Elections 2010 Siri ya Mshahara wa Rais na Marupurupu ya Rais Wastaafu...

Elections 2010 Siri ya Mshahara wa Rais na Marupurupu ya Rais Wastaafu...

Kama mishahara ya Spika wa Bunge, Jaji na wengineo ni kama hivi. Je Raisi itakuwa ngapi?

Hebu tupitie kidogo post hii hapa

MSHAHARA WA SPIKA, JAJI MKUU WAONGEZWA MARADUFU

Waandishi Wetu

SERIKALI imewaongezea mishahara viongozi wa kisiasa, majaji, wakuu wa mikoa na wilaya kuanzia Julai mwaka huu, huku jaji mkuu na spika wakiongezewa maradufu.


Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa mshahara wa jaji mkuu na spika, ambao ni viongozi wa mihimili mikuu miwili ya nchi, umepanda kutoka Sh2,760,000 hadi Sh4,850,000 kuanzia mwezi Julai na ongezeko hilo ni sawa na asilimia 75.7


Kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na vyanzo mbalimbali vya habari kutoka mihimili yote ya dola, mshahara wa naibu spika umepanda kwa Sh92,000, kutoka Sh2,080,000 hadi Sh2,172,000 na mbunge kutoka Sh1,840,000 hadi Sh1,921,000, ikiwa ni ongezeko la Sh81,000 kwa mwezi.


Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah aliliambia gazeti hili mwishoni mwa wiki kuwa amesikia kuhusu nyongeza hiyo ya mishahara, lakini hana taarifa rasmi wala namna yoyote ya kuthibitisha, kwa kuwa mishahara hiyo haimuhusu.


"Viwango vya mishahara kwa viongozi wa serikali vinawekwa na serikali, mimi hainihusu hivyo siwezi kuthibitisha hilo. Nimesikia tu kama mlivyosikia ninyi," alisema Dk Kashilillah alipotakiwa na gazeti hili kuthibitisha ongezeko la mishahara ya wabunge.


Katika viwango hivyo vipya vya mishahara ambavyo Mwananchi imefanikiwa kuviona, jaji wa Mahakama Kuu ameongezewa mshahara kutoka Sh2,160,000 hadi Sh3,645,000, ikiwa ni ongezeko la Sh1,485,000 huku jaji wa Mahakama ya Rufaa ameongezewa Sh1,940,000 (kutoka Sh2,310,000 hadi Sh4,250,000).


Vyanzo vimeeleza kuwa mshahara wa waziri umepanda kwa Sh102,000 (kutoka Sh2,320,000 hadi Sh2,422,000) na mshahara wa naibu waziri umepanda kutoka Sh1,960,000 hadi Sh2,046,000, ikiwa ni ongezeko la Sh120,000.


Mkuu wa mkoa, ambaye anapata mshahara wa Sh2,172,000, sasa atalipwa Sh2,080,000 na mkuu wa wilaya amepandishiwa mshahara wake kutoka Sh1,840,000 hadi Sh1,921,000 kwa mwezi.


Vyanzo hivyo vya habari vimedokeza kuwa viwango hivyo vipya vya mishahara, havijumuishi posho za vikao, mafuta ya gari na fedha za kujikimu.


Habari zinaeleza kuwa jaji mkuu anapata posho ya madaraka ya Sh6 milioni kwa mwaka na jaji kiongozi anapata posho ya Sh3 milioni, kwa mujibu wa viwango hivyo vipya.


Majaji 70 wanapata posho ya simu na umeme inayofikia Sh 386,400,000 kwa mwaka na posho ya mavazi ya Sh35 milioni kila mmoja.


Habari zinadokeza kuwa majaji 70 wametengewa lita 100 za mafuta ya gari kwa juma, lita moja imekadiriwa kugharimu Sh1,500 hivyo kupewa Sh600,000 kwa wiki ambayo ni sawa na Sh504 milioni kwa mwaka.


Moja ya vyanzo vyetu vya habari kilidokeza kuwa nyongeza hiyo ni ya kawaida ambayo inaenda sambamba na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma, ingawa mwaka huu kwake imeonekana kuwa kubwa zaidi.


"Hili ni kweli; mishahara yetu imeongezwa kuanzia Julai, lakini sisi tulidhani ni nyongeza ya kawaida inayoenda sambamba na nyongeza ya mishahara ya watumishi wengine wa umma, lakini ukweli mambo ni mazuri zaidi," alisema.


