Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?


  • Total voters
    710
What About Seasons?

The radius of the sun's orbit around the Earth's axis symmetry varies throughout the year, being smallest when summer is in the northern annulus and largest when it is summer in the southern annulus. Additionally it also raises and lowers. This causes the effect of the sun appearing to move in a figure eight throughout a year.





What about Day/Night and Sunrise/Sunset?

The sun simply illuminates only a portion of the earth at a time. This also explains timezones as we can then see the path of the Sun, a circle above the flat earth.
 

Attachments

  • 1478325397615.jpg
    23 KB · Views: 97
Hivi ukisimama kwa mfano pale feli Zanzibar utaiona hata kwa hadubini?
 
Kama jua limesima mbona tunasemaga kuwa JUA LIMETOKA MASHARIKI LIKAZAMA MAGHARIBI....limeanza lini kutembea
 

ahsante sana ...Tatizo watu hawasomi facts na kutafakari ,,,,
 
Wewe uliyefuatilia hebu nipe mwanga wa hili, jamaa amesema dunia ni tambarare na maji yamezuiliwa kwa mabonge makubwa ya barafu. Swali, mwisho wa hayo mabonge ya barafu ni wapi na baada ya hayo mabonge kuna nini!
Vizuri sana kupata watanzania wanaoongelea hili swala, huwezifika kwenye mwisho wa hizo kuta za barafu , kwanini the more unavyosogea kuelekea huko utakutana na upungufu wa oxygen mkubwa, shida za baridi kali na mengi kuwa na shida ya mawimbi makubwa kwa mfano kupata concept ya Flat earth kidogo angalia movie kama Jim Carry the tru man show, Under the dorm series na pia ka search under the dorm youtube utapata more info its interesting and wondering on the more unknowns we dont know in this earth.
 
Concept Ya Day and Night kwenye flat earth na practical truth nyie kweli watu wanafanya research sio sisi wabongo tunasubiri tuelezewe kila kitu.

 
Huo ndo uthibitisho mujarab kabisa kuwa dunia ni duara, kwenye flat duara hili linawezelana vipi??? Ningependa kujua wanaopanda ndege kwenda zenji huwa wanaexperiensi muono gani!
ni kama sisimizi umemuweka ktk mpira wa basketball.
 
Nasikia kuwa hakuna ndege za abiria inayoruhusiwa kupita juu ya anga la bara la antractic maana ndo kwenye kingo za dunia.
Jana nimejikita ktk hii topic hususan North na South pole, inasemekana kuna flights toka Australia mpaka Argentina kupitia south pole.
Hii topic iko very fascinating!!
 
Hivi ukisimama kwa mfano pale feli Zanzibar utaiona hata kwa hadubini?
Unaweza hata ukasimama kwenye jengo jipya la tpa kule juu na darubini yako kali ila zenji hautoiona, pia zenji hili jengo refu la bara hawalioni hata kwa darubini sababu ya CURVE ya duara la dunia.
 
Hivi ukisimama kwa mfano pale feli Zanzibar utaiona hata kwa hadubini?
Huwezi kuona, alafu hii dhana ya dunia tambarare haijaeleweka kwa baadhi ya watu , kwenye sakafu ya bahari Kuna sehemu imepanda, imeshuka. Kuna point 1 kuthibitisha dunia ni duara wametoa mfano wa meli alafu mtu anayethitisha yupo nchi kavu au beach. Kuna utata captain anayeongoza meli hawajamuhusisha, Captain yeye anaona flat kwenye bahari.
kama Kuna mtu yeyote either captain umewahi kumsikia anasema sasa hivi tunapandisha au tushuka kwenye bahari yupo ndani ya chombo
 
Huo ndo uthibitisho mujarab kabisa kuwa dunia ni duara, ni kama sisimizi umemuweka ktk mpira wa basketball.
Ndugu MI nitakubali dhana ya dunia ni duara, kama meli inayotoka South Africa kuja Tanzania itakuwa inapandisha ndo sifa ya duara, Captain wa meli yeye anaona flat hakuna kupanda wala kushuka.
Ajabu zaidi meli inayotoka bandarin Cape Town inashuka, meli hii ikiwa inaelekea Cape Town inaibuka kama inapanda, ikafika dar mchezo ule ule inaibuka kama inapanda ikitoka dar inashuka. what the meaning of the circle from the equator Toward South pole. Tutumie akili za kawaida chora duara lako mtu 1 akae kwenye ncha ya kaskazin na mwingine kusini watu wote waelekee kati yupi anaye pandisha na anayeshuka.
 
