa nguvu ya make upMwanamke huyo bhana.
Sasa umeamini wengine hatuna ujasiri wa kutembea bila make up?
Duuu hii hatari sasa. Kumbe kuna kuuziana mbuzi kwenye guniaAcheni kutusimanga[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]]View attachment 867785
Mmh. Kwa nini tusije Kaka? 😂😂Wnawake sidhani kama watakuja hapa aiseeeee
Unafanya matangazo au.km hufanyi matangazo.(KAMA UMEOLEWA/UMEOA TAFADHALI USISOME)
Kuna story za kutisha nyingi sana kutoka kwa wanaume, kuhusu kuamka asubuhi na kujikuta wakiwa wamelala kitandani pembeni ya viumbe wasio watambua baada ya kutoa MAKE UP usoni usiku.
Wanawake wengine hutumia pesa nyingi kila mwezi kununua make-up, na sababu kuu ya kutumia make-up kuzidi mipaka ni kutokujiamini kwa jinsi walivyo, hasa uzuri wao sehemu za usoni.
Wanawake ni kama bidhaa. Pindi bidhaa zikiwa sokoni, hua kuna na ushindani mkubwa wa biashara nzuri nzuri kuuzika. Na mtu yoyote aliekua mfanyabiashara atakwambia kua ni "lazima bidhaa kila siku kuifanya yenye mvuto sokoni" ili ipate wanunuzi.
Haina tofauti na wanawake kwa make-up. Ni lazima waongeze uzuri katika muonekano wao ili wavutie, hususan muonekano wa sura, kwasababu ya kumvutia mlengwa maana ndio kitu cha mwanzo hutazama (japo wengine huangalia mizigo).
View attachment 867654
Muonekano wa sura mitaani na sehemu za starehe huongopa, tumeshasikia story nyingi za kutisha kutoka kwa wanaume kuhusiana na kuamka asubuhi na kujikuta pembeni ya kitanda kuna mdada amelala asiemtambua. Najua inatisha kama imeshakukuta.
Mfano wa hizo story:
Kuna jamaa dalali wa magari siku moja alikua Club moja hivi, aliwaona wadada wakiwa wamependeza sana. Baada ya usiku wa furaha tele alimuimbisha dada mmoja na wakawa wanapeleka vyombo (tungi, nyagi, bia) pamoja mpaka wakazima. Alipo amka asubuhi, alichokiona pembeni yake kilikua ni cha kutisha. Ilibidi awapigie sim rafiki zake kuwauliza kama aliondoka na mtu sahihi ama laa.
Mwingine alikutana na dada mmoja mrembo maeneo ya beach, akashusha mistari mpaka dada akaingia kilaini, kisha akamuomba waende kuogelea. Walipo zama baharini, na kisha dada kuchomoka, aliona dada kabadilika rangi (rangi imefifia), kope na nyusi hana, mpaka jamaa akashtuka ni kipi kimemsibu yule dada.
Jamaa mwingine alimuona dada mrembo na kuamua kuongea nae, ilikua mwisho wa mwezi, na alikua anataka kujifyatua kidogo ili mwezi uishe viziri kwake, dada alikubali na wakaamua kwenda hotel. Walipofika chumbani dada aliomba taa izimwe na atoe make-up ili alale kwa amani, jamaa aliridhia. Dada aliingia chooni atoe make-up yake, cha ajabu alitumia muda mrefu sana mpaka jamaa akawa na wasiwasi, aliamua kumfuata na kujua kipi kinaendelea kwa ule ukimya. Alichokutana nacho kilimshtua sana, sura alioikuta haikua ile ya yule dada alieongea nae mwanzo, na hata ile shepu iliomvutia haikuwepo. Alijikuta amepiga kelele kubwa, yule dada alishtuka na kuamua kujifungia kule bafuni. Jamaa akasepa bila kuaga!!!
Mfano wa hayo matukio, ni haya
View attachment 867655
View attachment 867656
View attachment 867657
View attachment 867658
View attachment 867659
Sipingi kua make-up ni muhimu. Huwapa kujiamini kisaikolojia, kuonekana mzuri ni kujihisi mzuri. Ila iwe na mipaka jamani, mungu anawaona!!! Mtatutoa roho zetu ipo sikuView attachment 867660
Umeonaeee. Wengi wanakosea hapo na ndio sababu unakuta Mbagala rangi tatu zinakuwa nyingi sababu kuu ni hiyo.mm nadhan wanawake weng tunakosea rang za makeup!mtu unanunua makeup unafananisha na nguzi ya uso !aku mm hua nafananisha na sehem zingn za ngoz !mfano mikonoo!hata ukipaka hubadiriki unashine tu! msituchoshe
Kumbe ndio ipo hivyo, wengine wananunua tuMie naona waendage kwenye maduka makubwa ya Cosmetics huwa wanashauri kabisa kwamba makeup namba fulani ndio rangi ya ngozi yako. Ziko bei juu ila ni nzuri na haziondoi uhalisia wa mtu.