Sisi ambao hatutekwi na Wahubiri Waongo wa Miujiza ndiyo hatuna Akili au waliotekwa nao ndiyo hawana kabisa Akili?

Sisi ambao hatutekwi na Wahubiri Waongo wa Miujiza ndiyo hatuna Akili au waliotekwa nao ndiyo hawana kabisa Akili?

Sadaka siyo mali ya padri inakwenda jimboni na kutolewa kwa utaratibu maalum tofaut na walokole sadaka anachukua mchungaji anafanya anavotaka
Jimboni zikifika zinajenga shule na hospitali za bei mbaya ambazo wakatoliki mnarudi humu kupiga kelele tena kuwa hamzimudu ni kwa ajili ya matajiri hazisaidii wakatoliki maskini !!!what a paradox!!!
 
Tumedanganywa kwa Muda Mrefu sana. Kama Mungu angekuwa Ana Dini Pasingekuwa na Dini Tofauti tofauti zinazotofautiana

Ukiona Hivyo Hakuna Mungu hapo Bali ni Binadamu na Vitu vingine vinachanganya Kichwa chako ili viweze Kukutawala

Hakunq Mungu Mwenye Dini Tofauti tofauti unazoziona Leo hii . HAYUPO
Nilikuwa najiona kuwa labda nipo peke yangu mwenye ufahamu huu na kujitambua, kumbe tupo wengi. Ukiwaangalia watu wanavyopurukushwa sadaka hadi unawahurumia na kujazwa matango pori vichwani.
 
I wish Ulimwengu mzima ungekuwa na mtazamo huu. Dunia ungekuwa sehemu salama sana. Lakini walio wengi ambao hawajitambui ndio wameshatekwa na makanjanja wachache. Mtu anaamini amnyime jirani yake ambae ni maskini msaada ila ampelekee kanjanja fulani huko kanisani akimuaminisha ataingia uzima wa milele huku huyo anaekwambia hivyo hataki kujishulisha anategemea wewe uende ndio ale na kubadilisha magari. Ujinga hautoisha daima
Watanzania wamefikia Hatua. Wanapookolewa kwenye Ajali ya Gari na Binadamu mwenzake ila Wanaenda Kwa Mchungaji kumpa Sadaka za Shukurani na Huyo Mchungaji anaenda Kuzinywea Pombe na Starehe na Kujijenga Kiuchumi

Kwanini Usiende Kumpatia Aliyekuokoa kwenye Hiyo Ajali au Aliyekuona Umebanwa na Mlango pale kwenye Ajali akakutoa. Huyo aliyekuokoa Ni Binadamu mwenzako na Aliyeumbwa na Mungu. Eti ww unakimbilia Kwa mchungaji wako Kutoa Sadaka . Tumepotea sana Binadamu
 
Nilikuwa najiona kuwa labda nipo peke yangu mwenye ufahamu huu na kujitambua, kumbe tupo wengi. Ukiwaangalia watu wanavyopurukushwa sadaka hadi unawahurumia na kujazwa matango pori vichwani.
Ukiona Watu wanatafuta Ukweli kwa Muda Mrefu ujue Hapo hakuna Ukweli.

Hakuna Ukweli unaotafutwa miaka zaidi ya 2000 na Haupatikani. Ukweli hauwezi kuchukua hata Miaka miwili.

Watu tumepotoshwa sana. Miaka na Miaka watu wanatafuta Uponyaji na Hawaupati. Nyumba Zinazosema Zinatoa Mapepo na Majini ndizo zimejaa Majini na Mapepo humo humo

Kama Hayo majini na Mapepo yangekuwa yanatolewa kweli basi Hizo nyumba za Ibada zisingeweza kusogelewa na Mtu mwenye hayo Mapepo. Wangekuwa wanakamatwa kwa Nguvu na Kamba juu Wanapelekwa humo ila Wanaenda Wenyewe tu bila Shida na Kila Siku wanaudhuria Ibada
 
Sikiliza ukisali usiangalie mwingine anasalije Yesu alieleza kuhusu likiongozi moja farisayo la dini ambalo lilijipiga kifuani kwa majigambo kuwa mimi huwa sisali staili kama yule mtoza ushuru staili yangu super!!! Mtoza ushuru kwa staili yake ya kinyonge isiyokuwemk kwenye liturijia ya dini ya kifarisayo akalia akasema nisamehe mimi nisiyestahili sala yake ikasifiwa lifarisayo likalaaniwa

Unaposali hangaika na sala zako mwingine anasalije achana naye

Ndio maana katiba imetoa Uhuru wa kuabudu bila kuuingilia
 
Nimeshakujibu. Mungu hayupo Hivyo

Mungu haitaji Sadaka yako Yeyote. Ushajiuliza Sadaka Inamsaidiaje Mungu unapoitoa.