Kwa maelezo yako, nadhani ni kwamba wewe watu waliopo south poles kama new zealand, australia etc watakuwa wanatembea "upside down", je unaamini ktk gravitational pull of the earth?? Kwa nini kila kitu ukikiachia kinadondoka kuelekea ardhini??
Nafikiri pia kwa mtazamo wako ni kwamba mtu akiwa south pole alafu "apae" angani akiwa huko south pole basi "ataanguka" kuelekea chini ulimwenguni.
 
Hapo kwenye meli na chungwa umejikanyaga sana. Unaongelea dunia kuwa flat ya cd alafu tena upande wa pili wa duara ambao unafanye meli isionekane??????!!!!! Hapa umechemka.
Tatizo lako linaakisi matatizo ya watu wengi sana.......

Unaposoma maandiko halafu ukashindwa kuyaelewa unayatupia maandiko hayo lawama badala ya kuchunguza kama wewe ndiyo hujaelewa na maandiko hayo hayana tatizo kabisa.Ni sawa na wewe uwe umesimama barabarani na jamaa zako wanne ambao wanakuambia kuna gari la rangi ya bluu linapita barabarani na wewe unaendelea kukodoa na hulioni gari hilo,badala ya kufikiria tu kuwa inawezekana macho yako yana matatizo hivyo yanakufanya usilione gari hilo,wewe unakimbilia kusema jamaa zako ni waongo na gari hilo halipo.....

Nimezungumzia dunia flat ya CD,haiwezekani uwe na flat ya namna hiyo halafu kuwe na upande wa pili wa duara.Tatizo nililoliona hapa ni wewe kushindwa kusoma maandiko mengi na kuyaelewa.Kwenye maandiko yangu hapo juu nimezungumzia dunaia duara ya tufe kwa namna tofauti na dunia duara ya CD kwa namna tofauti,nikatoa na mifano. Nadhani mfano wa chungwa ndiyo umekuchanganya kabisa maana niliutoa nikionesha tofauti kati ya duara ya CD na duara ya tufe [chungwa] na uwezekano wa kuuona mti.....

Suala la upande wa pili lilikuwa kwenye duara ya chungwa na siyo duara ya CD.Nilisema mti uliosimikwa kwenye chungwa huwezi kuuona kwenye duara ya chuingwa unapokuwa upande mwingine wa duara ile hata ukitumia chomb cha kuonea mbali lakini, kwenye duara ya CD ambapo hakuna upande wa pili,ukisimika mti kisha ukaenda umbali wa kilomita 10 hutaweza kuuona mti huo pia lakini,ukitumia kifaa cha kuonea mbali unauona.....

Sasa kwa kutumia logic hiyo,meli inapokuwa haionekani kwenye macho yako baada ya kwenda mbali,wale ambao wanasema dunia ni duara ya tufe hudai kuwa unakuwa huioni kwasababu inakuwa imeshapotelea kwenye duara ya dunia hivyo inakuwa kwenye upande mwingine wa duara hiyo.Lakini ukichukua kifaa cha kuonea mbali unaiona meli hiyo.Swali la msingi,je kwanini uione wakati iko kwenye upande mwingine wa duara ya dunia?

Kama dunia ni duara ya tufe usingeweza kuiona meli hiyo na ungeishia kuona maji tu pale yalipopinda lakini ni kinyume chake,meli inaonekana bado na hii inathibitisha kuwa dunia ni flat lakini duara kama CD.Kama vile mti ukiusimika kwenye barabara ya urefu wa kilomota 10,halafu mti ule ukausimika mwanzo wa barabara ile kisha ukaenda umbali huo wa kilomita 10 ukatazama hutaweza kuuona mti ule,hii haimaanishi dunia imepinda kutokana na duara yake kama tufe bali huuoni kwasababu macho yako hayana tu uwezo wa kuona umbali huo.Ukichukua kifaa cha kuonea mbali utauona huo mti bila matatizo yoyote,hii inaonesha kuwa dunia haijapinda bali ni flat.....

Nadhani umenielewa....
 
Hoja hii ni dhaifu sana kutetea dhana ya dunia duara na nafikiria labda mngeleta hoja nyingine kwa sisi ambao tunataka kujua ukweli......

Hoja hii mtoa mada ameieleza vyema sana kwenye baadhi ya maelezo yake ni kwanini unaona hivyo na siyo kwamba kutoonekana kwa meli kunasababishwa na duara ya dunia kama tufe......

Pamoja na hilo,kukuonesha kuwa hakuna duara unayodhani ipo na inathibitishwa na hicho ulichokisema hapo ni kwamba ukichukua kifaa cha kuonea mbali hiyo meli unaiona bila shida yoyote.Kama meli hukuiona kwasababu ya duara ya dunia tufe,ni kitu gani kinakufanya uione kwa kutumia vifaa vya kuonea mbali?

Think......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…