Siri iliyofichwa kuhusu BIBLIA

Waislam hatuwezi kusoma Bible ila tutasoma Injili, zaburi, taurati, na Qur'an tu. Sisi hatujui na wala hatuamini kuwa Bible ni kitabu cha Mungu.
Hivyo vitabu navipata wapi nikavisome aisee?
 
Baada ya Kristo Yesu kupaa kurudi mbinguni kwa baba na kuketi mkono wake wa kuume hata pale baba atakapowaweka maadui zake chini ya miguu yake, kanisa likapitia adha kuu na mateso mengi, huu ulikuwa ni mpango wa shetani wa kuliua kanisa.

Tunaweza kuona wale mitume kumi na moja na Paulo akiwa wa kumi na mbili kwa nafasi ile aliyoipoteza Yuda Iskariote jinsi walivyopitia adha na mateso mengi, hata jinsi mtume wa mwisho Yohana Wa Kisiwa Cha Patmo alivyochemshwa kwenye tank la mafuta lakini hakufa, walipoona hafi wakaona ngoja tukamtupe katika kisiwa cha Patmo, kisiwa hicho hakina watu na huko kunaishi viumbe hatari na majoka hivyo walidhani basi huko hao viumbe wangemwua, lakini huko ndiko akapewa Ufunuo wa Yesu kristo wa matukio ya siku za mwisho uitwao "Ufunuo Wa Yesu Kristo Kwa Yohana", hili jina linalotumika sasa "Ufunuo Wa Yohana" lilibadilishwa na watu flani katika harakati hizihizi za upinga Kristo, nitaeleza kwanini. Ikumbukwa huyu Yohana ndiye yule mwanafunzi wa Yesu ambaye Yesu alimpenda sana, na pia alikuwa ndugu yake Yesu, ikafika mahali wanafunzi wengine walifikiri huyu Yohana hafi.

Biblia tuliyonayo sasa ya vitabu sitini na sita imeandikwa na watu tofauti tofauti wapatao arobaini ambao hawakuwahi kufikiri hata siku moja kwamba vitabu vyao vitakuja kuunganishwa na kuwa kitabu kimoja, na watu hawa waliandika vitabu vyao kwa nyakati tofauti tofauti, hawakukaa pamoja wala kujadiliana wala kushirikiana katika kuviandika.

Baada ya mtume wa mwisho kuondoka duniani, Yohana, miaka kadhaa baadae, ndipo shetani alijiuliza sana kwamba kwa nini kadiri anavyozidi kulitesa kanisa ndivyo hivyo kanisa linavyozidi kuongezeka kwa kasi na watu kuwa na imani ya Kristo na kuutetemesha ufalme wake wa giza zaidi.

Baada ya shetani kujiuliza sana ndipo akaja na mbinu mpya ya kuanzisha kanisa lingine ambalo litakuwa mfano wa nuru na watumishi wake watakuwa mfano wa mwana kondoo(mfano wa Yesu). Na pia shetani akaleta amani kati ya kanisa na serikali za kidunia na ikatolewa nafasi kwa viongozi wa kanisa kuchukua nafasi pia za uongozi serikalini. Kanisa likapata raha pasipo kugundua kumbe ilikuwa mpango wa shetani kwa sababu aliingiza watu wake katika kanisa walio ndugu wa uongo walioingizwa kwa siri katika kanisa.

Sasa shetani akawa amefanikiwa hilo lakini akawa anapiga hesabu ni namna gani ataingiza sanamu katika kanisa kwa sababu bado kuna watu wenye imani waliojichanganya kwenye kanisa lake la uongo alilolianzisha hivyo alijua atapingwa.

Sasa siku mpango wa kuingiza sanamu katika kanisa ndipo hapo mpango huo ulipingwa na vita kali ilitokea na watu wengi kuuawa kwa kuitetea imani. Na shetani akafanikiwa kuingiza sanamu katika kanisa lake alilolianzisha na ni kipindi hicho Biblia Original zilichomwa moto na zingine kutupwa baharini Biblia tulizonazo sasa zimepunguzwa maneno na vitabu.

