Muanzisha topic amepewa heshima ati ni verified user, what stupidity is this?
Ally Kombo, Ritz na Wanamajlis,
Jamaa wengi wametaka kujua nini kilitokea baada ya safari ya
Nyerere UNO.
Kwa heshima yao naongeza kitu kidogo ili kukamilisha historia hii muhimu ingawa mimi naamini somo limeeleweka. Hapa chini ndipo nilipomalizia safari ya Nyerere UNO 1955:
Siku iliyofuata ilikuwa Jumapili. TANU ilifanya mkutano wa hadhara Mnazi Mmoja ambao ulihudhuriwa na umati ambao kamwe haukupata kuonekana Dar es Salaam. Inakisiwa zaidi ya watu 40,000 walikuja kutoka kila upande wa mji kumsikiliza Nyerere. Hakuna mtu aliyekuwa na raha ya kuandika kuhusu mkutano ule na safari ya kihistoria ya
Nyerere kwenda Umoja wa Mataifa kuliko
Mashado Plantan katika gazeti lake Zuhra. Mtambo wa gazeti wa
Mashado Plantan uliokuwa Mtaa wa Ndanda, Mission Quarters ulichapisha nakala za ziada za gazeti hilo na toleo lote liliuzika."
Mashado Plantan inaaminika ndiyo mwandishi wa kwanza kumwandika
Nyerere katika gazeti
lake la Zuhra akimtambulisha kwa wananchi kama ndiyo kiongozi mkuu wa TANU. Hii ilikuwa Agosti 1954 baada ya mkutano wa kwanza wa TANU pale Arnautoglo Hall. (Nakala za gazeti hili zinapatikana Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East Africana).
Baada ya mapokezi yale ya
Nyerere na mwamko mpya uliogubika Tanganyika, Waingereza walijua kuwa siku zao zilikuwa zinahesabika.
Father Walsh alimwambia
Nyerere achague siasa au kazi ya ualimu. Kwa muda mrefu
Abdul Sykes alikuwa akimwambia
Nyerere ajiuzulu kazi na ashughulike na TANU lakini
Nyerere alikuwa bado hajaamua.
Baada ya kuelezwa hivyo na kuandikiwa barua rasmi
Nyerere aliichukua barua ile hadi kwa
Mzee Mtamila ambae ndiye alikuwa rais wa TANU na
Mzee Mtamila akaitisha mkutano wa Halmashauri Kuu na ile barua ikasomwa mbele yao.
Uamuzi uliofikiwa ulikuwa
Nyerere na ajiuzulu na TANU itakuwa nyuma yake kwa hali na mali. Kati ya wajumbe wa Halmashauri Kuu walikuwa
John Rupia, Bi Titi Mohamed na
Bi. Tatu biti Mzee. Mkutano huu muhimu katika historia ya
Nyerere ulifanyika nyumbani kwa
Mzee Mtamila Mtaa wa Kipata na Sikukuu. Nyumba hii ilikuwa kwenye kona. Hivi sasa nyumba ile haipo tena imejengwa ghorofa.
Nyerere alijiuzulu ualimu na siku alipokuja mjini kutoka Pugu na basi la Majigo (basi hili lilipewa jina Majigo kwa kuwa mwenye basi lile alikuwa Muhindi ambae abiria akipanda anamnadia kwa kusema, Majigo juu, majigo juu. Yaani mzigo juu, mzigo juu)
Nyerere moja kwa moja alikwenda ofisini kwa
Abdul Sykes Kariakoo Market si mwalimu tena. Kituo cha basi la Majigo kilikuwa Mtaa wa Msimbazi na Agrrey.
Nyerere alikaa nyumbani kwa
Abdul Sykes na mkewe Bi.
Mwamvua Mtaa wa Aggrey na Sikukuu kwa muda hadi TANU ilipompatia nyumba Magomeni.
Hapa ndipo katika nyumba ile miaka michache nyuma
Abdul alijitahidi sana kumshawishi
Chief David Kidaha Makwaia ajitoe alikokuwa aje TAA wamchague kuwa rais na kisha waunde TANU na yeye atakuwa rais wadai uhuru na ukipatikana yeye
Chief Kidaha atakuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika.
Hii ndiyo historia ya TANU niijuayo mimi na nimeiandika katika kitabu cha
Abdul Sykes (1998) kwa ajili ya kizazi kijacho.
Naamini ni baada ya kuandika historia hii ndipo katika kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru viongozi wetu waliamua kumtunuku
Abdul Sykes medali pamoja na mdogo wake
Ally.