Siri usiyoijua kuhusu ndoto na tafsiri zake

Mkuu Mimi nakupinga ,swala la ndoto Ni Pana Sana,hivyo ndoto haziwezi kuwa na constants,eti ikiwa hivi basi itakuwa vile no ,nakupinga,mfano Mimi nikiota nakula ubwabwa na maharage basi hapa nijiandae kupata pesa mungu,

Kuota uko juuu unapaa hamuwezi kuwa na maana moja,lazima uangalie kwanini unapaa,na uko mazingira gani,hivyo kwa dhana hii utapata maana tofauti za ndoto ya kupata.
Mfano mtu anaota anapaa lakini chini yake anamuona mtu aliyekufa dhaman,ndoto hii inamaana Pana na haiwezi kuwa na constants Kama ulizozitaja.
 
Mkuu naomba unipe tafsiri ya ndoto hizi mbili,kwanza nilishawahi kuiota mara kama tatu nimefiwa na mzazi wangu ilhali bado yupo hai inatokea nalia sana mpla machizi ila nikiamka asubuhi sioni chozi lolote
Pili hii imeshanitokea si chini ya mara nne naota nipo shuleni na nimeshamaliza shule mda mrefu.
Msaada please
 
Mkuu shukrani kwa ufafanuzi, Mimi naota Mara kwa Mara kufanya Mapenzi na wanawake au naweza ota naona mwanamke yuko uchi kabisa kitandani, Mimi jinsia ya kiume. Mkuu naomba codes.
 
Naomba unifafanulie ndoto hizi ambazo huota Mara kwa Mara
1) Nliwahi kuota Mara kadhaa ngombe wa nyumbani kwetu maziwa yamejaa then akazaa nkastuka usingizini

2)Ngombe kwa zizi letu wako wanne akatokea mmoja akazaa boma likajaa then mama angu akaniuliza huyu ndama aliezaliwa hakuna pakumweka mm nkamjibu tupunguze ngombe mmoja tumuze then nkastuka usingizini.

3) Nliota ngombe mzuri wakike maziwa yamejaa ana ngozi ya kuteleza anazaa ila akikua kipofu hua sielewi maana zake kwa ulimwengu wa roho

4) Juzi juzi nliota kua kuna mama mmoja(sikumfaham) alizaa mtoto wa kiume na mtoto yule akakua gafla na kuanza ktumbea pale pale. Naomba tafsiri yake mkuu
 
Mimi nimeota mwanamke niliyeachana nae ndio mpenzi wangu kwa kipindI hiki lakini ana mwanaume mwingine ikafikia kipindi akaniacha akapata nae mtoto je hii ina maana gani
 
Mimi nimeota mwanamke niliyeachana nae ndio mpenzi wangu kwa kipindI hiki lakini ana mwanaume mwingine ikafikia kipindi akaniacha akapata nae mtoto je hii ina maana gani
Ng'ombe huwa ni mwakilishi wa wanyama wote walao nyasi ,huwa kwenye bibilia hutamkwa kama ndama,kama umeota ng'ombe amenawiri basi unganisha jibu kwamba nyasi zitakua ni nyingi na kama nyasi ni nyingi basi ni kipindi cha neema,kwa hiyo utapitia kipindi cha neema lakini uwe na busara katika plan zako ,maana ni kwa mda tuu utapitia hicho kipindi ,kuzaliwa ndama kipofu codes zake no kuwa upofu =ulimwengu wa Giza ,hivyo ukipitia hicho kipindi cha neema omba sana maana itakupelekea kuangukia ulimwengu wa Giza .so mkuu piga goti na jichunge usije ukasombwa dhambini kipindi hicho
Kuhusu mama kuzaa mtoto akaanza kutembea,kwanza code ya mama na mtoto huwakilisha jamii au familiya hivyo kuna mambo ambayo utayashuhudia jamii au familia iliyokaribu nawe au inayokuzunguka ikikufanyia kinyume na unavyotarajia ,yaan hayaingii akilini ,pia yako kinyume na desturi ,sijui niwekeje ila ni kama kukuzushia ishu ambazo hazipo wala hukuwah kuwaza.
 
Inakuwaje story inaanza mwanzo mpaka inakamilika na wakati sii kweli?
 
Mimi nimeota mwanamke niliyeachana nae ndio mpenzi wangu kwa kipindI hiki lakini ana mwanaume mwingine ikafikia kipindi akaniacha akapata nae mtoto je hii ina maana gani
Hapo umeota usaliti,kiufupi kama huyo ex wako alikuaga na ugojwa flan unaoujua,au ndugu yake unayemjua ambaye alikua anaumwa ,basi itakua habari mbaya kwao.
 
Nashukuru sana mkuu,nikweli kuna baadhi ya matukio yameshanitokea katka ufafanuzi ulonipatia ila namshukuru Mungu nimeyashinda na sitachoka kumwomba Mungu japo napitia mitahani migumu sana, Ila ili dhahabu iwe bora zalima ipite kwenye moto. Barikiwa sana mkuu
 
niliota baba yangu mkubwa na babu yangu (wote ni marehemu) tulikua sehemu ambayo inaonekana ilikua ni nyumbani kwa ba mkubwa nikamwambia nataka kwenda shule (me ni mtu mzima saivi shule nlishamaliza mpaka chuo) akanambia nenda ndani sehemu fulaani utakuta hela chukua nenda shule kweli nikaenda nikachukua zile hela ila sikumbuki kama nlienda shule

ndoto nyingine nliota huyohuyo baba mkubwa ameacha familia yake na kwenda kusikojulikana na hakuna anaejua alipo/anafanya nini na roho ilikua inaniuma sana kumbe alienda kuanzisha maisha yake sehemu nyingine ila hakuoa mke mwingine na hakutaka mtu ajue yuko wapi na anafanya nn ila kumbe huko alikoenda alikua anaendelea na kazi yake ya ualimu na alikua anaishi mwenyewe tu hakutaka kujiusisha na mtu yaani kama alijitenga tu
 
Vipi na ndoto za kupanda milima Hadi juu, au kuota mlima mrefu na theluji yake?
 
Boss naitaj tafsiri hii pliz: usiku sa kuamkia leo nimeota nimesalitiwa. watu wangu ww mtaani kwetu nika amua kulipiza kisasi kwa wote walio nisaliti walikua 4 nikawasulubu then nika anza kuwadunga visu kila mmoja shingoni na kufariki... bada ya tukio hilo nika anza kutafutwa ili namimi niuliwe ila nikafanisha kutoroka jiji letu ambapo nilizaliwa nika elekea sehem mbali ambapo nika pokewa na askari wa2 waasi icho kijiji nimefika kulikuwepo vita ila mapigano yakawa yamesitishwa kwa kipindi ambacho nilikua huko na hivi karibuni kuliwahi kutoke mafuriko.....Mana ya ndoto hiyo nini nilipokua na tafutwa kwa kutukio ilibd mke wangu pia na yy akakusanye kila kitu chetu akashirikiana na mimi piaa!!! Nimeoa nina watoto2
 
H
Hiyo ndoto inamaanisha kuna tukio litampata mkeo ambalo litawaweka wote wawili kwenye wakat mgumu sana,hivyo piga magoti mkuu.
 
H

Hiyo ndoto inamaanisha kuna tukio litampata mkeo ambalo litawaweka wote wawili kwenye wakat mgumu sana,hivyo piga magoti mkuu.
Mungu akubariki kuna jambo tunapambana nalo mwaka sasa kabisa ila Kwa uwezo wa Mungu litakwishaa!! Na lina tu cost sote!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…