Mungu ni Mkamilifu Haitaji sadaka Yako maana Yeye Si Kiumbe Kama Wewe ulivyo. Hizo sadaka na Dhabihu zinaishia Hapa Hapa Duniani kwa Binadamu Wenzako unaowapa kwa Kutokujua kwamba Wameweka Misingi hiyo ili wawatawale Akili zenu.

Maana Hata Kwenye Biblia Sadaka za Agano la Kale si Sadaka za Agano Jipya. Mungu wa Agano la Kale hafanani kitabia na Mungu Wa Agano jipya

Kama unatumia Biblia, unaitumiaje wakati huiamini? Huoni kama wewe ni bonge la confuser?
 
Si ndio hapo sasa, Mungu si Kiumbe sasa Sijui anaongea na Nani.

Yaani hawa Wanaojiita Manabii wanawadanganya Sana. Eti ameongea na Mungu
Kuna wanaoamini Mungu ni mtu wanaongea naye wengine mizimu wanaongea nayo au wewe ndio unataka uwapangie waongee na Mungu yupi?

Mungu aliposema usiabudu miungu wengine alijua wapo sasa wewe unaposema wanaongea na Mungu yupi hujui kuwa IPO miungu mingi?
 
Jimboni zikifika zinajenga shule na hospitali za bei mbaya ambazo wakatoliki mnarudi humu kupiga kelele tena kuwa hamzimudu ni kwa ajiki ya matajiri hazisaidii wakatoliki maskini what a paradox!!!
Ndio hizo kina St nani Sijui St Nani. Ambazo zimejengwa na Masikini wa Makanisa Husika wanaotoa sadaka na Kupeleka Barua za Xmas na Pasaka n.k n.k. Ambao wanakuja Tena Kuzipongeza Zimefaulisha Vizuri wakati watoto wao hawajawahi hata Kugusa Geti la Shule hizo

Binadamu tubadilike tuwe na Akili Timamu. Wewe ukipokea Mshahara wako ukikatwa Unaambiwa Utakusaidia Katika NHIF..NSSF na Ukizeeka Baadae Unapewa Kiinua Mgongo

Sasa Sadaka Tunajua Hazifiki kwa Mungu ila hakuna Sehemu Muumini anaambiwa Kwa Sababu ya Sadaka zako basi Faida zake ni Hizi na Hizi
 
Anaongea akiwa wapi na nani ,
Kama hata hujui kuna Mungu anayejibu na kuongea, wewe hii mjadala haukufai. Ninaongea na mtu aneyekwenda anayesali kwa Mungu muumba wa mbingu na nchi , lakini pengine kapungukiwa na maarifa ya kumjua huyu Mungu. Lakini wapagani, hapa siyo mahala sahihi kwa level yenu. Unahitaji darasa lingine.
 
Kama unatumia Biblia, unaitumiaje wakati huiamini? Huoni kama wewe ni bonge la confuser?
Unatakiwa Kujiuliza Kabla ya Biblia Mungu hakuaminiwa!? Au ulikuwa Humuamini Mungu kabla Hujaijua Biblia. Wazee wako walikuwa wanaishije Sasa au wao walikuwa hawajaumbwa na Mungu.. Maana Biblia ni ya Juzi tu na Tanzania imekuja baada ya Wakoloni kuja

Biblia Ni Vitabu vilivyoandikwa na Watu na Wengine hata Walikuwa si Watu wa Mungu ila Ni Waandishi tu wa Kawaida
 
Utaratibu maalumu au Siyo!!. Huo Utaratibu ushakusaidia Kitu gani Kama Muumini!?

Ukiajiriwa Sehemu Mwajiri atleast anakuambia Atakupelekea Michango NSSF,NHIF n.k huko Kanisani Hizo Sadaka Zishakukatia Hata Bima Ya Afya ... bima za Moto. Bima za Maisha. Bima za Ajali n.k

Hakuna Sadaka inayoenda Kwa Mungu hata mara Moja maana Mungu hayupo hivyo. Hizo sadaka zinaenda Kwenye Account za Watu waliojiwekea Organization maalumu ya Kuzicontrol halafu ww unakuja Kutetea Humu wakati hizo sadaka hazikusaidii chochote kile katika Maisha Yako. Ukiugua Hakuna Kanisa wala Padri anachanga Kuugua Kwako zaidi ya Kuja Kukuombea. Wakat wao wakiugua Ww Unachanga Pesa Wakatibiwe

