Siri niliyoipata katika kufunga siku 21 kila mwanzo wa mwaka

Kuwa mwanga au mchawi ni application ya spiritual power. Unafanya mida ya usiku kwa sababu hali ya hewa na kuna utulivu.
Mkuu sorry, uzi wako una hang sana. Sijafahamu hata una base kwa Mungu au miungu ufundishapo hapa kuingia katika ulimwengu wa kiroho ili kupata matokeo.
 
Mkuu samahani bado sijaelewa yaani swali langu hujaninibu...Hilo la Sauli kumwendea mwanamke mchawi ili Kujua ya Rohoni Ni baada ya Mungu kutokumjibu Sauli kwa Lolote....ndipo saulinakaamua kuwaendea wenye pepo wa Utambuzi

Sasa tuko kwenye Agano lililo Bora zaidi...na njia ya Kupakaribia patakatifu uko wazi kwa kila aaminiye....

Sasa Ni Jambo gani au siri gani ambayo Roho Mtakatifu ameshindwa kutufunulia Mpaka tukaitafute kwa Kuzungumza na Wafu??

Na Ni Siri gani ambayo Roho Mtakatifu haijui Mpaka kufikia Hatua ya Kuzungumza na Wafu??

Hata Bwana Yesu alituambia Huyo Roho atawafunulia Yote hata Siri na Mafumbo ya Mungu

1 Wakorintho 2:10
[10]Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
But God hath revealed them unto us by his Spirit: for the Spirit searcheth all things, yea, the deep things of God.
 
Mkuu sorry, uzi wako una hang sana. Sijafahamu hata una base kwa Mungu au miungu ufundishapo hapa kuingia katika ulimwengu wa kiroho ili kupata matokeo.
Mkuu, Mungu ana_operate kwenye ulimwengu wa kiroho na miungu pia ni hivyo hivyo. Kwahiyo itategemea dhamira/nia yako ipi. Na ndio maana mwenye uzi ameweka wazi kuwa mmoja anaweza kutumia hizo nguvu kwa nia ovu na mwingine akazitumia kwa nia njema.
 
Nadhani hapa unaongelea kitu tofauti kabisa na kile ninachokiongelea.

Hapa ninaongelea vitu vinavyotokea baada ya kufunga ukiwa serious.
Kwenye maongezi yangu hapa niliongelea kuwa unapofunga lazima uwe na lengo. Nikasema katika ulimwengu wa Roho kwa ninavyofahamu upo katika levels 6.

Nilieleza kuwa level ya kwanza ipo na kelele nyingi. Nikaendelea kusema katika level hiyo utaweza kukutana na watu waliokufa.

Hapa ninaongelea matokeo ya kufunga.
Hata hivyo hebu soma hapa:-

2 Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
2 Wakorintho 12:2

3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);
2 Wakorintho 12:3

4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.
2 Wakorintho 12:4
 
Mkuu, Mungu ana_operate kwenye ulimwengu wa kiroho na miungu pia ni hivyo hivyo. Kwahiyo itategemea dhamira/nia yako ipi. Na ndio maana mwenye uzi ameweka wazi kuwa mmoja anaweza kutumia hizo nguvu kwa nia ovu na mwingine akazitumia kwa nia njema.
Asee! Sikua nafahamu hili. Mtu afunga tatu kavu kwa Bwana halafu anaingia ulimwengu wa kiroho kufanya ushirika na miungu na kuongea na marehemu.
 

Kwani wakristo mnafungaga?
 
Heeee!!!! Mkuu wa anga nani na anafanya nn mda huo? Na je mtu akiamka mda huo akaomba nn kitatokea???
Kuna maandiko yanasema mida hiyo roho ya Mungu inashuka karibu na anga la dunia, na pia kwa upande wa giza na wenyewe unakuwa kwenye peak ya utendaji wake. Kwa maana nyingine, wakati huo anga la dunia linakuwa neutral ground... sasa itategemea wewe umepanga kujihusisha na nguvu ya upande gani kwa muda huo.
 
ubarikiwe. yote unasema ya kweli. ila mimi nilichojifunza kwenye kufunga na kuthibitisha kuwa ndicho cha kweli ni hiki:

1. kufunga hakumlazimishi Mungu atende, yaani you can never force God to act upon your desires just because of fasting.

2. kufunga kunakusaidia tu kuitiisha nafsi yako/mwili wako ili kusogea mbele za Mungu kwa unyenyekevu, na hapo ndipo utapata nafasi ya kuongea na Mungu kwa unyenyekevu. Mungu anapatikana kwenye unyenyekevu na utulivu.

3. Kufunga kwa namna yeyote ile, kwafaa sana na kuna majibu. kuna baadhi ya mambo mengine huwezi kuyapata bali kwa kufunga na kuomba, ikiwa na maana kwamba, hadi utiishe sana nafsi yako kwa unyenyekevu mbele za Mungu, na Mungu kwa hiari yake baada ya kuona unyenyekevu wako anaweza kuamua kukujibu. kwa neema yake anaweza kujibu hata kabala ya wakati uliokuwa umepangwa, au akaingilia kati kwasababu ikinyenyekea sana mbele za Mungu, unakuwa umesogea sana mbele zake hivyo anakusikia sana, and as long as wewe ni mtoto wake, ukipiga kelele anakusikia na anasogea kukusaidia kwa haraka kuliko ukiwa mbali.

4. kufunga kunakusaidia kuua kiburi cha mwili na mapenzi yake. jua kwamba, mwili siku zote hushindana na roho, mwili hupenda tamaa za dunia hii na huwezi kusogea mbele za Mungu ukiwa na tabia za tamaa za mwili/dunia hii, ila ukizifisha ukasogea kwa Mungu kwa roho, hapo utamwona kwasababu Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli. pia huwezi kupata Roho Mtakatifu bila kuufisha mwili na kuiweka roho mbele. yote hayo yanakulazimu ujinyenyekeshe mbele ya mkono wa Mungu ulio hodari, kitabu cha mika pia kinaeleza kuwa Mungu anachohitaji toka kwetu ni kujinyenyekeza na kutii Neno lake. yote haya ni magumu kufanya kama huna tabia ya kufunga kwa kuutiisha mwili ili roho iinuke na kumtafakari Mungu. ubarikiwe.
 
Mleta huu Uzi siku ukifika kuzimu utaikuta hivi kazi unayoifanya...maana unayatumia maarifa vibaya ... Unafundisha mfungo wa siku 21 afu unawaambia watu wachague uchawi au (....) Mabano haujisemi wewe ni nani - mlokole au mpagani... Neno la msalaba ni upuzi kwao wanaopotea Bali kwetu sisi tunaokolewa ni nguvu ya Mungu .. Siionei haya injili ni uwezo uletao wokovu..Kol 3;
16-17 Na kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo fanyeni yote ktk Jina la Bw Yesu mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye...Mimi ni mlokole !
 
Mleta mada uje uelezee haya mambo, kwanza unasema tupange pounti za kuomba..kivipi wakati Roho mt hutusaidia kuomba.
 
Mkuu, ni kipi unashangaa hapo?

Kwani hujui kuwa 'mwanga' na 'giza' ni kitu kimoja ila hutofautiana kwa kiasi (degree)? Ni kama joto na baridi.

Bila giza hakuna mwanga, bila giza huwezi kuelewa faida ya mwanga. Ni kama shilingi ilivyo na pande mbili, shilingi ni hiyohiyo lakini ina kichwa na mwenge. Huwezi ukatengeneza shilingi ikawa ina kichwa pekee, itakuwa haijakamilika.

Kwahiyo spiritual energy/power ni ileile. Application ya hiyo energy ndio itakuweka upande unaostahili.
 
Kabla hamjafanya hayo mambo yenu je mna uwakika na izo ibada zenu?.

Wengi wa kizazi cha leo mnauchukulia powa uwo ulimwengu wa Roho?

Kwa bahat nzuri ama mbaya hakuna wala awezaye kuingia ktk Ulimwengu huo ilihali hajafa au hayupo ktk sleeping mode, yaan hali ya nusu ufu na kuruhusu Nafsi yako kutengana na mwili na kutenganisha mawazo+fikra za mwili, kuelekea ktk ulimwengu usio onekana.

Kabla hujafanya izo ibada zako kuwa unataka kuingia ktk Ulimwengu usio ujua, unatakiwa ujuwe kuwa je unae msaidizi wa kukupa muongozo uwapo ktk uo ulimwengu?.

Naposema msaidizi namaanisha Kiumbe wa kiroho kulingana na imani yako, mfano wasaidizi hawa ni kama malaika,majini, mapepo, mashetan, ama mizimu.

Sas wew unaetamani ama unataka kuingia ktk Mipaka isiyo kuhusu, juwa kuwa unafanya kitendo cha hatari kitakacho yagharimu maisha yako, either kifo ama kuandamwa na mapepo.

Automatic unapoingia ktk ulimwengu huo lzma uwe na mwenyej atakaye kuwakilisha na kukupeleka unapostahili kwa lengo lililokupeleka huko.

Wengi hamjui kuwa Ktk ulimwengu huo kuna kila aina za viumbe wenye nguvu kubwa na wamejawa utisho wa hali ya juu, hivyo bas wew beginner unaetaka kujaribu mambo usiyoyaweza nakutahadharisha, utaumia na hutakuwa na wakumlaumu.

Enyi Viongozi wa dini acheni upotoshaji, hakuna mwenye uwezo wa kuingia huo ulimwengu kiholela namna hiyo, izo ndoto zenu na hisia mupatazo kwa kuwaza kuwa mpo ktk level ya kiroho zinawadanganya, mtapotea bure.

Namna ya kwenda huko, ni lazma uwe invited by God's willing or Satanic willing.

Ninaposema satanic willing namaanisha ni hawa wachawi,waganga, wapiga ramli na washrikina wanaoingia ktk limwengu hizo kupitia invitation ya Shetan na Ulimwengu wake, hivyo hata akiingia huko anajulikana ni wa upande wao, na wanajua anakwenda kwa madhumuni gani.

Na God's willingness ni pale Muumba wa kweli anapoamua yeye mwenyewe bila kushurutishwa na mtu na kumchukuwa mtu kiroho kupitia msaidizi wa kiroho(malaika) ambaye anakuwa mlinzi na kiongozi wa mtu huyo kumpeleka anapostahili ili akajifunze ama kupata ujumbe wa jambo fulani, ama kupata maono ya jambo fulani.

Usidanganyike na hawa matapeli kuwa huko wanajiingilia kama chooni, ndugu yangu utakufa kabra ya umri wako,

Usifanye mzaha na Mambo yaliyo juu ya uwezo wako.

Malaika wanatishaa kama huna nguvu huwez stahimili kuwaona ama kukaa nao sambamba, utakufa, hata hao viumbe wa Giza wana nguvu, huwez stahimili kuingia ulimwengu huo kama huna msaidizi ama huna nguvu za kishirikina, utakufa mapema ama ugeuke kuwa chizi.

Acheni utani nyie wafia dini, msipende kuchukulia Simplest mambo ya kiroho yanatisha, hakuna mzaha kule

Kama njaa&madhambi yamekushinda kuyahandle, sas utaweza stahimili kuingia ulimwengu usio wako? Unataka kuingiza roho yako matatani? .

Acheni mizaha someni hizo biblia zenu, hutoona watu walikuwa wakifanya mizaha na ibada za Kiroho, akina Yohana walipoingia ktk ulimwengu huo na kupelekwa kupata maono ya siku za mwisho, walikuwa na wasaidizi ambao ni malaika wenye nguvu.

Not easy
 
Wew sijui nikuite mtumishi ama nani, em tafakari kabla hujawaletea hawa izo mbinu zako za kiroho kama zina madhara ama la!.

Huwez kuingia huko kiholela namna hiyo, or otherwise uingie kupitia mind tricks kama vile Third eye opening, meditation and astral projection, accidentally unapokuwa umelala, vinginevyo haiwezekani acha kuwalisha watu watango pori
 
Siku hizi kila mtu ni mwalimu, ndiomaana hawana uchungu wanafunzi wao wakipotoka na kupotea...kamwe usije tamani kufanya jambo ambalo huna uwakika nalo, haswa kama lahusu haya Mambo ya rohoni
 
Tatizo unajifanya mjuaji. Una okoteza maneno/terms huko na kuja kuwatisha watu.

Hakuna cha kuhofia zaidi ya hofu yenyewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…