Siri ya Pinda kuongezwa kwenye ‘Kikosi Kazi’ ni wajumbe kuelemewa na hoja ya Katiba Mpya

Siri ya Pinda kuongezwa kwenye ‘Kikosi Kazi’ ni wajumbe kuelemewa na hoja ya Katiba Mpya

Tuongezeee!!!!

Wamachinga jeeeee? Watakuwemo humo humo?

Bodaboda ndiyo kabisa. Mfano yafanyike maandamano ya amani kila mkoa au wilaya kutaka Katiba Mpya, serikali hawataamini huo umati wa watu. Watajua kweli hii nchi wanaendesha kwa ubabe.

Wafanyakazi nao wanakazia Katiba mpya.

Wagongwa mahospital wanapiga magoti kuomba Katiba mpya.

Madalali msiwahesabie hawa ndio watu wao. Hawa wapo kwa kazi maalumu. Ndiyo maana wanajiamini Kama Usalama wa Taifa.

CCM Kama wako vizuri na raia si waruhusu mcakato wa Katiba mpya ya Warioba uendelee ili wananchi wawachague chama zilipendwa?
Ni wepesi mno hao wanaopinga Katiba mpya, Kodi za Wananchi ifike Mahali ziheshimiwe. Amen
 
Marekebisho yoyote ya Katiba yafanyike kwa kutumia Ile Katiba pendwa ya Warioba,maana ndo yalikuwa maoni halisi ya WENYE NCHI YAO(WANANCHI).Ile Katiba ya Hayati SITA Ichomwe Moto maana ilikuwa Ni kejeli kwa watanzania
Mkwawa masawe has spoken..

Na mimi nakazia tu..mchakato uanzie kwenye rasimu ya Warioba kwa kufanya some few adjustments.
 
WAKUU

Nina wasiwasi Sana!

Hivi wanachama wenzangu wa ccm Huwa wanasoma makala,vitabu kweli!!?

Kama ni wasomi wasingethubutu kabisa kuchezea mchakato wa KATIBA!!

HAWAONI,hawasomi alama za NYAKATI!!?


Pole yao!!
 
Kumbukumbu niliyonayo ya kumkumbuka Pinda ni Lile la albino kuuwawa alivyomwa machozi baba wa watu.

Mwache atatoa Tena machozi. Hawajui vijana walivyo na usingo wa maisha.

Akae atulie ale pension yake.
Pinda hayupo serious hata kidogo
 
Kazi kubwa ya Kikosi Kazi cha Rais ni kupata maoni kuhusu kudorora kwa Hali ya Demokrasia nchini lkn yenyewe imejikita zaidi kwenye upatikanaji wa Katiba Mpya.

Baada ya Kikosi Kazi kupendekeza katiba isubiri hadi 2025 wajumbe waligawanyika kuna wanaotaka mchakato uanze sasa na kuna wanaosema usubiri.

Pamoja na hayo maoni mengi ya wadau wanaohojiwa na Kikosi Kazi yanapendekeza kuanza mapema kwa mchakato wa Katiba, wanadai kama hoja ni muda au gharama waendelee ilipoishia Tume ya Warioba, hoja ambayo wanaotaka katiba isubiri wameshindwa kuijibu.

“Kuna wakati Kikosi Kazi huwa kinaelemewa na hoja za wanaokuja kutoka maoni hivyo wanaamini uwepo wake na uzoefu wake utasaidia kuongeza utulivu.” Profesa Rwekaza Mkandara.

Pinda alizima hoja ya Zanzibar ni nchi au siyo nchi, kaletwa kujaribu kuzima hoja ya Katiba mpya ni sasa au isubiri baada ya uchaguzi, je atafanikiwa? yetu macho na masikio.
Mizengwe, Pinda.
 
Mbona kama huyu Mzee ni kama wamemsusha sana? Mtu aliyewahi kiwa Waziri Mkuu wa Nchi inakuwaje anakuwa mjumbe wa kawaida kwenye kikosi kazi hiki? Yaani sasa anapokea maelekezo kutoka kwa Prof. Mukandala!
Sijui watu wa itifaki wanasemaje katika hili. Mimi kwa ufahamu wangu mdogo katika mambo haya naona haijakaa sawa.
 
Mkuu
Inategemea hekima katika nini!!

Je hekima ya kuchelewesha mchakato Ili ccm ishinde uchaguzi ujao?au hekima ya kuharakisha mchakato Ili wananchi wapate haki yao!!!


TUSUBIRI
Katiba mpya ndiyo itakufanya ushinde uchaguzi?
 
Moja wapo ni Zitto Kabwe anataka katiba isubiri 2025
Ameshabadilisha Gia angani kimya kimya. Msaka fursa yule hawezi kukaa upande usipmpa sifa. Alipoona CHADEMA wanapata sifa na yeye akajifanya watu hawakumuelewa. Soma maoni ya chama chake utaona alivyonadilika na yeye anataka Katiba mpya kabla ya 2025.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom