Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710
Dude, planet earth is SPHERICAL.
 
Nijibu mimi peke yangu.
Kama dunia ipo tambarale mbona dunia visiwa vya zanzibar hatuvioni tukiwa hapa dar es salaam? Au vimo ndani ya maji?
 
Usidhani nimekosea kukushauri ukamkumbatie mkeo. Maana unachofanya ni kujaribu kujitwika dunia kichwani.
Ni nini kimeviziba visiwa vya zanzibar mpaka sisi huku dar hatuvioni kwenye dunia yako flat?
 
Kaka hili swali lako la mwisho nimelipenda.
 
Usidhani nimekosea kukushauri ukamkumbatie mkeo. Maana unachofanya ni kujaribu kujitwika dunia kichwani.
Ni nini kimeviziba visiwa vya zanzibar mpaka sisi huku dar hatuvioni kwenye dunia yako flat?
Lengo kubwa ni kuelekezana Kuna kitu kinaitwa worldview ni mtazamo wa watu wengine kuhusu dunia wanaionaje. Kuna watu walikuwa wanaona dunia kama meza, tambarare na duara
Naamini kabisa akija mtu kuandika uzi umbo la mstatili una pembe 5 watambisha sana na kuonekana mjinga tumekalilishwa kuwa mstatili una pembe 4 ajuwi kama mtu alikaa chini kufikiria na wengine wakifikiria wanaonekana wajinga. Kuna kanuni ya pembe 3 watu walikaa chini kufikiri wakatengeneza a^2 +b^2=c^2 ukijiundia formula yako majibu utakayoyapata mmhh
Kuna kitu nafikiria hivi Galileo kwa mara anagundua dunia inazunguka jua alitumia kifaa gani? Je alitoka nje ya dunia.
 
Nimependa ujengaji wako wa hoja uliozama kwenye maandiko..
 
Jibu swali tujue:-
Je visiwa vya zanzibar vimezibwa na nini hata tusivione sisi tulio dar kwenye dunia yako tambarale??

 
Umeandika mengi.kwa kukujibu ni kwamba dunia no duara.na ndo maana duniani haina mwisho.na inazunguka.kisichozunguka ni jua ndo maana tunapata usiku na mchana.upande mmoja ukimulikwa na jua unakuwa mchana na ule upande wa pili unakuwa usiku.
 
Hapa kueleweshana kwa njia ya maandishi itakuw ngumu, cz wengi bado hawajaipata logic hasa ya utambarare au uduara wa hyo dunia.

Kwa nielewavyo mimi, sifa za uduara zipo kote kote kati ya dunia mviringo na wanaoamini dunia tambarare.
Uduara wa Dunia tambarare ni wa kama sahani, disk, au mfuniko wa ndoo, na uduara wa dunia mviringo ndio huu ambao wote tunaujua, big ball.
Kwenye kueleweshan kwanza tusipingane juu ya uduara mana wote tunaongelea dunia ya duara ila katika utofauti wa maumbo.

Tangu mwanzo nasisitiza, mtoa post hajaoteshwa, ila elimu hyo ameitafutwa haifundishwi katika mitaala kama elimu ya dunia duara/mviringo ambayo wengi tunayo.
So ktk kupingana ni lazima wote tujifunze kwanza mtazamo wa wanaosema dunia ni tambarare bila hivyo, hamtapata uelewa nakubaki na uelewa wa kile mlichokuwa mnafundiswa tangu class mimi nikiwa ni mmoja wao.

Mtoa post source yake ni www.theflatearthsociety.org tembeleeni kwnza huku mjibiwe maswali yenu bila kujaribu kumuua mjumbe.
 
mkuu samahani ivi DUNIA si ni sayari? kama ni tambarale na zile sayari zingine zinakaaga wapi?
 
Jibu swali tujue:-
Je visiwa vya zanzibar vimezibwa na nini hata tusivione sisi tulio dar kwenye dunia yako tambarale??
Jibu lake rahisi sana dunia Kuna mabonde, milima, mitelemko kama Kuna bonde, mlima, miinuko na mitelemko katika utawezaje kuona zanzibar.
Alafu kitu kingine kuwa uwezo wa macho yetu kuona ndo inasababisha zanzibar isionekane. Mfano nzuri angalia Anga utaona Kuna blue lakin hakuna mawingu ya blue, blue tunayoiona angani Mwisho wa upeo wa macho yetu kuona. Ukipanda mlima kilimanjaro kwa kutumia macho yetu Mji wa Nairobi huwezi kuona lakin ukitumia vifaa maaluma Mji wa Nairobi unaona bila shida.
 