Akiwasilisha hotuba yake kwa mwaka 2000/2010, waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma, Hawa Ghasia alisema serikali inatarajia kutumia Sh1,774 trilioni kugharamia mishahara kwa watumishi wa umma,


Fedha hizo pia zitatumika kulipa mishahara kwa watumishi waliopo kazini, ajira mpya, upandishaji vyeo watumishi, kulipia madai ya malimbikizo na mapunjo ya mishahara ya watumishi wa umma nchini.


"Serikali itaendelea kuhakikisha watumishi wake wanapandishwa vyeo na kurekebishiwa mishahara yao ipasavyo," alisema Waziri Ghasia wakati akiwasilisha makadirio ya wizara ambayo wabunge waliyapitisha bila marekebisho.


Suala la mishahara hiyo mipya limekuwa siri kubwa hasa ikizingatiwa kuwa wakati wa bajeti ya serikali ya mwaka huu, waziri mwenye dhamana hakuweka bayana viwango vipya vya mishahara ya watumishi wa umma.


Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili zilisema kuwa serikali hivi sasa iko katika mkakati muhimu wa kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wenye taalumu ili kuzima wimbi la wasomi kukimbilia nyadhifa za kisiasa.


"Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia madaktari na wanataaluma wengine wanaacha taaluma zao wanakimbilia ubunge kwa sababu anaona labda atateuliwa kuwa waziri na maslahi ni mazuri,¡"kilidokeza chanzo chetu cha habari.


Source: Mwananchi Date:8/25/2009
 
1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania = ?

2. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania= ?

3. Rais wa Zanzibar = ?

4. Waziri Mkuu = ?

5. Katibu Mkuu Kiongozi =?

6. Mawaziri = Sh2,422,000

7. Manaibu waziri =Sh2,046,000

8. Makatibu Wakuu =?

9. Wakuu wa Mikoa =Sh2,080,000

10. Wakuu wa Wilaya =Sh1,921,000

11. Wabunge =Sh1,921,000

Haya sasa piga hesabu mwenyewe Tanzania ina mikoa 26 x 2,080,000
Idadi ya Wilaya x 1,921,000 halafu bado mawaziri, wabunge na wengineo wengi ambao sijapata data. Ukijumlisha yote hayo utapata sh. ngapi???????
Bado idadi ya wabunge n.k. yaani ni hela nyingi sana.
 
1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania = ?

2. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania= ?

3. Rais wa Zanzibar = ?

4. Waziri Mkuu = ?

5. Katibu Mkuu Kiongozi =?

6. Mawaziri = Sh2,422,000

7. Manaibu waziri =Sh2,046,000

8. Makatibu Wakuu =?

9. Wakuu wa Mikoa =Sh2,080,000

10. Wakuu wa Wilaya =Sh1,921,000

11. Wabunge =Sh1,921,000

Haya sasa piga hesabu mwenyewe Tanzania ina mikoa 26 x 2,080,000
Idadi ya Wilaya x 1,921,000 halafu bado mawaziri, wabunge na wengineo wengi ambao sijapata data. Ukijumlisha yote hayo utapata sh. ngapi???????
Bado idadi ya wabunge n.k. yaani ni hela nyingi sana.
Viongozi wa nchi yetu na wawakilishi wa wananchi wote ni wabinafsi wa hali juu ktk Nchi yetu.

Hakuna uwiano hata kidogo wa kimshahara.Fikiria watumishi wa umma kima chao cha chini ni mara asilimia 4000 zaidi ya mshahara wa spika na majaji na mara asilimia 2000 zaidi kwa wakuu wa mikoa na pengine ni mara asilimia zaidi ya 8000 kwa Rais.Na bado Rais anatoka hadharani kuona madai ya wafanyakazi hayatekelezeki lkn ya kwao yanatekelezeka. Kumbuka bado wana marupurupu kibao na mtu wa kima cha chini hana.

Kwanini wasiangalie upya viwango vya mishahara yao wakavipunguza na watakachosave huko waongeze kwenye kima cha chini kikidhi angalau mahitaji muhimu hasa ukizingatia kwamba wanadai nchi ina hali ngumu badala ya kutoka hadharani kuwatukana watumishi wa umma ambao wanaona kila siku wakinyonywa nao kupitia mgao dhaifu wa keki ya Taifa!

What a jokes?
 
