Siyo hiyo tu mkuu, Mimi nina rafiki yangu alisikia kanisa fulani jirani limeanzishwa. Tena wanajitangaza kwenye redio na kuwaita wagonjwa na wenye shida mbalimbali waende wakaombewe na kuponywa bure. Jamaa yangu kusikia hivyo si akaenda. Alipofika aliambiwa Kuna huduma ya mwana wa nabii anaonana na mtu mmoja mmoja, alichoambiwa ni kuwa shetani ameyapiga sana maisha yake, na asipo angalia atapata matatizo makubwa sana kwenye maisha yake kwasababu (huyo muhubiri) ameonyeshwa na Mungu kuwa kuna jirani yake anamroga. Jamaa yangu akamwambia naomba unisaidie mtumishi. Huyo mtumishi akamwambia, "unatakiwa utowe shilingi elfu 86 ili nikuombee na nikupe maji ya baraka na mafuta ya upako."
Tena kanisa lenyewe lipo Tabora mjini maeneo ya Ipuli, wanajiita Wana wa nabii Elisha Muliri. Watu wengi wametapeliwa hapo,