Siri ya Pinda kuongezwa kwenye ‘Kikosi Kazi’ ni wajumbe kuelemewa na hoja ya Katiba Mpya

Ni wepesi mno hao wanaopinga Katiba mpya, Kodi za Wananchi ifike Mahali ziheshimiwe. Amen
 
Marekebisho yoyote ya Katiba yafanyike kwa kutumia Ile Katiba pendwa ya Warioba,maana ndo yalikuwa maoni halisi ya WENYE NCHI YAO(WANANCHI).Ile Katiba ya Hayati SITA Ichomwe Moto maana ilikuwa Ni kejeli kwa watanzania
Mkwawa masawe has spoken..

Na mimi nakazia tu..mchakato uanzie kwenye rasimu ya Warioba kwa kufanya some few adjustments.
 
WAKUU

Nina wasiwasi Sana!

Hivi wanachama wenzangu wa ccm Huwa wanasoma makala,vitabu kweli!!?

Kama ni wasomi wasingethubutu kabisa kuchezea mchakato wa KATIBA!!

HAWAONI,hawasomi alama za NYAKATI!!?


Pole yao!!
 
Katika mawaziri wakuu ambao naonaga kabisa wanakula hela ya bure, hawakuwahi kufanya jambo lolote la kukumbukwa nchini nadhani huyu jamaa anaongoza; hata nikiilazimisha AKILI yangu imkumbuke kwa LIPI, sipati hata moja yaani.
 
Kumbukumbu niliyonayo ya kumkumbuka Pinda ni Lile la albino kuuwawa alivyomwa machozi baba wa watu.

Mwache atatoa Tena machozi. Hawajui vijana walivyo na usingo wa maisha.

Akae atulie ale pension yake.
Pinda hayupo serious hata kidogo
 
Mizengwe, Pinda.
 
Mbona kama huyu Mzee ni kama wamemsusha sana? Mtu aliyewahi kiwa Waziri Mkuu wa Nchi inakuwaje anakuwa mjumbe wa kawaida kwenye kikosi kazi hiki? Yaani sasa anapokea maelekezo kutoka kwa Prof. Mukandala!
Sijui watu wa itifaki wanasemaje katika hili. Mimi kwa ufahamu wangu mdogo katika mambo haya naona haijakaa sawa.
 
Mkuu
Inategemea hekima katika nini!!

Je hekima ya kuchelewesha mchakato Ili ccm ishinde uchaguzi ujao?au hekima ya kuharakisha mchakato Ili wananchi wapate haki yao!!!


TUSUBIRI
Katiba mpya ndiyo itakufanya ushinde uchaguzi?
 
Katiba mpya ndiyo itakufanya ushinde uchaguzi?
Itasaidia wananchi kuwawajibisha VIONGOZI wao wanapotumia madaraka yao vibaya!!ushindi wa uchaguzi ni matakwa ya wananchi TU na matakwa hayo yataheshimiwa bila kuchakachua kura zao!!!!
 
Moja wapo ni Zitto Kabwe anataka katiba isubiri 2025
Ameshabadilisha Gia angani kimya kimya. Msaka fursa yule hawezi kukaa upande usipmpa sifa. Alipoona CHADEMA wanapata sifa na yeye akajifanya watu hawakumuelewa. Soma maoni ya chama chake utaona alivyonadilika na yeye anataka Katiba mpya kabla ya 2025.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Yule ni dalali wa kisiasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…