Utashangaa kesho watu wataandamana sehemu mbalimbali kuunga mkono "hotuba ya kihistoria ya rais aliyoitoa kwenye kumbi wa Diamond Jubilee Mei 04, 2010"
 
Utashangaa kesho watu wataandamana sehemu mbalimbali kuunga mkono "hotuba ya kihistoria ya rais aliyoitoa kwenye kumbi wa Diamond Jubilee Mei 04, 2010"
Watakao andamana ni wale wanaounga mkono Chama cha CCM sio Wananchi wote kaka Waandamanaji ni Wafuasi watiifu wa CCM Sio Walala hoi mkuu.
 
Barack Obama

⇒ Annual salary*: $ 400,000
shadow-banner.png

Since you arrived on this page at 2:35 a.m. Barack Obama earned: 2 dollars 65,63 cents

2 dollars 65,63 cents
transparent.gif
2.jpg
0.5.jpg
0.05.jpg
0.03.jpg



Barack Obama's salary:
daily.png
hourly.png
minutely.png
secondly.png
1666 dollars 66 cents 208 dollars 33 cents 3 dollars 47 cents 5 cents
transparent.gif
1000.jpg
600.jpg
50.jpg
10.jpg
5.jpg
1.jpg
0.5.jpg
0.1.jpg
0.05.jpg
0.01.jpg
transparent.gif
200.jpg
5.jpg
2.jpg
1.jpg
0.25.jpg
0.05.jpg
0.03.jpg
transparent.gif
2.jpg
1.jpg
0.25.jpg
0.2.jpg
0.02.jpg
transparent.gif
0.05.jpg

http://www.salary-money.com/barack-obama-salary-400000.php
 
Government-TUCTA dispute needs patience, understanding
04_10_re6egm.jpg
TRADE Union leaders attend one of their meetings. Left is TUCTA acting Secretary General Nicholaus Mgaya. (File Photo)

NATIONWIDE strikes not only paralyze the national economy, but also cause lots of inconveniences to the general public at large.

Try to imagine, what will happen if doctors, nurses and other medical practitioners, for instance, embarks on an endless nationwide strike. Such kind of events are not only nuisance to the population, but the worst part of it is that they end up punishing the wrong people who may not even be aware of factors that led to the incident.

Just a few weeks ago, Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA) officials publicly asserted that the union has dedicated the International Labour Day on May 1st to mobilizing all workers in the country to stage an infinite countrywide strike starting on 5th May.

The threat to lay down tools follows what TUCTA officials described as ‘the government failure’ to respond to a 90-day notice issued by the trade union to meet the workers’ longtime demands. TUCTA, established in 2000, is a new umbrella organization for trade unions in Tanzania, and it has a total membership of approximately of over 370,000.

The union President, Mr Ayoub Omary Juma, was quoted by the local media as saying TUCTA will definitely go on strike unless the government meets their demands before 5th May this year. The demands, he said, include, salary increment, a need to review the current social security schemes, and that of reduction of 'pay as you earn' (PAYE) deductions .

The trade union, for example, passionately claims that the current social security scheme does not meet the needs of the beneficiaries (retirees), and therefore the union wants pension benefits issued by the Pension Provident Fund (PPF), Public Service Pension Fund (PSPF) and the Local Authorities Pension Fund (LAPF) improved.

In another demand Mr Juma said: “The Government determines the salary increments without involving trade unions which contravenes the law, since we cannot take the government to court, we have resorted to strike to express our grievances."

The union proposes minimum salary of 315,000/-, and one TUCTA official said: “The Government determines salary increments without involving trade unions, and this arbitrary move contravenes the law of the land, and since we cannot take the government to court, we have no option but to strike," he added.


A few weeks ago, TUCTA acting Secretary General Nicholaus Mgaya, told a news conference in Dar es Salaam that the May Day celebrations will be graced by TUCTA president and not any of the country's top political leaders.

"For the first time, we shall not invite the head of state and other top government leaders as the guests of honour to our event as an expression of workers’ disappointment,” said the Secretary General.

The secretary general went further as saying the Trade Union Congress of Tanzania, a union of 17 trade unions has already formed a ten-man committee to co-ordinate the planned countrywide strike.

In its response, the government has shown positive attitude toward finding amicable solution to the problem stressing the need to solve it through negotiations. This has taken president Jakaya Kikwete to appeal cogently to the trade union officials to pursue negotiations instead of resorting to a general strike.