We kweli kiboko!!!
Unapendekeza kuwa kuna mlima wa maji?
Yaani hata taa za usiku tusizione?
Acha ubabaishaji, nadharia zako ziliishi karne nyingi sana zilizopita na zilithibitika kuwa ni uongo, uongo, uongooo.
 

Kaka huyo jamaa moudytunechi amekaririshwa kwenye misahafu na alipopata wenzie wa flat earth ndio ameshindwa kabisa kuachia ubongo wake ufanye kazi ya kutafakari, mifano mitatu ambayo labda inaweza kumfikirisha ni hii

1: kama upo kwenye basi na linaenda speed na linaenda mbele, je yeye kama abiria anaweza kitembea kwenda mbele na kurudi nyuma?, je atatembea kwa speed ya basi ya 120km/hr? ITAWEZEKANA KWA SABABU NA MTU ATAKUWA SUBJECTED KWENYE SPEED YA BASI

2: je yeye akiwa kakaa kwenye basi lenye speed say 120km/hr akachukua chungwa akarirusha juu pale alipokaa je chungwa halitamrudia yeye mwenyewe? Je akirirusha nyuma au mbele au atakako halitaenda? ITAWEZEKANA KWA SABABU CHUNGWA NALO LIPO SUBJECTED KWENYE SPEED YA BASI

3: je alishawahi kumfatilia mdudu kama nzi akiwa kwenye gari lenye speed?, nzi ana uwezo wa kupaa na kwenda kokote atakako hata basi likiwa kwenye speed gani, ANAWEZA HIVYO KWA SASABU NA YEYE YUPO SUBJECTED NA SPEED YA BASI

HIYO MIFANO YOTE INAONYESHA, JAPOKUWA DUNIA IKO SPEED NA SISI PIA NA VYOMBO VYETU VYA USAFIRI MABASI, NDEGE NK. TUPO SUBJECTED NA SPEED YA DUNIA na tunaweza kwenda kokote iwe along the speed direction au opposite yake
 
We kweli kiboko!!!
Unapendekeza kuwa kuna mlima wa maji?
Yaani hata taa za usiku tusizione?
Acha ubabaishaji, nadharia zako ziliishi karne nyingi sana zilizopita na zilithibitika kuwa ni uongo, uongo, uongooo.
Wewe kweli umeenda shule? , nakuwa na wasiwasi na wewe ujuwi kwenye floor ya bahari Kuna milima, mabonde, miinuko na mitelemko.
Kuna watu tambarare iliyozugumzwa hawaielewi.
 
Mkuu,nianze kusema tu kuwa nasikitika sana baada ya kusoma uzi huu kwa namna watu walivyochangia na wanavyochangia......

Mtoa mada amekuja na kuandika mambo mengi sana namna anavyosema juu ya umbo la dunia na ushahidi ameweka.Ameelezea kuwa yeye anaamini kuwa umbo la dunia ni flat,lakini akasema ni flat ya namna ipi anayoizungumzia.Shida ya kwanza ya watu inaanzia hapa...

Kuna watu wanapoona neno flat basi wanakimbilia kwenye fikra zao namna wanavyofikiria flat,wanafikiria flat kama ya meza tu,hapa ndipo panaponisikitisha kuliko mahala pengine popote pale.Mtoa mada ameelezea kuwa dunia ni flat duara yaani kama cd na michoro ameweka,watu wanakuja kujenga hoja kutoka na fikra za flat ya meza au umbo ambalo soyo duara kabisa.

Kwa kukuthibitishia hili angalia watu wanaojenga hoja kwa kuonesha kuwa mtu anaweza kutoka Dar hadi Sydney kisha akaenda Marekani kisha akarudi Accra na baadaye kurudi Dar.Ukiangalia hoja hii imelalia kwenye fikra za dunia isiyokuwa duara ya namna mleta mada aliyoizungumzia kwenye mada yake maana ukiangalia kwenye hoja za mtoa mada utaona kuwa mtoa mada naye anasema kuwa dunia ni duara lakini siyo mviringo kama tufe bali ni mviringo kama CD.Kwa mviringo huu unaweza kabisa kufanya safari hizo nilizotaja hapo juu bila kuhitajika kurudi nyuma.

Hoja ya watu kuzunguka dunia na kujikuta wamerudia pale pale,hoja hii nayo haishindikani kwenye hoja ya dunia duara ya kama sahani.Ukiangalia utaweza kuona kuwa inawezekana kabisa kuwa mtu akatoka Afrika ya kusini,akapitia Australia kisha akafika Amerika ya kusini kisha akarudi tena alipotoka maana atakuwa amezunguka duara inayosemwa na mtoa mada.Kwa maana hii bado hii haithibitishi kabisa kuwa dunia ni duara kwa maana ya tufe.....

