Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

injili maana yake ni habari njema kwa waislam tunaami ni kitabu alichokuja nacho naabi issa bin mariam bin imran kwa wana wa islael na kitabu hicho hakipo kwa sasa kimepotea.
 
Aisee umeandika sana ndugu lakini hujajibu hoja ya huyu jamaa hata kidogo. Jaribu kufikirisha akili kujibu hicho anachouliza huyu jamaa. Kama hujawahi kukisikia tafuta usahihi wake. Swali kubwa na la msingi kwanini baadhi ya vitabu vilitolewa kwenye biblia kwa kigezo cha kukinzana wakati vipo vitabu vinakinzana na havijatolewa?
 
Mkuu nisaidie kupata hizo hizo old version na hivyo vya akina Yuda, Enoch nawengine walau nikipata hats copy tatu tu zinatosha mkuu
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Aiseeeeeeee
we acha tu Mkuu .. wanasema muhhamad ilikuwa haiwezekani kumpiga picture ukimpiga picture inaungua " wanaosema hivi hata hawajui tech ya camera imegunduliwa mwaka gani "... Imani mbaya sana hizi
 
MKUU NIPO KUSAIDIA,UNAWEZA KUNIAMBIA TOFAUTI KATI YA AYA HIZO MBILI(MWANZO 50 NA MATENDO 7)WEWE UNAONA NI NINI?.
 
Ushahidi mkuu unaongea bila ushahidi
 
Ni nini kinachokuonesha kwamba mistari mingine ilifutwa na mingine kuongezwa mkuu
 
MKUU NIPO KUSAIDIA,UNAWEZA KUNIAMBIA TOFAUTI KATI YA AYA HIZO MBILI(MWANZO 50 NA MATENDO 7)WEWE UNAONA NI NINI?.
Tofauti ni kwamba mwanzo 50 na matendo saba zinakinzana wapi Yakobo alizikwa maana shechem na macpelah ni kama Kibaha na Geita alafu kabila liliowauzia hayo makaburi yanakinzana mmoja anasema ni kabila la Wahiti mwingine kabila la Hamron ambao yote ni makabila tofauti kabisa kama wasukuma na wachagga ndio maana nikasema kama walikinzana Je kivp wawe wameongozwa na roho takatifu alafu wakinzane ndio hoja yangu imejikita hapo.....
 
Ni nini kinachokuonesha kwamba mistari mingine ilifutwa na mingine kuongezwa mkuu
Si nimeweka mistari ambayo ilikuwepo Kwenye KJV ila imefutwa na NIV?? Au ulitaka ushahidi gani zaidi
 
Ushahidi mkuu unaongea bila ushahidi
Ushahidi gani unataka?? Si ufungue Biblia ya King james alafu linganisha na NIV alafu uone kama hii mistari niliyoweka humu haijafutwa!! Kwani kipi kigumu
 
Mkuu huu uzi tayari umeuandika au tuendelee kusubiri?
 
Sawa Mkuu nimeelewa hoja zako!!.

MAJIBU YA MASWALI YAKO NI KAMA IFUATAVYO:

WAANDISHI WOTE WAWILI WAKO SAHIHI KWA ASILIMIA MIA KABISA,UNACHOPASWA KUFAHAMU NI KUWA MWANDISHI WA MATENDO AMEONGEZA HABARI NYINGINE/MPYA.

"HAELEZI HABARI YA KIFO CHA YAKOBO NA MAHALI PA MAZIKO YAKE PEKEE,BALI ANAELEZA PIA KUHUSU VIFO VYA PATRIARCHS(WAZEE) NA MAHALI WALIPOZIKWA"

1:UTOFAUTI WA MAENEO.(MAKPELA NA SHEKEM)

Katika kitabu cha Mwanzo 50: 13 Biblia inaeleza,

"Kwa kuwa wanawe wakamchukua mpaka NCHI YA KANAANI,nao WAKAMZIKA katika PANGO ya shamba la MAKPELA,iliyo mbele ya Mamre,aliyoinunua Ibrahim pamoja na shamba kwa Efron MHITI,pawe milki ya kuzikia"

FAFANUZI: Katika aya hiyo hapo juu sehemu/eneo ambalo Nabii Musa analotaja kuwa mahali alipozikwa YAKOBO ni NCHI YA KANAANI,anaongezea habari kuwa alizikwa katika PANGO la shamba ya MAKPELA

FAHAMU : MAKPELA(Kiebrania: Me'arat ha - makhpela - The cave of double)
Sio jina la mji/kijiji au jiji kama BETHEL,YAFA,KAPERNAUM,GAZA ni jina la PANGO - Lilikokuwa katika shamba ambalo Ibrahim alilinunua pamoja na shamba ili afanye kuwa mahali pa kuzikia Watu wake - JINA LA MAHALI HAPO NI KIRIATH - ARBA/HEBRON.
Rejea,Mwanzo 23: 1 - 9
....."9" ili kwamba anipe PANGO YA MAKPELA iliyo katikati ya shamba lake ...."

-Kisha anamalizia kutaja jina la MTU aliyemuuzia Ibrahim SHAMBA pamoja na PANGO lililo ndani yake kuwa ni Efroni,kutoka Katika kabila yake ni MHITI.