In his monthly address (March this year) to the nation, Mr Kikwete clearly stated that a decision to go on strike would not be conducive to the general public as it will only ‘yield negative results’.

Thus the head of state called upon the parties to establish a common ground that will be of the benefit to workers and the nation at large. Politicians, academicians and other members of the public have appreciated the presidents’ use of genius and common sense to find amicable solution.

It was of course the opposite to the thinking of other people who would have erroneously expected the president to issue warning, threat or any form of intimidation to the trade union.

Mr Mgaya has even appreciated the government approach to dealing with the problem saying: “We are very happy that president Kikwete has shown concern over this delicate issue and we have received his call for more discussions,” Mr Mgaya told reporters.

Talks between government and trade union representatives are now underway, and they are being facilitated by the Labour, Economic and Social Council (LESCO) and the Commission for Mediation and Arbitration (CMA). Officials say that progress is being made through the negotiation table which has brought together all key players.

The Minister for Labour, Employment and Youth Development, Mr Juma Kapuya, says the government has been striving to review the PAYE as saying the deductions from the workers’ salaries had been reduced from 18.5 per cent to 15 per cent, and taxable pay raised from 80,000/- to 100,000/- .

The parties have been meeting in several times in trying to reach a common deal. On 6th April this year, for instance, the parties jointly agreed that TUCTA officials, through Public Service Joint Staff Council, have to submit their proposal on tax reform to be discussed by relevant government organs.

Not each and every agreement must be made in public, but a good thing is that the negotiations are taking place, and the general public is optimistic that the parties, government, TUCTA, LESCO and CMA will continue to play a decisive role with a target of yielding positive results.

It is also important for other key players such as politicians, NGOs, media practitioners and others to refrain from inflammatory or derogatory remarks that may end up fuelling the dispute rather than solving it.

http://www.dailynews.co.tz/feature/?n=9311&cat=feature
 
Hii nchi inaendeshwe kisenge senge sana. Yaani mpaka leo hatujui mshahara wa raisi ni kiasi gani. Huu mshahara si unatokana na kodi za wananchi au?

Kuna haja hii iwe ni issue katika uchaguzi ujao. Je Rais anapata mshahara na marupurupu kiasi gani kwa mwezi?? Na analipa kodi kiasi gani kwa mwezi? Mawaziri nao na Wabunge wanapata mshahara na marupurupu kiasi gani kwa mwezi na wanalipa kiasi gani kama kodi halafu tulinganishe na kima cha chini wanacholipwa wanyonge. Je, kodi inayolipwa na hawa waheshimiwa ni asilimia ngapi ya mishahara yao na marupurupu combined? Haiwezekani kabisa sisi kama walipa kodi ambao ndiyo tunalipa mishahara ya hawa watu tusiijue mishahara yao? Na ni sababu zipi zinafanya mishahara yao na marupurupu kufanywa ni siri kubwa? wanaficha nini hasa?
 
Viongozi wa nchi yetu na wawakilishi wa wananchi wote ni wabinafsi wa hali juu ktk Nchi yetu.Hakuna uwiano hata kidogo wa kimshahara.Fikiria watumishi wa umma kima chao cha chini ni mara asilimia 4000 zaidi ya mshahara wa spika na majaji na mara asilimia 2000 zaidi kwa wakuu wa mikoa na pengine ni mara asilimia zaidi ya 8000 kwa Rais.Na bado Rais anatoka hadharani kuona madai ya wafanyakazi hayatekelezeki lkn ya kwao yanatekelezeka. Kumbuka bado wana marupurupu kibao na mtu wa kima cha chini hana .kwanini wasiangalie upya viwango vya mishahara yao wakavipunguza na watakachosave huko waongeze kwenye kima cha chini kikidhi angalau mahitaji muhimu hasa ukizingatia kwamba wanadai nchi ina hali ngumu badala ya kutoka hadharani kuwatukana watumishi wa umma ambao wanaona kila siku wakinyonywa nao kupitia mgao dhaifu wa keki ya Taifa!What a jokes?

Halafu Kikwete anatwambia nchi ni maskini!!!! Wakati mishahara yao ni sawa kabisa na mishahara ya nchi tajiri duniani!!! Enzi za Nyerere mshahara wake haukuwa na tofauti kubwa kiasi hiki. Wakati wamepandisha mishahara yao kwa kasi na kiasi kikubwa sana lakini ile ya Wafanyakazi haikupandishwa kabisa au imepanda kwa kiasi kidogo sana.
 
