Tetesi: Siri ya TANESCO kupandisha umeme kuanzia January ni kulipa deni la IPTL

Watu walishasema watakao bebeshwa huo mzigo wa kulipa hayo madeni ni wananchi.
Ni heri warudishe service charge kuliko hiki kitu wanachotaka kufanya.
Tuubebe tu ndo tupate akili maana hakuna namna. Wakati Kafulila analipigania hili suala bungeni watu walikuwa wanamkejeli kwamba katumwa. Haya, sasa Std Chartered Bank na IPTL nao wametumwa tuone kama mtabisha. Ili tukae sawa na deni liwahi kuisha kila anayetumia umeme anunue unit kwa shilingi 3000/-
 
Duuuh mkuu ni laana sana kuzaliwa kwenye nchi yenye maamuzi ya hovyo kama Tanzania
 
Is getting too much ila hakuna namna, tulipe tu. Watanzania hatuna utamaduni wa kufanya maandamano ya kupinga 'mambo ya hovyo' kushinikiza viongozi kuwajibika,hatuna uchungu na kodi zetu ambazo serikali & Co wanazitapakanya hovyo na kukwapua. Hadi siku watu wengi watakapokuwa tayari kupigania Taifa lao, naamini hata vyombo vya dola vitakuwa upande wa wananchi.

KADA
 
Yes of course
 
Ccm Haina Huruma Jamani
Tuliyoaminishwa Ndiyo Yale Yale Ya Vat Tafsiri Nyingi Zikatolewa Mwisho Jibu Zuri Na Murua Ni Kuwa Mlaji (Mwananchi) Ndiyo Mlipaji Madeni Yote Wasomi Wetu Kimya Ukiwaona Kwenye Tv Wanasema Jpm Yupo Vemno.

Fukua Makaburi Tuone Ikiwa Utayafukuwa Kwa Maslahi Ya Taifa Hakika Wananchi Watakuunga Mkono
 
Mbona hilo lilikuwa linajulikana,kula wale wao mzigo abebeshwe mnyonge.
 
TAARIFA KWA UMMA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyotolewa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu ombi la kurekebisha bei za umeme kwa mwaka 2017.

Ombi la mabadiliko ya bei za umeme liliwasilishwa EWURA kulingana na Agizo la kubadilisha bei za umeme la mwaka 2016 lililoanza kutumika tarehe 1 April 2016. Ifahamike kuwa bei za umeme (Electricity Tariffs) zinazotumika zilitolewa zitumike mpaka tarehe 31/12/2016, hivyo itakapofika Januari 2017, inatakiwa bei mpya za umeme (New Electricity tariff) kutolewa kwa mujibu wa sheria.

Hivyo TANESCO ilitakiwa kufanya tathmini ya gharama za uzalishaji , usafirishaji na usambazaji umeme na kupeleka mapendekezo hayo kwenye Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA), ili kupitiwa na kufanyiwa taftishi(kupata maoni ya wadau) ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushauri la Serikali . Hivyo basi ikiwa bei za umeme zitapanda au kutopanda, hiyo itategemea na mapitio ya tathmini ya gharama za kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme tulizo wasilisha EWURA.

TANESCO haiwezi kuamua yenyewe kupandisha au kutopandisha bei za umeme. Kwa mujibu wa sheria, EWURA inapaswa ifanye mapitio ya bei za umeme kwa kila robo mwaka (Periodic Tariff Adjustment).

Tunapenda Umma ufahamu kuwa kupanda au kushuka kwa gharama za umeme ni suala la kisheria na ni jambo la kawaida kwani bei ya umeme imeshawahi kushuka katika vipindi tofauti kwa mfano Mwaka 2015 (robo ya kwanza ya mwaka) bei ilishuka kwa asilimia 2.5. Vivyo hivyo Mwezi Aprili mwaka 2016 pia gharama za umeme zilishuka kwa asilimia 1.6

IMETOLEWA NA: Mhandisi FELCHESMI MRAMBA
Mkurugenzi Mtendaji
Shirika La Umeme Tanzania (TANESCO)
08 Novemba 2016

Tanesco yetu tarehe 11/08/2016
 
Haaaah uo ni utetezi thaifu mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…