Na alisema Serikali itauza Umeme nchi ya Ethopia Yani TZ itaanza ku export Umeme kwenye Ethopia sasa kikowapi kuanza kupandisha bei ya Umeme ?
(a) Miradi ya Uzalishaji umeme
Ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme na kukidhi mahitaji ya uchumi wa viwanda, Serikali imekamilisha ujenzi wa mitambo ya Kinyerezi I (MW 150) Mwezi Machi, 2016 na katika kipindi cha Mwaka 2016/17 ujenzi wa mitambo mipya ya
Kinyerezi I Extension (MW 185) unatekelezwa kwa gharama za Dola za Marekani Milioni 188 na
Kinyerezi II (MW 240) unatekelezwa kwa kiasi cha Dola za Marekani Milioni 344.
(b) Miradi ya Njia za Usafirishaji Umeme.
Ili kuenda sambamba na miradi ya kuzalisha umeme, Serikali kupitia TANESCO inatekeleza miradi kadhaa ya kusafirisha umeme. Miradi hiyo ni kama ifuatavyo:-
i.
Mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga (backborne) ambapo upo katika hatua za mwisho kukamilika. Mradi huu utaimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo ya Kanda ya Ziwa, Kati na Kaskazini. Mradi huu umekamilika kwa
asilimia 98; ambapo utatekelezwa kwa
kiasi cha Dola za Marekani Milioni 490;
ii.
Mradi wa kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea wa msongo wa kilovoti wa 220 wenye urefu wa kilomita 250 pamoja na kusambaza umeme katika mikoa ya Njombe na Ruvuma. Kazi zinazoendelea ni ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme, kwa upande wa njia ya kusafirisha umeme, kazi zinazoendelea ni usanifu wa kina (
Detail Feasibility Study), uingizwaji wa vifaa vya ujenzi na uandaaji wa eneo la mradi (
Site Moblization). Mradi wa kusafirisha umeme wa Makambako Songea utatekelezwa kwa
kiasi cha Dola za Marekani milioni 190;
iii.
Miradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 1,148 kutoka Mbeya - Sumbawanga - Kigoma - Nyakanazi (North - West Transmission Line);
iv.
Mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 yenye urefu wa kilomita 664 kutoka Dar es Salaam - Chalinze – Tanga - Arusha (North - East Transmission Line) ambapo zaidi ya Dola za Marekani Milioni 55 zitatumika kuteleza mradi huu. Mkopo wa kiasi hicho cha fedha zimepatikana kutoka katika benki a Exim ya China. Kazi zinazoendelea kwa sasa ni kuweka mipaka kwenye njia ya kusafirisha umeme;
v.
Mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Somanga fungu hadi Dar es Salaam (Kinyerezi), gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 150. Kwa sasa Serikali inatafuta fedha za kutekeleza mradi husika;
vi. Pia Serikali inatekeleza miradi ya Kikanda kama vile miradi ya
kusafirisha umeme kutoka Zambia - Tanzania – Kenya (ZTK). Lengo la miradi hii ni kuweza kuimarisha upatikanaji wa umeme katika eneo la Afrika Mashariki pamoja na kuimarisha biashara ya kuuziana umeme.
Aidha, mradi huu unatekelezwa kwa sehemu, ambapo itajengwa njia ya kusafirisha umeme kutoka Namanga (mpakani kati ya Tanzania & Kenya) hadi Singida yenye urefu wa kilomita 414 ambapo itagharimu kiasi cha
Dola za Marekeni Milioni 258 ambapo wafadhili wa mradi huo ni AfDB na JICA, njia ya kusafirisha umeme kutoka Singida hadi Iringa (mradi huu wa backborne upo katika hatua za mwisho kukamilika), njia ya kusafirisha umeme kutoka Iringa hadi Mbeya yenye urefu wa kilomita 292 pamoja na ujenzi wa
substations mbili (2) (mradi utagharimu
kiasi cha Dola za Marekani takribani Milioni 200), na sehemu ya mwisho ni njia ya kusafirisha umeme kutoka Mbeya hadi Tunduma yenye urefu wa kilomita 100 itagharimu
Dola za Marekani 38 Milioni.
(c) Miradi ya Njia za Usambazaji umeme.
Serikali kupitia TANESCO imeendelea kutekeleza miradi kadhaa ya kuimarisha miundombinu ya kusambaza na kusafirisha umeme katika Majiji na Miji hapa nchini, ambayo ni;
i. Mradi wa kuimarisha upatikanaji wa umeme katika Jiji la Dar es Salaam ambapo ujenzi wa kituo cha kupoza umeme katikati ya Jiji upo katika hatua za mwisho za kukamimilika (
Improving the Electricity Power Supply relability in City of Dar es Salaam), ambapo mradi huu
unafadhaliwa na Serikali ya Finland pamoja na Serikali ya Tanzania kwa kiasi cha Euro Milioni 28.2.
ii. Pia mradi mwingine wa kuboresha miundombinu ya usambazaji umeme unaofadhaliwa na Serikali ya Japani unaendelea kutekelezwa katika Jiji Dar es Salaam.
Kiasi cha Dola za Marekani Milioni 38 zitatumika kutekeleza kazi hiyo.
iii.
Mradi wa Tanzania Energy Development and Access Project (TEDAP) unatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro. Mradi unakusudia kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mikoa husika . Mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza, kusafirisha pamoja na vituo vya kupoza umeme.
Kiasi cha Dola za Marekani Milioni 26.44 zitatumika kutekeleza mradi huu pindi utakapokamilika.
Kwa kuzingatia kuwa azma ya Serikali ni kufikia uzalishaji wa umeme wa Megawati 5,000 ifikapo 2020 na Megawati 10,000 ifikapo 2025. Serikali ilianzisha mkakati maalum wa kuongeza uwekezaji katika miradi ya kuzalisha umeme ambayo inatekelezwa kwa kushirikiana na sekta binafsi kutoka ndani na nje ya nchi.
(a) Miradi ya uzalishaji ni kama ifutayo:-
i. Miradi midogo ya Nishati Jadidifu (
Renewable Energy) yenye MW 16.29 imetekelezwa na sekta binafsi, miradi hiyo ni;-
· Miradi midogo ya kuzalisha umeme wa maji (
Min Hydropower) ambayo ni Uwemba - MW 0.84; Mwenga MW 4; na Yori MW 0.95; na
· Miradi midogo ya kuzalisha umeme kwa kutumia tungamo taka (
Biomass) ni Tanwat MW 1.5 na TPC MW 9.0.
ii.
Kilwa Energy Gas Fired Plant (371.2 MW) - US$ Milioni 465,
Mwekezaji yupo katika hatua za mwisho za majadiliano ya Mikataba mbali mbali ambayo ni; Mkataba wa nyongeza wa utekelezaji (
Addendum to Implementation Agreement), Mkataba wa Ubia (
Shareholders Agreement), na Mkataba wa kununua gesi asilia (
Direct Gas supply Agreement) ili kupata ufadhali wa mradi.
(b)Miradi ya usafirishaji umeme
Uwekezaji kwenye miundombinu ya usafirishaji wa umeme ni jukumu la Serikali na si sekta binafsi. Aidha, Sheria ya umeme ya Mwaka 2008 inaruhusu sekta binafsi kupitisha umeme kwenye miundombinu hiyo kwa kulipia
Wheeling Charge na wala si kumiliki miundombinu husika.