Mtu anajisifu kaongeza Mshahara toka 65,000 hadi 104,000. Hivi kweli unadiriki kujisifia mshahara wa namna hiyo!!!
Siamini.

Mshahara wa 65,000 ulikuwa mwaka gani na je wame-calculate inflation rate? siyo kutupatia data za ajabu ajabu - inawezekana hata hizo 65,000 by then zilikuwa zinasaidia - fake calculations!
 
1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania = ?

2. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania= ?

3. Rais wa Zanzibar = ?

4. Waziri Mkuu = ?

5. Katibu Mkuu Kiongozi =?

6. Mawaziri = Sh2,422,000

7. Manaibu waziri =Sh2,046,000

8. Makatibu Wakuu =?

9. Wakuu wa Mikoa =Sh2,080,000

10. Wakuu wa Wilaya =Sh1,921,000

11. Wabunge =Sh1,921,000

Haya sasa piga hesabu mwenyewe Tanzania ina mikoa 26 x 2,080,000
Idadi ya Wilaya x 1,921,000 halafu bado mawaziri, wabunge na wengineo wengi ambao sijapata data. Ukijumlisha yote hayo utapata sh. ngapi???????
Bado idadi ya wabunge n.k. yaani ni hela nyingi sana.

Mkuu these guys salaries zao huwa ni Pure savings! sidhani katika list yako kuna mtu anategemea mwisho wa mwezi - akishika postion hiyo lets say kwa ten years ina maana ana mishahara 10 times 12 = 120 months SAVINGS - Sasa atafikiriaje mtanzania kwenye njaa kali? na hayo marupurupu ya pembeni ambayo ni makubwa kuliko huo mshahara yote ni pesa za kodi zetu.

Sina tatizo na mishahara yao lakini lazima hizi pesa wazifanyie kazi - watekeleze majukumu kama viongozi wetu - Bado TUCTA wana hoja za msingi ambazo serikali inajiumauma tu sijaona jibu kamili.
 
Plato told Aristotle no one should make more than five times the pay of the lowest member of society. J.P. Morgan said 20 times. Jesus advocated a negative differential -- that's why they killed him.
Rais amejisifu kuwa serikali yake imeongeza kima cha chini kwa zaidi ya 60% mpaka kufikia 104,000/-. Tukichukulia mfano wa mwana JF mmoja kuwa mshahara wa Rais ni 9,000,000/-, ina maana kuwa itamchukua mfanyakazi wa serikali wa kima cha chini zaidi ya MIAKA SABA (7) ili kufikia mshahara wa Rais wa mwezi mmoja tu! Binafsi nina amini kuwa mshahara wa Rais ni zaidi ya 9m/- kwa mwezi. Pia huwa Rais hagusi mshahara wake kwa vile kamwe halipi rent, hanunui chakula wala mavazi, halipi bili ya umeme, maji, wala kuweka mafuta kwenye gari na hulipwa poshi nyingi sana na marupurupu lukuki.
Je, Rais kweli ana moral authority kusema 315,000/- ni pesa mingi sana wakati mshahara wake yeye mwenyewe ni SIRI?

WAANDISHI WA HABARI fanyeni kazi yenu. Mtege waziri wa utumishi, waziri wa kazi, waziri wa utawala bora, msemaji wa ikulu, katibu mkuu kiongozi, waziri wa habari au JK mwenyewe kwa kuuliza mshahara wa Rais ni shilingi ngapi? Lazima watakwepa kusema ukweli na hapo iandikwe habari kuwa wakati serikali imekataa nyongeza ya mshahara wa kima cha chini, inafanya siri mshahara wa Rais. Hivi hata Mgaya mwenyewe anajua mshahara wa Rais ni kiasi gani?

JK angekuwa na busara za uongozi angetangaza kupunguza mshahara wake yeye binafsi na wa vigogo wengine wakuu serikalini. Hii isingeathiri kipato chake hata kidogo ila ingempa political capital kubwa sana kwenye mgogoro wake na TUCTA. Ni mtazamo wangu tu!
 
Ni wazi mwenye shibe hamjui mwenye njaa!

Tatizo ni kwamba mtu anayepata mshahara wa juu na malupulupu mengi anafikiria kuwa wanaopata mshahara kidogo unawatosha. Na ikumbe kuwa kulikuwa wimbo wa maisha bora kwa kila Mtanzania ifikapo 2010. Lakini siku hizi wimbo huu hausikiki tena.