Katika Biblia zilizokuwepo kipindi hicho Yesu alizungumza mengi, mpaka mpango wa dini moja utakao tokea nyakati za mwisho na alitabiri mambo mengi ya kipindi hichi, na nyakati za mwisho itakavyokuwa, jinsi kanisa litakavyoondolewa kwenye msingi na jinsi litakavyo rejesha kwenye msingi, jinsi maadui zake watakavyowekwa chini ya miguu yake na ni kwa namna gani n.k n.k n.k, yote hayo yalipunguzwa yasiandikwe kwenye Biblia tuliyonayo sasa tusije tukayasoma tukashtuka na kugundua uongo wao. Na ili tusiweze kupambanua ipi ni nuru halisi ipi ni mfano wa nuru, wapi ni watumishi wa Mungu wa kweli na wapi ni wa uongo. Kitabu cha "Ufunuo Wa Kristo Kwa Yohana", kikabadilishwa jina kikaitwa "Ufunuo Wa Yohana", lengo la yote ni kujaribu kutupotosha sisi kanisa.

Hawakuishia hapo karne ya sita Uislamu ukaasisiwa na Papa wa kipindi hicho na namna ya uendeshaji ibada zao n.k n.k n.k, sielezei sana hili swala ila nnachotaka kusema katika mpango wa dini moja unaosimamiwa na Papa wa sasa tayari wamekwisha kujiunga dini kumi na tatu ikiwemo Islamu wale ambao ni ndugu. Yote haya yalitabiriwa ila yameng'olewa kwenye Biblia tusiyaone.

HITIMISHO
Kwa wale wenzetu wa imani tofauti wanaotushawishi tujiunge nao kwa kusema kwenye Biblia yetu ya zamani kuna maandiko yanataja mji wao mtakatifu ili tuuache ukristo. Napenda kuwapa ujumbe kwamba wanapofichua yaliyomo kwenye Biblia yetu ya zamani wafichue na haya niliyoyaandika.

Biblia Original bado zipo kwenye store za Rumi, nchini Italia.
 
@zitto junior pitia hii
 
Rafiki umeandika vingi, lakini vingi vinahitaji nukuu (reference). Kwa maoni yangu kuna vitu umechanganya, ila siwezi sema kitu mpaka utuletee nukuu hizo.
 
Rafiki umeandika vingi, lakini vingi vinahitaji nukuu (reference). Kwa maoni yangu kuna vitu umechanganya, ila siwezi sema kitu mpaka utuletee nukuu hizo.
Ipi hapo unataka nikupe reference yake katika hayo niliyoyaandika?
 
navuta siti hapa stoki nasubil wajuvi... karbn
 
Sisi Jews tunasheherekea mwaka mpya mwezi wa abib ambao ni wa kwanza kitabu chetu ni The book of Yhweh ambacho kina Torah tu,hatuvuki mstari,kwenda kwa kina yohana,
Halelujah hallelujah, MATZAH TUDOH KHAI ACHCTY.
 
kumbe hicho kitabu kimeandika utopolo namna hiyo ilikuani sahihi kifichwe ili kificha aibu kwa mwandishi
 
mwanasayansi yupi na wamethibitisha wapi,tupe link
kamwe biblia haijawahi kusema dunia ni duara as globe, ila ni duara kama disc! hivi ndivyo wanasayansi hata wa sasa walivyothibitisha, na kufuta uongo uliopenyezwa kwa miaka mingi kuwa dunia ni duara linalozunguka mile 1000 kwa saa.None sense!
 
hii
hii habari yote imeandikwa kama hadithi za abunuwaasi au sungura na fisi hakuna rejea yoyote wala ushahidi,ulijuaje ka shetani alikaa akaanza kujiuliza sana ,nanialikua nae wakati anajiuliza.baada ta yesu kuketi kuume kwa mungu ndio kanisa likaanza kuteswa ,yani kanisa liteswe wakati yesu tayari amekutana na Mungu mkuu mwenye nguvu ameketi pembeni yake upuuzi na upumbavu mtupu
 
paulo hakuwa mtume wa 12 ili kuziba nafasi ya yuda. Mtume wa 12 aliye chaguliwa kuziba nafasi ya yuda aliitwa Mathia
 
paulo hakuwa mtume wa 12 ili kuziba nafasi ya yuda. Mtume wa 12 aliye chaguliwa kuziba nafasi ya yuda aliitwa Mathia

Hilo nalijua. Mungu hafanyi uteuzi kwa kuangalia kura zilizopigwa na wanadamu, kwani baada ya kura kupigwa ulimsikia tena huyo Mathia akitajwa popote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…