Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

Siri kubwa kuliko zote kuhusu dunia yetu tambarare

JE Dunia ina umbo gani?

  • Total voters
    710
Mi ni mmoja wa wanaoamini dunia ni tambarare duara. Maswali yako yote yana majibu.

Huwa nashindwa kuyajibu kwasababu moja kubwa, wengi wa wanaopinga huu uhalisia huwa hawapo tayari kujifunza au kutafiti wao binafsi kwakutumia maharifa yao au wanayoyapata, na hii inatokana na Elimu tuliyoipata juu ya umbo la dunia tangu utotoni tulipoanza kufundishwa mpaka tumekua,

so akili kubadilika kupitia huu uzi wenye elimu isiyofikia hata saa moja ni ngumu kupingana na elimu iliyotumia miaka katika kujifunza umbo la dunia.

Huu uzi ukiuchukulia kama sehemu yakutafakari upi ni ukweli hakika utaitafuta elimu yake na majibu ya maswali yako yote utayapata na utayahoji kulingana na usahihi wake, kinyume na hapo utaendelea kubishana mpaka mshindi apatikane na ndio maana kumewekwa hadi Kura ili kuwajua washindi na washindwa.

Kubwa la kuanza kujiuliza
. Je Ni Kwanini tumefundishwa juu ya Umbo la Dunia?
. Je Ni vitu gani tungefeli maishani kwasababu ya kutokujua Umbo la Dunia?
. Na mwisho Ni kwanini tuambiwe Jua limesimama ilhali tunaona linatembea kama Mwezi?

Wengi wanahoji ninnini sasa Sababu ya kudanganywa juunya Umbo la Dunia?

Jibu lake ni Somo lingine Pana zaidi na linalohitaji Utulivu Sana ili uweze kujua Vita vya Ulimwengu wa Kiroho. Na Silaha moja wapo ni Namna ya kumpotosha Mwanadamu juu ya Ukweli wa Uumbaji Wa Muumba vyote ambapo itamfanya mwanadamu awe mbali na Kumuamini Anepingana Nae.

"TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAHARIFA"
Mtu ambaye hata kuandika Maarifa hawezi kila kitu ataona anaongopewa tu, sioni point ya kukuelewesha
 
Uthibitisho ni uthibitisho!!! Wether hauridhishi, haijakamilika au sio wa kweli utaendelea kuitwa uthibitisho. Kwahy wewe unatakiwa useme uthibitisho huo hauridhishi kivipi, haujamilika wapi au sio wa kweli kivipi full stop.
Vizuri,..kama kwako kila kinachoitwa uthibitisho ni uthibitisho basi vizuri endelea kuamini hivyo.
 
Unaojulikana si umesema umesoma na ndio maana unaukataa? Sasa wewe ndio utueleze wapi Kuna changamoto na sio kuja na hoja ya tambarare. Malizana kwanza na sababu za kuikataa then Fanya utafiti wako kuhusu utambarare
Sababu kuu ya kukataa hiyo nadharia ya dunia tufe linalozunguka ni kwamba kwenye uhalisia ni kitu ambacho hakionekani,......ilipaswa nadharia husika iwe supported na reality kwenye mazingira lakini kwa bahati mbaya haipo hivyo,.

Kwenye uhalisia Dunia ni flat na haionekani, wala kuhisiwa kwamba ina move,....
 
BTW, nilikupa picha za Dunia ulizoomba ukaishia kusema ni katuni sema zile picha ukatuni wake ni nini? Clear Kila kitu unachoopinga au kuongea humu sio kukimbia.
Hizo sio picha halisia,...Ni computer generated images,.. mimi ni mtu wa fikra huru so nadhani ili kuondoa utata leteni video halisia not CGI ikionyesha umbo la Dunia in all sides 🌎 ,.....Video itaweza kuonyesha Nchi na Vijiji hata upside down.....kisha video itaweza kutuonyesha jinsi Dunia inavyozunguka.,,,,,

Hapo tunaweza kuondoa utata au unasemaje?
 
Sababu kuu ya kukataa hiyo nadharia ya dunia tufe linalozunguka ni kwamba kwenye uhalisia ni kitu ambacho hakionekani,......ilipaswa nadharia husika iwe supported na reality kwenye mazingira lakini kwa bahati mbaya haipo hivyo,.