Huo Utaratibu maalumu ungekuwa ni wakuwawezesha Waumini wafaidike na Sadaka zao maana Tunajua Sadaka haziendi kwa Mungu zinaenda Kwenye Account za Kanisa. Mwisho wa siku Sadaka Hazileti matokeo kwa Muumini Husika na Hakuna Muumini Anayepata Faida ya Sadaka zake moja Kwa Moja Zaidi ya Kupigwa pigwa chenga ya Kusema UNAMTOLEA MUNGU
Tofauti ipo, huku kwingine na brain wash inatumika sana yaani mawazo ya mtu mmoja tu ndo yatumike Sasa mtu uchukuliwe uchumi unaotafuta kwa jasho kama maagizo ya Mungu bado naakili yako uambiwe isutumike ila utumie akili ya mtu mmoja na pale unajiongeza kutumia akili yako unaambiwa hiyo ni dhambi mfano umeamka Asubuhi unahela kidogo ya mlo mmoja tu unaambiwa uende nayo kanisani ukatoe yote alafu ushinde na njaa na kesho ukose nauli na nguvu ya kwenda kazini usubiri kunguru atakudondoshea hela bila kufanya kazi yoyote ya kuingiza kipato wakati huyo mwingine angeenda kwenye ibada yake masaa machache na asitoe chochote na akiwaeleza Wana wanamuelewa siku hiyo yupo vibaya.
 
Si ndio hapo sasa, Mungu si Kiumbe sasa Sijui anaongea na Nani.

Yaani hawa Wanaojiita Manabii wanawadanganya Sana. Eti ameongea na Mungu
Siyo hiyo tu mkuu, Mimi nina rafiki yangu alisikia kanisa fulani jirani limeanzishwa. Tena wanajitangaza kwenye redio na kuwaita wagonjwa na wenye shida mbalimbali waende wakaombewe na kuponywa bure. Jamaa yangu kusikia hivyo si akaenda. Alipofika aliambiwa Kuna huduma ya mwana wa nabii anaonana na mtu mmoja mmoja, alichoambiwa ni kuwa shetani ameyapiga sana maisha yake, na asipo angalia atapata matatizo makubwa sana kwenye maisha yake kwasababu (huyo muhubiri) ameonyeshwa na Mungu kuwa kuna jirani yake anamroga. Jamaa yangu akamwambia naomba unisaidie mtumishi. Huyo mtumishi akamwambia, "unatakiwa utowe shilingi elfu 86 ili nikuombee na nikupe maji ya baraka na mafuta ya upako." Jamaa akamwambia kwasasa Nina matatizo naomba uniombee, then baadae ntakuketea nikauze kitu changu, au naomba bas nikuachie hata simu yangu kama bondi then nikileta hiyo pesa utanirudishia, alichojibiwa ni kuwa mbona kwa waganga hamuendi bure, hivi ingekuwa ni kwa mganga ungeenda bila pesa, nenda katafute hiyo pesa kwanza ndo nije nikuombee. Ndio Hayo yaliyotokea jamani, dini imekua biashara
Tena kanisa lenyewe lipo Tabora mjini maeneo ya Ipuli (kanisa la maturubai), wanajiita Wana wa nabii Elisha Muliri. Watu wengi wametapeliwa hapo,
 
Unatakiwa Kujiuliza Kabla ya Biblia Mungu hakuaminiwa!? Au ulikuwa Humuamini Mungu kabla Hujaijua Biblia. Wazee wako walikuwa wanaishije Sasa au wao walikuwa hawajaumbwa na Mungu.. Maana Biblia ni ya Juzi tu na Tanzania imekuja baada ya Wakoloni kuja

Biblia Ni Vitabu vilivyoandikwa na Watu na Wengine hata Walikuwa si Watu wa Mungu ila Ni Waandishi tu wa Kawaida
Wewe unaanzisha imani yako isiyoamini katika Maneno ya Biblia? Kama ndiyo sema ndiyo usipindishe pindishe. Nyooshsa maelezo ili tuende pamoja kwa sababu Ukristo huwezi kuupindisha ukaufanya unachotaka wewe kiwe.
 
Siyo hiyo tu mkuu, Mimi nina rafiki yangu alisikia kanisa fulani jirani limeanzishwa. Tena wanajitangaza kwenye redio na kuwaita wagonjwa na wenye shida mbalimbali waende wakaombewe na kuponywa bure. Jamaa yangu kusikia hivyo si akaenda. Alipofika aliambiwa Kuna huduma ya mwana wa nabii anaonana na mtu mmoja mmoja, alichoambiwa ni kuwa shetani ameyapiga sana maisha yake, na asipo angalia atapata matatizo makubwa sana kwenye maisha yake kwasababu (huyo muhubiri) ameonyeshwa na Mungu kuwa kuna jirani yake anamroga. Jamaa yangu akamwambia naomba unisaidie mtumishi. Huyo mtumishi akamwambia, "unatakiwa utowe shilingi elfu 86 ili nikuombee na nikupe maji ya baraka na mafuta ya upako."
Tena kanisa lenyewe lipo Tabora mjini maeneo ya Ipuli, wanajiita Wana wa nabii Elisha Muliri. Watu wengi wametapeliwa hapo,
Maji ya Baraka ni lugha ya Warumi, si lugha ya Wakristo.
 