Ameelezea mambo mengi sana pia,miongoni mwa mambo aliyozungumzia ni namna usiku na mchana unavyopatikana,watu hawasomi kabisa majibu na thread yote na unakuta mtu anakuja kurudia hoja ambazo zimeshajibiwa kwa uwazi kabisa na hili ni tatizo jingine,uviovu.Huwezi kujifunza mambo mazito kama haya huku ukiwa mvivu,huwezi na hutaweza kabisa kamwe......

Hoja nyingine ni route za ndege.Mtoa hoja amesema kuhusu hili,watu badala ya kujibu sababu ya ndege kutokuwa na rout hizi wameongeza swali kuwa vipi kuhusu ndege binafsi.Kwanza nafahamu kuwa kuna maswali ambayo ukiulizwa unaweza kuuliza aina fulani ya swali ambalo ukilijibu linaweza kukupa jibu la swali lako,lakini swali hili linaweza kujibu au kutokujibu swali kuu la mtoa mada kwasababu zifuatazo....

1;Hakuna uthibitisho ambao umetolewa hadi sasa wa uwepo wa ndege binafsi zinazokatiza north pole au south pole...

2;Kama kuna huo uwezekano wa ndege binasi kukatiza hapo,ni kwaninio ndege za kibiashara zisipite hapo ili kupunguza umbali mrefu? Kutoka South Afrika hadi Urusi kupitoa Siuth pole na kupitia katikati ya bara la Afrika hadi Geneva kisha Moscow wapi ni karibu?

Kimsingi hoja zote hizi ni mfu na zinaongeza maswali zaidi.Hakuna aliyejisumbua kujibu kuhusu ukweli wa binadamu kwenda mwezini.Hakuna ushahidi wa bibadamu kwenda mwezini....

Suala la meli kitoonekana kwa macho inapokuwa mbali ya macho yako hili mtoa mada amelijibu na ndiyo jibu bora kabisa linaloenezea suala hili.Watu walikuwa wanachukulia suala hili la meli kuzama kuwa ni moja ya ushahidi wa duara ya dunia,hii ikiwa na maana kuwa meli ile inakuwa imeshafika kwenye upande mwingine wa duara ya dunia.Mtoa mada amesema kuwa,kama inakuwa hivyo basi ukichukua kifaa maalum cha kuonea mbali usingeiona meli maana itakuwa iko kwenye upande mwingine wa duara ya dunia.

Mfano mzuri wa jambo hili ni kuchukua kijiti kifupi na ukakichoma kwenye chungwa kwenye upande mmoja kisha ukaligeuza chungwa lile upande mwingine kisha ukaanza kutazama,hutaweza kukiona kijiti kile kwakuwa kitakuwa kwenye upande ambao unazuiwa na muinuko wa chungwa lile hata kama utachukua kifaa cha kuonea mbali.Lakini ukichukua mti ukauchoma chini kwenye barabara iliyonyooka kisha ukaenda umbali wa kilomota 10 ukatazama mti ule hautauona bado lakini hii haimaanishi kuwa huuoni kwakuwa upo kwenye upande wa pili wa dunia bali ni kwasababu macho yako hayaoni tu,ukichukua kifaa utaweza kuuona mti huu.....

Kwa mfano huu ni dhahiri kuwa hoja za dunia duara bado zimegaragazwa kwenye mada hii,leteni nyingine......

Sisi tunajifunza na kuhoji pale ambapo tunaona kuna haja ya kufanya hivyo.......
 
Maji yapi yenye mlima! Ni haya yakimbiliayo bondeni, yenye tabia ya kuwa chini kiasi uka suggest kwa character hiyo yangemwagika kutoka kwenye tufe la dunia?
We pumba kweli!!!!
Wewe kweli umeenda shule? , nakuwa na wasiwasi na wewe ujuwi kwenye floor ya bahari Kuna milima, mabonde, miinuko na mitelemko.
Kuna watu tambarare iliyozugumzwa hawaielewi.
 
Umefelishwa tayari.
Niwekee mchoro hapa wa dunia santuri yenu unaoonyesha kupatwa kwa jua na mwezi.

Meli iki vanish upeo wa macho pale coco beach hata utumie hadubini gani huioni ng'o!!!

Kwa nini jua linachelewa kuchwea kongo compared to dar.


 
Umempa maswali yenye majibu murua
 


Unakaribia kuwa kichaa .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…