Serikali yetu huwa naifananisha sawa na mtu mwenye 'kakichwa kadodo', 'limdogo likubwa', 'vimacho vidogo' na 'vimasikio vidogo'. Ikiwa na maana kuwa kufikiri/ubunifu kidogo sana, maneno mengi, kuona mbali kidogo sana na kusikiliza matatizo/ushauri mzuri kidogo sana pia.

Kwa hali hii maendeleo yanakuwa magumu sana!
 
SWALI LA KIZUSHI: Mnyalu Lukuvi analipwa mshahara upi? wa mbunge? au mkuu wa mkoa?
 
Viongozi wasiri wanao ogopa hata kutaja mishahara yao hawatufai,
kwani wao ndio wezi namba moja.
Tusiwachague waficha makucha, tunataka transparency
 
Hawa jamaa wanalipwa mishahara mikubwa, wanapewa nyumba full furnished (samani zinabadilishwa kila mwaka) bure, wanalipwa posho ya chakula milo yote (asubuhi, jioni na usiku) kila siku kwa familia yake yote. Anaousafiri limos, ulinzi kila mahali nk. Anaposho ya kazi kila siku, anasafari 2/3 ya mwezi za nje na ndani. Anapoenda nje ya nchi analipwa outfit allowance (pamba nyepesi) perdiem za nguvu. Kwa hiyo hata huo mshahara wake hauna matumizi.

Nemesis ni mkweli kuwa ukiangalia tu mishahara (basic salaries) ya Rais na hao viongozi wengine walioorodheshwa hautapata picha halisi ya kipato wanachopata kutokana na kazi zao (income from employment). Ukweli ni kuwa mishahara yao ni sehemu ndogo sana ya kipato chao. Ili upate picha halisi angalia allowances zifuatazo:-

1. Subsistence Allowance
2. Disturbance Allowance
3. Entertainment Allowance
4. Acting Allowance
5. Special Duty Allowance
6. Outfit Allowance
7. Furniture Allowance
8. Overtime Allowance
9. Lunch Allowance
10. Responsibility Allowance
11. Transport Allowance
12. Fuel Allowance
13. Sitting Allowance
14. Housing Allowance
15. Allowance for incidental expenses on journeys
16. Training Allowance
17. Perdiem Allowance
18. Presentation Allowance
19. HonorariaUtility Allowance
20. Mileage Allowance
 
Nemesis ni mkweli kuwa ukiangalia tu mishahara (basic salaries) ya Rais na hao viongozi wengine walioorodheshwa hautapata picha halisi ya kipato wanachopata kutokana na kazi zao (income from employment). Ukweli ni kuwa mishahara yao ni sehemu ndogo sana ya kipato chao. Ili upate picha halisi angalia allowances zifuatazo:-

1. Subsistence Allowance
2. Disturbance Allowance
3. Entertainment Allowance
4. Acting Allowance
5. Special Duty Allowance
6. Outfit Allowance
7. Furniture Allowance
8. Overtime Allowance
9. Lunch Allowance
10. Responsibility Allowance
11. Transport Allowance
12. Fuel Allowance
13. Sitting Allowance
14. Housing Allowance
15. Allowance for incidental expenses on journeys
16. Training Allowance
17. Perdiem Allowance
18. Presentation Allowance
19. HonorariaUtility Allowance
20. Mileage Allowance

Duu!! Mkuu hii orodha inatisha, no wonder mkulu anawaona wafanyakazi kama sisimizi, hapa lazima mtu ulewe madaraka si bure!
 
Hii nchi inaendeshwe kisenge senge sana. Yaani mpaka leo hatujui mshahara wa raisi ni kiasi gani. Huu mshahara si unatokana na kodi za wananchi au?

Mkuu taratibu hapo penye red nikisikia najua mtu ameshapiga vi castle lite then akazingulliwa na jambo ...
 
Duu!! Mkuu hii orodha inatisha, no wonder mkulu anawaona wafanyakazi kama sisimizi, hapa lazima mtu ulewe madaraka si bure!

Dah kama ningekuwa Nyerere namba mbili(2),ningepunguza allowance za kipumbavu hapa! Ala!
 
Niliwahi kusikia eti mshahara wa Mkuru ni TZS. 780 milioni p.a. excluding travel & meeting allowances!!
 
Back
Top Bottom