Kwenye uhalisia Dunia ni flat na haionekani, wala kuhisiwa kwamba ina move,....
Yaani macho yako yanaona less than 5 percent ya Dunia nzima then una conclude et Dunia nzima ni tambarare? Yaani hii ndo sababu yako???
 
Hizo sio picha halisia,...Ni computer generated images,.. mimi ni mtu wa fikra huru so nadhani ili kuondoa utata leteni video halisia not CGI ikionyesha umbo la Dunia in all sides 🌎 ,.....Video itaweza kuonyesha Nchi na Vijiji hata upside down.....kisha video itaweza kutuonyesha jinsi Dunia inavyozunguka.,,,,,

Hapo tunaweza kuondoa utata au unasemaje?
Sababu za kusema hizo picha ni CGIs??

Sio unaropoka tu kuwa sio halisi, Kwa technology ya Sasa generated images zote zinaweza kutambuliwa, Sasa nipe sababu za wewe kuita hizo picha zimekuwa generated.

eo_pe_14797031062_4cbe0f218f_o_sm.png

eo_pe_iss062e117852_sm.png
 
Video itaweza kuonyesha Nchi na Vijiji hata upside down....
Unaona usivyotumia akili? Unataka video ya upside down?? Ipigwe kutoka wapi? Unajua ni Kwa umbali Gani unatakiwa uwe Ili upige picha uoneshe umbo zima la Dunia? Sasa Kwa huo umbali utaona vipi upside down? Au utazoom vipi mpk uone maybe watu au miti ya Duniani ipo upside down?? Tumia akili kuwaza au kama unabishana tumia logic.
 
Yaani macho yako yanaona less than 5 percent ya Dunia nzima then una conclude et Dunia nzima ni tambarare? Yaani hii ndo sababu yako???
Wewe mbona macho yako yanaona less than 5% ya Dunia nzima., kisha unahitimisha kwamba Dunia ni tufe na inazunguka...?

Kwanini unafanya double standard?,...wewe apart from kuambiwa Dunia ni tufe linalozunguka,..huwezi kuthibitisha on your own anything kuhusu hivyo ulivyoaminishwa...,nasema uongo?

Thibitisha basi kwamba Dunia inazunguka,..Mpaka saa 4 asubuhi ya leo tarehe 9 Disemba ukishindwa kuthibitisha kwamba Dunia inazunguka basi utakua unaamini blindly...!
 
Unaona usivyotumia akili? Unataka video ya upside down?? Ipigwe kutoka wapi? Unajua ni Kwa umbali Gani unatakiwa uwe Ili upige picha uoneshe umbo zima la Dunia? Sasa Kwa huo umbali utaona vipi upside down? Au utazoom vipi mpk uone maybe watu au miti ya Duniani ipo upside down?? Tumia akili kuwaza au kama unabishana tumia logic.
Duh,..kwani video lazima ipigwe na Binadamu kwamba asimame umbali fulani?

Si mtumie hata advanced drones kuonyesha umbo kamili la Dunia na jinsi inavyozunguka kwa uhalisia wake?
 
Sababu za kusema hizo picha ni CGIs??

Sio unaropoka tu kuwa sio halisi, Kwa technology ya Sasa generated images zote zinaweza kutambuliwa, Sasa nipe sababu za wewe kuita hizo picha zimekuwa generated.

View attachment 3172701

View attachment 3172702
Waliotengeneza hizo picha wenyewe wanakuambia kwamba zimeongezewa vitu fulani kwa kutumia computer kwa madai kwamba wakitoa hizo picha kama zilivyo watu watashindwa kuzielewa so wanasema wana edit ili kuzifanya ziwe clear zaidi... kama unabisha jitahidi usome descriptions/captions ya hizo picha toka kwenye taasisi ulizochukulia.
 
Tukifanya mdahalo live utaweza kuthibitisha kwamba Dunia ni tufe linalozunguka?