TUKIREJEA:Katika kitabu cha MATENDO : 7:15 - 16,Biblia inaeleza,

"Basi YAKOBO akashuka mpaka Misri;AKAFA YEYE (NA) BABA ZETU;wakachukuliwa mpaka SHEKEM,wakazikwa katika kaburi lile,ambalo Ibrahim alilinunua kwa kima cha fedha kwa wana wa hamori huko SHEKEM"

FAFANUZI:Mkuu Mwandishi wa MATENDO anaelezea habari mbili kwa wakati mmoja( TWO NEWS IN ONE/A SINGLE CONTENT),habari hizo ni;

"Basi YAKOBO akashuka mpaka Misri;AKAFA YEYE........"

1 :KIFO CHA YAKOBO NA MAHALI ALIPOZIKWA - KIRIATH - ARBA/HEBRON/MAKPELA(.Mwandishi anasema;"Katika kaburi lile,ambalo Ibrahim....")

"......NA BABA ZETU..."

2:KIFO CHA BABA ZAKE NA MAHALI WALIPOZIKWA - SHEKEMU
(HAPA SHEKEMU WAMEZIKWA NABII YUSUPH NA WANAWE,NA BAADHI YA WANA WA NABII YAKOBO.HADI LEO PANAITWA;

*QEVER YOSEF(Hebrew)/QABL YUSUF(Arabic). - "Kaburi la Yusuph"

HIVI LEO NI SEHEMU ILIYO KATIKATI YA MLIMA GEZARIMU NA EBEL,UMBALI WA MITA 300 KASKAZINI MWA SHEKEMU/SYKAR.

NOTE/KUMBUKA: KIRIATH - ARBA/ILIPO MAKPELA NA SHEKEMU ZIKO KATIKA WILAYA MOJA - INAYOITWA SAMARIA.

PILI: UMBALI KUTOKA MIJI HII MIWILI SIO KAMA ULIYOELEZA KUWA NI SAWA NA KUTOKA *KIBAHA - GEITA* AMBAPO NI KILOMETRES 850.

BALI NI MILE 50/KM 75 SAWA NA KUTOKA BUNDA - MUSOMA/AU DAR - BAGAMOYO/MVOMERO
((AMBAO NI UMBALI WA KAWAIDA KABISA,IKIWA MIJI IMO NDANI YA WILAYA TU)

MWISHO:Mwandishi wa MATENDO HATAJI KABILA anaposema HAMORI bali anataja JINA LA UBINI/SONS OF HAMORI.

..."16" Ambalo Ibrahim alilinunua kwa kima cha fedha kwa WANA WA HAMORI...."


MLINGANISHO.

-Waandishi wote wanataja YAKOBO alikufa.
-Wote wanakubaliana kuwa alifia MISRI
-Wote wanakubaliana kuwa alizikwa katika kaburi la Ibrahim katika PANGO/MAKPELA
-Mmoja anataja kabila la waliomuuzia Ibrahim shamba kuwa ni MHITI,mwingine anataja jina la ubini(sons of).
-Wote wanakubaliana kuwa watu wa ukoo wa Ibrahim walizikwa mahali/eneo/wilaya/mkoa mmoja kama Ibrahim aliyotaka.
- Mmoja analezea habari za baba zake wengine WALIOZIKWA SHEKEMU(Sio YAKOBO),mwingine hawaelezei.

REJEA;MWANZO 12:6

"ABRAM akapita katikati ya nchi mpaka mahali PATAKATIFU PA SHEKEMU,mpaka mwaloni wa More.Na WAKANAANI siku zile walikaa katika NCHI HIYO.

Natanguliza shukrani Mkuu.
 
Mkuu Dukeson nimekuelewa sana tu na ningependa JF iwe hivi yaani mtu anapoleta hoja inapingwa kwa hoja nzito kama hii sio mipasho au matusi!! Nina maswali nitarudi ila nimependa ulivyojenga hoja mkuu ubarikiwe sana.
 
Mkuu Dukeson nimekuelewa sana tu na ningependa JF iwe hivi yaani mtu anapoleta hoja inapingwa kwa hoja nzito kama hii sio mipasho au matusi!! Nina maswali nitarudi ila nimependa ulivyojenga hoja mkuu ubarikiwe sana.
Amina sana Mkuu;
wewe ni mmoja wa watu unaoniongezea vitu vipya maishani mwangu,mengi nimejifunza kupitia wewe ubarikiwe sana,lengo letu ni moja tu KUJIFUNZA na LEARNING IS THE LIFETIME PROCESS.
Shukrani Kiongozi.
 
Neno Bilia linamaanisha ni mkusanyiko wa vitabu -collection of books.Ninavyojua Biblia ina Maudhui yake -Yaani kuna taarifa juu ya anguko la mwanadamu,NA Ukombozi wa wa mwanadamu.

Ni Vitabu vya dini vilivyokusanywa na kuwekwa pamoja.Vitabu ambavyo maudhui yake hayakuwa sawa na vingine (kupingana)viliachwa.Siri ya biblia huwa haipingani. Kama kuna sehemu ipo wazi inasema usinywe kilevi ,haiwezekani biblia hiyo hiyo iseme tunywe pombe au usile nguruwe na pengine iseme kula nguruwe.

Sisi Wakristo tunaamini biblia iliandikwa na waandishi waliovuviwa uwezo kwa roho mtakatifu. Hivyo kuielewa unahitaji uwe na uwezo ndani yako wa roho mtakatifu,la sivyo utachanganya na kuiona haipo sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…