Sipingi kuwa make-up ni muhimu ila iwe na mipaka jamani

Wanawake tumeumbwa kupendeza.
Japo muda mwingine make-up inasitiri ila ikizidi kero.

Mie nisiwe mnafiki, napaka ila kwa kiasi.
Na inategemea naenda mahala gani.
Kama harusini napaka mpaka utanisahau, ila kama sehemu za starehe napala kwa kiasi nisije mkimbiza bwana mpya asubuhi.
Hahahhahaha
 
Umeona Dada ake.

Hiyo natural tuiachie misitu kwa kweli. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Na hatukatai maana kila mmoja na akipendacho.
 
Kumbe kujenga mwili ni nafuu kuliko na kujenga uzuri.

Ukijenga mwili vizuri, hutohitaji make up tena.

Jitajidini kujenga mwili kwa vyakula bora ili muepuke msaada wa make up
😳😳😳😳😳
 
Ila wanaume ni wanafiki watupu.
Mbona wanawaacha wake zao majumbani wenye sura za naturally na kwenda kwa vimada wanaopaka make up.
Wanaume waambie waache unafiki
Dada na sio vimada pekee hata hao wake zao wanapaka sana tu.

Ila hapa wote team natural. Wanaume nyieee Mungu anawaona aiseee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…