Ngoja sasa nadhani huu mtego unaotaka ndiyo mzuri,....nikiwa tayari nitakufahamisha.
Ndiyo, kama nilivyoweza kukuthibitishia hapa nitakuthibitishia pia meanwhile wewe hautoweza kuthibitisha kama dunia ni flat na haizunguki.
Hizo mambo za kusema nikiwa tayari ndo ngonjera nisizozitaka, wewe sema precisely siku gani tualike watu hapa tufanye mdahalo kila mtu aweke hoja zake na azitetee hoja zake.

NB. Huwezi na hutoweza kamwe kuthibitisha kama dunia ni flat. Kama unajiamini taja siku hapo tuchambue hoja
 
Ukisema hakuna uthibitisho uliopewa kama dunia ni tufe unakuwa na upungufu wa akili na mropokaji,
Wewe ndiye hujaleta uthibitisho wowote hapa kuelezea madai yako.
Dunia saivi ni kama kijiji tu hakuna kufichana, fortunately kuna mashirika ya anga zaidi ya 70 na idadi kubwa ya wana anga, hao wote wamefanikiwa kutoka na kupata picha za dunia na kuonesha ikiwa sphere na hakuna yoyote anayeclaim kama dunia ni flat amewahi kufanya hivyo ila tu mkaamua kusema haya mashirika yote Yanaongopa (kwasababu ambazo hamjaziweka wazi) sasa huoni kama ni ukichaa huo mdogo angu?

Taja siku hapa tualike watu mdahalo ufanyike live sio kusema nikiwa tayari blah blah blah, itakuwa tayari lini?
 
Kwanini unafanya double standard?,...wewe apart from kuambiwa Dunia ni tufe linalozunguka,..huwezi kuthibitisha on your own anything kuhusu hivyo ulivyoaminishwa...,nasema uongo
Hivi kaka Kwa maana hiyo umuhimu wa elimu haupo sasa? Kama kusoma na kureason unasema ni kuambiwa na kuaminishwa?? We umepewa uthibitisho sema ni wapi haumake sense.

Sijui ww upo katika field Gani, lkn Kwa upande wangu Nina application za GIS, spherical earth inaapply huku na unamake sense. Inamaana unataka kunambia kuwa tunadanganywa watadanganya katika field ngapi na Bado wamake sense, basi hao watu ni magenius sana.
 
Thibitisha basi kwamba Dunia inazunguka,..Mpaka saa 4 asubuhi ya leo tarehe 9 Disemba ukishindwa kuthibitisha kwamba Dunia inazunguka basi utakua unaamini blindly...!
Point yako ni nn? Kuwa Dunia ni tambarare au Dunia sio duara? Unataka nisemeje nn kipya kuhusu umbo la Dunia duara? Umesema umesoma sema wapi panakuchanganya kama hujasoma inamaana unabisha kitu hujui?
 
Waliotengeneza hizo picha wenyewe wanakuambia kwamba zimeongezewa vitu fulani kwa kutumia computer kwa madai kwamba wakitoa hizo picha kama zilivyo watu watashindwa kuzielewa so wanasema wana edit ili kuzifanya ziwe clear zaidi... kama unabisha jitahidi usome descriptions/captions ya hizo picha toka kwenye taasisi ulizochukulia.
Kwa usivyo na uelewa unajua kwamba NASA, ISS wapo Kwaajili ya kuaminisha watu umbo la Dunia ni tufe😄😄.

Picha hizo zinakuwa processed kwaajili ya matumizi fulani fulani kutokana na lengo lao wap, kama huna application ya GIS itakuwa ngumu kuelewa kwako. Mambo ya weather forecasting, minerals and water exploration Kwa kutumia GIS picha zake zinatoka kwenye hizi mamlaka kwahy zinakuwa processed kutokana na mahitaji maalumu na Wala sio Kwa ajili yako wewe eti Ili wakuaminishe kuwa Dunia ni duara. Unachekesha wewe.

Halafu kama wangekuwa wanadanganya kwann wakuambie kuwa hizi picha zimekuwa processed? Wangeweza kusema hazijawa processed na Bado utasema nn?

Bado hujaonesha ni kivipi hizo picha sio halisi😄😄, kuwa processed haimaanishi sio halisi ni sawa naww tukupige picha then hiyo picha tuipunguzie mwanga au kuongeza mwanga Sasa utasema hiyo picha sio halisi Bali imetengenezwa?
 
Back
Top Bottom