Kuna wanaoamini Mungu ni mtu wanaongea naye wengine mizimu wanaongea nayo au wewe ndio unataka uwapangie waongee na Mungu yupi?

Mungu aliposema usiabudu miungu wengine alijua wapo sasa wewe unaposema wanaongea na Mungu yupi hujui kuwa IPO miungu mingi?
Sasa Wao wanaifananisha Na Mungu muumba wa Vitu Vyote aliyekataza unayosema wewe. Wao ndio wanasema wameongea naye

Hata Mashetani,majini na Malaika wapo wanaojiita Miungu labda wanaongea na Hao ndio wanatuletea Mambo yao humu
 
Unafanya vyema. Kanisani kwenu mna raslimali zozote za kanisa labda? Kanisani kwenu pia kuna wajane na yatima? Huwa mnawahudumiaje?
Kanisalni kwenu mna vyombo vya kuhubiria? Mnavipataje na mnavitunzaje?
Kanisani kwenu kuna watu mmeajiri mfano walinzi, wafanya usafi, watu wanaokaa kanisani kwa masuala ya utawala labda. Hao watu huwa mnawahudumia namna gani kama wapo?
Sijajua kanisa unaloshiriki. Ningependa pia kujua mna makanisa mangapi ya aina hiyo na huwa mnayaanzisha namna gani?
Unajua kushirikishana ni kuongezeana maarifa. Naomba unisaidie.
Sasa hapo sikuwajulisha tu watu kwa Upendo watoe hela kwaajili ya hizo huduma zinazofanya wapate sehemu ya kukusanyika na kuwa pamoja kwenye shida na raha na siyo kuwaambia wanampa Mungu hivi Kuna mtu anaweza kumpa Mungu sadaka za pesa? Alafu aanze tena kumuomba Mungu Pesa? Maana yake Mungu ni mwenye uwezo wa Kila kitu anachohitaji ni Imani ya mtu tu kumwamini kama yupo na mambo ya sadaka za pesa ni mambo yetu wanadamu na ndo maana Kuna watu wakisema Leo sinahiyo pesa ya kutoa huyo aliyekuwa anategemea hiyo pesa ananuna na kuchukia kwa matarajio yake kukwama.
 
Kweli nimeamini ukristo ni din kubwa sana chin ya jua coz kila leo unajadiliwa sana kuliko din yoyote ile mfano dini ya kiislam lini imeongelewa humu??!!
 
Wewe unaanzisha imani yako isiyoamini katika Maneno ya Biblia? Kama ndiyo sema ndiyo usipindishe pindishe. Nyooshsa maelezo ili tuende pamoja kwa sababu Ukristo huwezi kuupindisha ukaufanya unachotaka wewe kiwe.
Sijapindisha Kitu nimekuuliza Kabla Ya Biblia wewe Ulikuwa Kiumbe cha Nani!? Maana Biblia nayo ina Errors nyingi tu za Kimaandishi.

Jiulize mwenyewe wewe Kabla ya Biblia ulikuwa ni nani au Hao wazazi wako na Ma babu zako walikuwa Viumbe wa Nani. Maana Najua Bila Biblia usingejua hata kama Kulikuwa na Sodoma na Gomora.

Mungu hakuandika Kitabu chochote Kile kwahiyo usijiweke akili yako kwenye Kitabu
 
Sasa hapo sikuwajulisha tu watu kwa Upendo watoe hela kwaajili ya hizo huduma zinazofanya wapate sehemu ya kukusanyika na kuwa pamoja kwenye shida na raha na siyo kuwaambia wanampa Mungu hivi Kuna mtu anaweza kumpa Mungu sadaka za pesa? Alafu aanze tena kumuomba Mungu Pesa? Maana yake Mungu ni mwenye uwezo wa Kila kitu anachohitaji ni Imani ya mtu tu kumwamini kama yupo na mambo ya sadaka za pesa ni mambo yetu wanadamu na ndo maana Kuna watu wakisema Leo sinahiyo pesa ya kutoa huyo aliyekuwa anategemea hiyo pesa ananuna na kuchukia kwa matarajio yake kukwama.
Una Akili Timamu
 
Back
Top Bottom