Siri usiyoijua kuhusu ndoto na tafsiri zake

Ndoto haihitaji tafsiri mnapoteza muda na kujazana ujinga.
 
Nilikua naota ng'ombe mwenye mapembe kama nyati ananikimbiza ule mwende wa tren ya mwendokasi.. ya umeme yan basi tu nikiamka sina hamu tena na usingizi.

Siku nyingine naota nikipaa juu halafu chini kuna majitaka yale ya kijani tii.

Naota niko hom mvua inanyesha kwetu tu maji yanaingia ndani yote.

Naota tena niko na rafiki zangu mahali tunafurahiya, nikatoka pale kuenda msalani kumbe kuna bonde refu nikatumbukia kule chini, wakati nikiwa kule chini mawe mazito yakaanza kuporomoka na hakuna mahali pa kutokea.
 
Nimeota Mdogo wangu alikua na matatizo kaandamwa na mikoani tukashauli aombewe badala yake yule Mchungaji akaanza kuniambea mimi nikakubali anscombe katikati ya maoni nikaanza kuwapiga mchungaji na wasaidizi wake nikawa kama mwehu hadi wakakosa nguvu
Dadayangu akaja ailipoona lile tukio akaomba waache kuniombea sababu niliwadharirisha wachungaji akaogopa wasije kunidhuru baada ya muda mfupi nikawa nimelala sifanyi chochote dadayangu akaanza kulia akahisi nimekufa
 
Ni takribani mwezi sasa naota tu mambo ya kufanya mitihani shuleni ama chuo ilhalia nishamalizaga mambo ya elimu.

Mara ya kwanza kwanza nliona kawaida ila daah imekua too much karibu kila siku naota eidha najiandaa na pepa( hapa nakua na hofu kichizi lakin nkishaingia kwenye pepa narelax), nafanya pepa ( nikiota hivi huwa nakua nimeconcetrate kwenye pepa na mara nyingi nakua sina hofu) , au nshamaliza pepa ( hapa napo huwa panantesa kwasababu huwa naanza kukumbuka nilichoandika ambacho sijaandika yani sijakiota ila pia sijui kumbukumbu inatokaga wapi ila nakua sawa kua nlichoandika kina usahihi kwa kiasi chake na marafiki wengine wameenda opp na hapa nakua washkaji tunajadili tulichoandika.
 
Msaada mara nyingi sana naota nakemea pepo,wachawi,..Yani nasali na kukemea ndotoni ..hii inamaana gani?
 


Tafsiri hizi ulizitoa biblia ipi ?? KJV, NKJV, AV, NIV, QJV, .........
 
Ni muda mrefu sasa huwa naota nipo darasani nafanya mtihani ilihali sijajiandaa na mtihani lakini kwenye matokeo huwa sifeli.
 
ukilala ubongo nao unalala kwa iyo ili usionekane umekufa kuna ubongo wa ziada una itwa oblongata una kua aujalala ndo una tuleteaga malue lue ya ndoto ukiamshwa tu wanyewe una lala ubongo orijino una anza kufanya kazi ndiomaana unaweza ota mengine usiyakumbuke nisawa na genereta automatic umeme ukikatika lina jizima ukirudi linajiwasha na ubongo orijino ukilala wenyewe una ijwasha ukiamka wenyewe una jizima hao wanasema wana tafsri ndoto waongo wapiga dili sana sana waganga wa kienyeji na wenye mizimu ndo wanatutishiaga hivyo na manabi wa uongo wachungaji vishoka ila unaweza ukaota kwa kubahatisha labuda umeota kuna mtu amekufa kesho una kuta amekufa kweli sio kwamba ndo mungu kakupa maono wala aiwezi kujirudia mara mbili ikawa kweli au ukajipangia kwamba kesho nitaota hivi
 
Mkuuu nimeota leo nipo shuleni kwetu niliposoma O level mara muda wa kunywa chai saa 4 nitoka na sahani kubwa imejaa mihogo ya kuchemsha ssa ni mingi sana nikakutana na wadada 2 nikawaambia njooo tule mihogo wakanibeza hatuli mikavu mie nikaanza kula mikavu nilikuwa na tu maji kidgo sana nikala mihogo kma kipande kdgo na maji yakaish du nikakutana na rafiki yangu simtaji jina
Nikamuambia mihogo mingi akasema njooo hapa wadau wengi nikaweka chini du hapo ndio nikastuka
JE MAAANA YAKE NINI?
 
Mkuuu kwa nni mie ndoto zangu nyingi nikiamka nazikumbuka je kuna nini hapo mkuuu????
 

Mimi Mara nyingi huwa naota naendesha gari, naota nakimbia tena kama mshale yaani nakimbia kama ni nguvu fulani ya mvutano unanivuta na pia huwa naota nipo darasani nafanya mtihani lakini Mara nyingi mitihani inakusanywa sijamaliza yaani napataga ugumu!! Sijui hizi ndoto zinakuwa na maana gani?
 
Dah mkuu mtarimbo hii ndoto nimeota mida ya saa kumi usiku leo. Nimeota mtu wa makamo yupo ndani ya gari anashuka darajani, sasa kabla hajavuka daraja tairi ya gari yake ikakwama kwenye kishimo akaamua kushuka aangalie. Alipokuwa ameinama wakatokea simba, wawili (majike) akawapiga risasi kwa bastora aliyokuwa nayo wakafa, likatokea simba dume kwa pembeni na kumrukia na kumwangusha chini na kumng'ata shingoni, mzee akaamua ajimalizie kwakujipiga risasi.
Mimi nipo kwa juu hivi kwenye muinuko nikilishuhudia lile tukio na kuamua kupanda juu ya mti. Ule mti ni mrefu una machache, wakati napanda juu nikaangalia chini na kumuona simba jike pale chini akiniangalia. Kwa presha niliyokuwa nayo nikaparamia tawi jembamba, kumbe lilikuwa likibend chini mimi nikiparamia kwenda juu, kutahamaki nipo karibia na chini nikamkanyaga yule simba jike kichwani ili nigain momentum ya kurudi juu. Wakati narudi juu nikarukiwa na simba dume hata sijui alikuwa kwa wapi, maumivu niliyosikia nilitamani nife tu.
Sielewi inamaanisha nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…